• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AENDELEA NA MAONO YA KUKUZA KILIMO MKOANI MOROGORO.

Posted on: June 27th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima, ameendelea kubeba maono ya kukuza sekta ya kilimo katika mkoa huo kwa kulima mazao ya kimkakati yakiwemo karafuu, kakao, parachichi, chikichi na kahawa, ambayo amesema yatachochea ukuaji wa uchumi ndani ya Mkoa na Taifa.


Mhe. Malima amebainisha hayo Juni 26, 2025, wakati akifungua mkutano wa Baraza la Biashara la Mkoa wa Morogoro uliofanyika katika Hotelli ya Morena halmashauri ya Manispaa ya Morogoro na kujumuisha viongozi ngazi ya mkoa, wilaya, makampuni binafsi na wajasiriamali.


Mhe. Malima amesisitiza kuwa huu ni wakati muafaka kwa Mkoa huo kujitangaza na kutambulika kitaifa na kimataifa kupitia sekta ya kilimo, hasa kilimo cha kisasa cha mazao ya kimkakati yana soko ya kimataifa huku akibainisha kuwa ifikapo 2035, Morogoro itakuwa inazalisha tani elfu 20 za karafuu.


"...Sisi tukipanda miche isiyopungua milioni 2 ya mikarafuu, Morogoro, yaani, utakuwa unasema mzalishaji namba moja wa karafuu duniani ni Indonesia, namba mbili ni Morogoro – na inawezekana...," amesema Mhe. Adam Kighoma Malima.


Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo mkoani humo kubuni na kutumia fursa zinazotolewa na kilimo cha viungo na matunda, kwa lengo la kuutangaza amkoa wa Morogoro kimataifa kupitia uzalishaji wa mazao hayo.


Pia, ameeleza kuwa wadau wa biashara wanapaswa kubadili mtazamo kuwa kilimo si chaguo la mwisho bali ni eneo muhimu la kiuchumi linaloweza kuinua maisha ya mwananchi mmoja mmoja, na kuchangia kwa kiasi kikubwa uchumi wa taifa.


Naye Mwenyekiti wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo Mkoa wa Morogoro, Muadhini Mnyanza, ameeleza kuwa chemba ya biashara mkoani humo inaendelea vizuri na kuimarisha ushirikiano na mahusiano na sekta mbalimbali ikiwa ni sehemu ya mikakati ya pamoja ya kukuza uchumi wa mkoa huo.


Kwa upande wake, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Gairo ambaye ni Mkuu wa Mkoa mteule wa Mkoa wa Songwe, Jabiri Makame, amebainisha kuwa wilaya ya Gairo imeanza kutekeleza majaribio ya kilimo cha parachichi na viazi mviringo kwa lengo la kuendeleza ajenda ya mkoa ya kuifanya Morogoro kuwa kituo cha kilimo cha kisasa.


Nao baadhi ya wafanyabiashara wa Mkoa huo wamebainisha kuwa changamoto wanazokumbana nazo ni uhaba wa malighafi na kukosa mitaji jambo ambalo linasababisha baadhi ya viwanda kushindwa kuendelea na uzalishaji huku wakibainisha changamoto za kucheleweshwa upatikanaji wa hati miliki pindi wanaponunua maeneo ya kuwekeza.


MWISHO.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AMUUMA SIKIO DC MVOMERO, KUTUMIA BUSARA ZAIDI.

    June 27, 2025
  • RC MALIMA AENDELEA NA MAONO YA KUKUZA KILIMO MKOANI MOROGORO.

    June 27, 2025
  • Maadhimisho ya miaka 80 hospitali ya Rufaa Morogoro yaanza kuleta Matokeo

    June 25, 2025
  • RC MALIMA AENDELEA KUPAMBANA KUTATUA KERO YA MAJI MANISPAA YA MOROGORO.

    June 21, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.