• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

TAASISI ZA KIDINI MOROGORO ZAPONGEZWA KATIKA KULETA MAENDELEO.

Posted on: March 20th, 2023

Kufuatia jitihada mbalimbali zinazofanywa na taasisi za kidini hapa nchini katika kuwahudumia wananchi, Serikali imezipongeza na kuzihamasisha taasisi hizo kuendelea na juhudi hizo za kuwaletea maendeleo wananchi wake.

Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Mhe. Shaka Hamdu Shaka (kulia) akiwa pamoja na Shekhe Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu wa Ahmadiyya nchini wakisikiliza salamu kutoka kwa viongozi wa dini kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 134 ya kuzaliwa kwa Jumuiya ya Ahmadiyya. 

Pongezi hizo zimetolewa Machi 19 mwaka huu na Mkuu wa Wilaya  ya Kilosa  Mhe. Shaka Hamdu Shaka kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa wakati akizungumza na viongozi wa dini pamoja na wananchi kwenye hafla ya kuadhimisha miaka 134 ya kuanzishwa kwa Jumuiya ya Waislamu  wa Ahmadiyya hapa nchini iliyofanyika katika viwanja vya msikiti wa Ahmadiyya uliopo katika Manispaa ya Morogoro.

Mhe. Shaka amesema Serikali inatambua mchango na jitihada za taasisi za dini katika kufanikisha maendeleo ndani ya Mkoa huo na taifa kwa ujumla. Akitolea mfano Jumuiya ya waislamu  wa Ahmadiyya Mkoani Morogoro amesema Jumuiya hiyo  imekuwa ikichangia kwa kiasi kikubwa maendeleo ya nchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo elimu, afya, na maji kwa kuchimba visima katika maeneo mbalimbali ndani ya Mkoa huo.

"...lakini Serikali inathamini namna ambavyo mnavyounganisha nguvu katika kuleta maendeleo na mfano mzuri ni kwa Jumuiya ya Ahmadiyya pamoja na madhehebu mengine..." amesema Mhe. Shaka Hamdu Shaka.

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya amewahakikishia viongozi wa dini Mkoani humo kuwa  Serikali itaendelea kuheshimu na kuthamini michango inayotolewa na taasisi hizo za kidini Ili kuongeza kasi ya kuwaletea wananchi Maendeleo.

Nae Shekhe Mkuu wa Jumuiya ya Waislamu Wa Ahmadiyya nchini Tanzania Bw. Tahir Mahmood Chaudhry ameishukuru na kuipongeza Serikali ya Tanzania kwa kuruhusu uhuru wa kuabudu, hivyo ni nchi ya kusifiwa na kujivunia kwenye hili kwa sababu zipo nchi duniani hazina uhuru wa kuabudu.

Kwa upande wake Shekhe Saidi Hamadi Kondo mwakilishi wa Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Shekhe Twaha Kilango amewataka viongozi wa dini, Serikali na Wazazi kushirikiana ili kupambana na vitendo vya ukatili kwa watoto, hivyo elimu itolewe kwenye nyumba za Ibada na mashuleni ili kuwakinga watoto hao dhidi ya vitendo hivyo.

Jumuiya hiyo ya Waislamu wa Ahmadiyya ilianzishwa mwaka 1886 na Leo imetimiza miaka 134 tangu kuanzishwa kwake, hafla ya maadhimisho hayo imehudhuriwa na wajumbe wa kamati ya Haki na Amani ya Mkoa, kamati ya Maridhiano ya Mkoa na Jumuiya ya Waislamu wa Bohora Mkoani humo.

 MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.