Serikali Mkoani Morogoro imeazimia kuendeleza viwanda ili kutoa ajira katika kada mbalimbali na kuwezesha bidhaa za wajasiriamali kushindana katika masoko ya ndani, kikanda na kimataifa hivyo kuijenga Tanzania yenye uchumi endelevu wenye nguvu imara na wenye ushindani.
Hayo yamebainishwa Mei 24 Mwaka huu na Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Albinus Mgonya wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa wajasiriamali wachakataji, wauzaji na wasambazaji wa viungo vya chakula kutoka Mkoani Morogoro, yaliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chief Kingaru katika Manispaa ya Morogoro.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.