• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

Posted on: May 8th, 2025



Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amesema serikali ya Mkoa huo haitomvumilia mlanguzi yeyote anayenunua mazao kwa wakulima kienyeji na kwa bei ndogo kwani serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan ina nia njema kuanzisha mfumo wa stakabadhi za ghala ili kuwanufaisha wakulima.

Mhe. Malima amesema hayo Mei 7, Mwaka huu wakati akifungua kikao cha tathmini ya mfumo wa stakabadhi za ghala kilichofanyika katika Halmashauri ya Ifakara Mji Wilayani Kilombero kikiwa na lengo la kubaini changamoto zilizojitokeza msimu wa 2024/2025 na maandalizi ya msimu mpya wa 2025/2026.

Aidha, Mkuu huyo wa Mkoa ametaka kuimarisha ushirikiano kati ya wakulima, watumishi wa serikali pamoja na wanasiasa  ili kuleta mapinduzi ya kilimo Mkoani Morogoro na kuwa mfano bora barani Afrika katika kuchochea mabadiliko ya kiuchumi kupitia sekta ya kilimo.

Mhe. Adam Malima amesema wakulima wanapaswa kuuza mazao yao kupitia mfumo wa Stakabadhi za ghala kwani mfumo huo umeongeza bei za mazao likiwemo zao la kakao kutoka kilo 1 kuuzwa Tsh. 4,000 hadi Tsh. 28,000 hivyo kuinua uchumi kwa wakulima nataifa.

Kwa sababu hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amesema Mkoa huo unahitaji kuzalisha tani 20,000 za ufuta  zitakazoingiza Tsh. Bil. 80 kutokana na mfumo wa Stakabadhi ghalani na kukuza vipato vya wakulima.

Mazao  mengine ya biashara yanayolimwa Mkoani humo ambayo yanatakiwa yapitie mfumo huo wa stakabadhi za ghala ni pamoja na Mbaazi, Kakao, Korosho na karafuu ambapo huongeza mapato ya ndani kwa kiasi kikubwa Mkoani humo kupitia mfumo huo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Biashara, Viwanda na Uwekezaji Mkoani Morogoro Bi. Beatrice Njawa amesema kutokana na changamoto zinazodaiwa kucheleweshwa kwa malipo ya stakabadhi ghalani Serikali ya Mkoa imetengeneza kamati ya kuhakikisha malipo ya mazao ya mfumo huo kulipia kwa wakati.

Naye, Mrajisi Msaidizi wa Vyama vya ushirika Mkoa wa Morogoro  Bi. Cesilia Filimin amesema mfumo wa stakabadhi za Ghala umesaidia kuwepo kwa soko la uhakika kwa mazao yanayolimwa Mkoani humo huku akibainisha kuwa kukosekana kwa elimu ya kutosha kuhusu mfumo huo kwa wakulima ni moja ya changamoto inayopelekea baadhi ya wakulima kuendelea kuuza mazao yao kwa walanguzi.



Mwisho.

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.