• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

Posted on: May 14th, 2025

Vyama vya ushirika hapa nchini vimetakiwa kuendana na maendeleo ya sayansi na teknolojia duniani, ambapo matumizi ya  Teknolojia ya Habari na Mawasikiano - TEHAMA yanatajwa kuwa ni njia bora ya kurahisisha utendaji kazi na kuongeza tija katika maendeleo ya vyama hivyo.


Hayo yameelezwa na Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya Ushirika Mkoa wa Morogoro, Bi. Cesilia Filimin, wakati akifungua Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoani humo, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Mbaraka Mwinshehe uliopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.


Akifafanua zaidi, Bi. Cesilia amesema kuwa vyama hivyo vinapaswa kuachana na matumizi ya mifumo ya analojia, hususan matumizi ya karatasi katika utunzaji wa takwimu na taarifa nyingine muhimu, badala yake vigeukie mifumo ya kidijitali ambayo ni rahisi na ya haraka ili kuleta ufanisi katika utendaji kazi.


"Dunia kwa sasa inaelekea kwenye matumizi makubwa ya TEHAMA; zama za matumizi ya karatasi zimepitwa na wakati. Jikiteni kwenye dijitali," amesema Bi. Cesilia Filimin.


Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Jukwaa la Maendeleo ya Ushirika Mkoa wa Morogoro, Bw. Iddi Bilali, amesema jukwaa hilo limekuwa likifanyika kila mwaka na limekuwa na mafanikio makubwa katika kubadilishana uzoefu, kujadili changamoto na mafanikio ya vyama, pamoja na kuimarisha utendaji kazi na uendeshaji wake.


Kwa upande wao wanachama wa vyama vya ushirika akiwemo Bi. Florentina Kachelwa amesema kabla ya kujiunga na vyama hivyo, wakulima walikuwa wanakumbwa na changamoto za upatikanaji wa pembejeo za kilimo, mbolea na mbegu bora. Hata hivyo amesema baada ya kujiunga na vyama hivyo, baadhi ya changamoto hizo zimeanza kutatuliwa.


Hata hivyo ameiomba serikali kuendelea kuunga mkono juhudi za kutatua changamoto hizo ili kuwawezesha wakulima wanaotegemea vyama vya ushirika kuendesha maisha yao kwa ufanisi.


Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.