• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC Malima awataka Madiwani kusimamia miradi ya maendeleo.

Posted on: June 10th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara Bi. Lena Nkaya kushirikiana na  Madiwani wa Halmashauri yake katika kusimamia miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Halmashauri hiyo kwa lengo la kuongeza chachu ya ubora na ukamilishaji wa miradi hiyo kwa wakati.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima (katikati) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Kilombero Mhe. Danstan Kyobya (kulia), Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Ifakara Bi. Lena Nkaya na viongozi wengine kwenye eneo la ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya Mlimba.

Mhe. Malima ametoa agizo hilo Juni 9 mwaka huu wakati akizungumza na Madiwani kwenye Mkutano maalum wa kupitia hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali - CAG uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima akitoa maelekezo wakati akikagua ujenzi wa jengo jipya la Halmashauri ya Mlimba.

Akiongea wakati wa Mkutano huo Mkuu wa Mkoa amesema suala la usimamizi wa miradi katika Halmshauri hiyo ni wa kusua sua na kubainisha kuwa Diwani ndiye msimamizi wa miradi ya maendeleo katika eneo husika.

Kwa sababu hiyo, Mkuu wa Mkoa amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Ifakara kuratibu namna Madiwani watakavyosimamia miradi katika maeneo yao.

"...sasa msimamizi mkuu wa miradi ni Mhe. Diwani, kwa hiyo Mkurugenzi nisikilize vizuri sana hili ni agizo la Mkuu wa Mkoa mimi, kwamba muorodheshe miradi yote inayo kwama kisha kwenye kila mradi kuwe na wasimamizi Madiwani wanne wanne..."
amesema Mkuu wa Mkoa.

Muonekano wa jengo jipya Wilayani Kilombero ambalo linaendelea kujengwa.

Aidha, Mhe. Adam Malima ametaja miradi ambayo Madiwani hao wanatakiwa kuisimamia kuwa ni pamoja na  miradi ya maji, afya, elimu na barabara za TARURA.

Akisisitiza zaidi, Mhe. Malima amesema Mkurugenzi wa Halmashauri atahusika  katika kuratibu na kugharimia safari za Madiwani hao  ili mradi tu wahe. Madiwani waweze kufanikisha zoezi hilo.

Kwa upande wake Mkaguzi wa nje na mdhibiti wa Hesabu za Serikali Mkoa wa Morogoro CPA Peter Mwabwanga amemshukuru na kumpongeza Mkuu wa Mkoa katika harakati zake za kuzirekebisha Halmshauri za Mkoa huo katika ukusanyaji wa mapato na ukamilishaji wa miradi ya maendeleo  na kukili kuwa juhudi hizo zinaonesha nia yake njema ya kuwaletea Wananchi wa Mkoa huo maendeleo.

Nae Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro Ndg. Solomon Kasaba amewataka Madiwani wa Halmashauri hiyo kushirikiana na Uongozi wa Mkoa na Wilaya katika harakati za kuwaletea Wananchi maendeleo bila woga.

MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.