Septemba 23, 2024 Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Alexander Pastory Mnyeti (mb) amefanya ziara ya siku moja Mkoani Morogoro na kufungua Mkutano Mkuu wa 29 wa Mtandao wa Vikundi vya Wakulima Tanzania (MVIWATA). Mkutano huo umefanyika katika Chuo Kikuu cha Waislam (MUM) kilichopo Halmashauri Manispaa ya Morogoro.
Mhe. Naibu Waziri kabla ya kufungua Mkutano huo aliwasili Ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kupokelewa na Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mali Dkt. Rozalia Rwegasira na kusaini kitabu cha wageni.
MWISHO.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.