• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

WAKUU WA IDARA YA KILIMO WATAKIWA KUIMARISHA HUDUMA ZA UGANI.

Posted on: May 11th, 2021

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amewataka Wakuu wa Idara ya Kilimo katika Halmashauri  za Mkoa huo Kuimarisha huduma za ugani ili kuwajenge uwezo wakulima kulima mazao yao kisasa.

Agizo hilo amelitoa Mei 10, 2021 wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya wataalam wa kilimo Mkoani  Morogoro juu ya  utambuzi wa visumbufu vya mazao na namna ya kukabiliana navyo yaliyoendeshwa na Taasisi ya Afya ya Mimea - TPRI katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

‘’…..Hamuwafikii wakulima ipasavyo, mmeitwa wataalam kwa sababu kilimo kinawategemea nyinyi, mkulima anapata utaalam kupitia huduma za ugani, kama hatufanyi maana yake ni nini? nataka ndani ya Mkoa wa Morogoro nyie wataalam muoneshe uwepo wenu’’ amesisitiza Kalobelo.

Mhandisi Kalobelo ameonekana kukasirishwa na kukosekana kwa huduma za ugani kwa wakulima hali ambayo inayopelekea mazao yao kutostawi vizuri kisha kushambuliwa na visumbufu vya mazao bila kuwepo msaada wowote kutoka kwa maafisa hao wenye jukumu la kutoa ujuzi kwa wakulima.

Aidha, Mhandisi Kalobelo amesema hakuna sababu ya msingi ya mazao ya wakulima kushambuliwa na visumbufu vya mazao hivyo kuwataka Wakuu wa Idara ya Kilimo kujiheshisha kupitia Elimu zao kuwaelimisha wakulima namna nzuri ya kulima kwa kisasa na kukabiliana na visumbufu.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Kalobelo amewataka Wakuu hao wa Idara kuwahamasisha wakulima katika maeneo yao kujikita katika kilimo cha pamoja (Block farming) ili kuleta tija ya uzalishaji, kusaidiwa kwa wakati na kupewa taarifa mbalimbali pale majanga yanapojitokeza.

Kwa upande wake Mtaalam wa udhibiti wa visumbufu vya mimea na viwatilifu kutoka TPRI Ndg. Maneno Chidege ametaja leongo la mafunzo hayo ni kutoa Elimu kwa wataalam wa kilimo ili waweze kuwasaidia wakulima kukabiliana na visumbufu wageni ambao wanashambulia mimea katika maeneo yao.

Ndg. Chidege amebainisha baadhi ya visumbufu vya mimea ni Nzige wa Jangwani, panzi, panya, Kantangaze na vijeshi vamizi ambavyo vyote vimeshapatiwa dawa za kukabiliana navyo ikiwa ni pamoja na  magonjwa ya mnyauko.

Naye, Kaimu Afisa Kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro Bi. Ruth Masengu amesema hali ya visumbufu katika Wilaya hiyo ni tishio hususan visumbufu aina ya kwerea kwerea ambao wanaharibu mazao ya mpunga na vijeshi vamizi wanaoshambulia mazao ya mahindi.

 

MWISHO.

 

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • WAHARIRI NCHINI WAPATIWA MAFUNZO USIMAMIZI WA MNYORORO WA UGAVI.

    June 17, 2025
  • ZAIDI YA TRILIONI 3 ZATEKELEZA MIRADI YA MAENDELEO MKOANI MOROGORO

    June 16, 2025
  • UPUNGUFU WATUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • UPUNGUFU WA TUMISHI WAIBUKA HOJA ZA CAG MLIMBA.

    June 11, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.