• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

SERIKALI YAAGIZA WANANCHI WANAOISHI BONDENI KUHAMA.

Posted on: May 18th, 2021

Serikali Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro imewataka wananchi  wanaoishi mabondeni kuhamia katika maeneo maalumu yaliyotengwa  na Halmashauri hiyo  ili kuepukana na athari za maafa ya mafuriko.

Hayo yamebainishwa Mei 18, 2021 Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro  na Mkuu wa wilaya hiyo Mhe. Adam Mgoyi wakati wa ufunguzi wa semina ya siku tatu ya kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maafa yatokanayo na mafuriko.

‘’Natoa wito kwa wananchi wanaojenga katika mapito ya maji wanazuia  maji kufuata mkondo wake na kusababisha maafa ya mafuriko, lakini pia wa mabondeni wahamie maeneo ya miinuko, waliojenga kwenye maeneo ya kilimo na waliogeuza maeneo ya kilimo kuwa makazi baadala ya kujenga makambi ya muda kwa ajili ya kusimamia mashamba yao warudi katika maeneo tuliyowapatia’’ amesema Mgoyi

Mgoyi amebainisha kuwa kumekuwepo na utamaduni wa wananchi kutaka fidia maafa yanapotokea bila kutambua wao ni sehemu ya visababishi vya maafa hayo huku akiwasistiza kutokuwepo fidia kwa mwananchi ambaye atakaidi maagizo ya Serikali.

Sambamba na hayo, amefafanua kuwa Serikali Wilayani humo  imeanza mpango mkakati wa kuhuisha miundombinu ya maji ili kusaidia kukabiliana na kasi ya maji ambayo inaleta athari kwa wananchi Wilayani humo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Waziri Mkuu Kituo cha Oparesheni Mawasiliano ya Dharura, Ndg.  Selestine  Masalamado, amewataka wananchi Wilayani humo kuchukua hatua za kupunguza athari za maafa zikiwemo kutochimba madini kando ya mito, kutofanya shughuli za kilimo na ufugaji kando ya mito hiyo.

Naye Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) ambaye pia ni Mratibu wa Usimamizi wa maafa Mkoa wa Morogoro, Anza Ndossa  amebainisha kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa wananchi hao kwa kuwa Wilaya ya Kilosa ina kata 40 huku 11 kati ya hizo zinaathirika na mafuriko ambapo kijiji cha Kitete huathiriwa sana na maafa,  ambapo Machi 2020 kaya  takribani kaya 791 ziliathirika kwa maafa ya mafuriko.

Akizungumza kwa niaba ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji (IOM), Reuben Mbugi ameihakikishia Serikali yaTanzania  kuwa wataendelea kushirikiana nao katika kuijengea jamii uwezo wa kukabiliana na maafa yatokanayo na mafuriko.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti  wananchi wa  Kichangani, Tindiga na Changarawe wameishukuru serikali kwa kuendesha elimu hiyo ambayo itawasaidia katika kujenga uwezo wa kujiandaa, kuzuia na kukabili maafa ya mafuriko iwapo yatatokea.

Ofisi ya Waziri Mkuu Idara ya Uratibu wa Maafa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Kilosa chini ya Ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wahamaji (IOM), wanatoa Elimu kwa Umma inayolenga kuongeza uelewa wa jamii kuhusu maafa yatokanayo na  mafuriko katika kata  tano za wilaya hiyo zilizo katika hatari zaidi ya kuathirika na maaafa ya mafuriko.


MWISHO


 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.