TAARIFA FUPI YA UTALII NA VIVUTIO VYA UTALII MKOANI MOROGORO
1. Utangulizi
Mkoa wa Morogoro umebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya utalii ukihusisha mbuga zenye bio-anuai nyingi na mandhari za kupendeza, milima, maporomoko ya maji, vyanzo vya maji, na wanyamapori, ndege wa aina mbalimbali, mapango ya kihistoria, maeneo ya njia za watumwa na misitu minene na safu za milima ya Tao la Mashariki.
Mkoa wa Morogoro ni wa pili kwa ukubwa baada ya Mkoa wa Tabora lakini pia ni wa pili kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii vya aina mbalimbali hasa mimea na wanyama katika ukanda wa kusini (Southern Tourist Circult) baada ya Mkoa wa Arusha katika ukanda wa kaskazini (Northern Tourist circuit)
2. Aina ya hifadhi (Protected Areas) zilizomo katika Mkoa wa Morogoro:
Misitu ya Asili (Catchment Forest Reserves). Mkoa una misitu 39 yenye ukubwa wa hekta 321,236.
Hifadhi za Taifa (National Parks): Mkoa una Hafadhi mbili za Taifa ambazo ni Hifadhi ya Milima ya Udzungwa (52 km2) na Hifadhi ya Taifa Mikumi (4,471km2)
Hifadhi ya Milima ya Udzungwa
Hifadhi ina ukubwa wa kilomita za mraba 1,990; ni hifadhi yenye viumbe ambavyo havipatikani maeneo mengine kokote duniani: Mbega wekundu (Iringa red colobus) na Sanje crested mangabey; ndege: chozi bawa jekundu (Rufous-winged sunbird) na jamii mpya Kwale kugunduliwa (Patridge-like Francolin).
Maporomoko ya mto Sanje yenye urefu wa mita ~170 yakianguka na kutua mithili ya ukungu.
Aina ya maua adimu: African violet
Hifadhi ya Taifa Mikumi
Eneo kuu la muhimu katika hifadhi hii ni uwanda wa mafuriko (Mbuga za wazi) pamoja na safu za Milima katika hifadhi pamoja na misitu ya miombo.
Ndege huongezeka hadi kufikia aina 300 wakati wa mvua kutokana na kuwepo kwa ndege wahamiaji kutoka nchi za Ulaya na Asia na kuungana na makundi ya ndege wakazi.
Makundi makubwa ya Viboko, Pundamilia, nyumbu na mengine mengi.
Hifadhi iko Kaskazini mwa mbuga ya Selous na njiani kuelekea/kutoka hifadhi za Ruaha na Udzungwa.
Pori la Akiba la Selous (Selous Game Reserve). Ni mbuga kubwa Afrika na yenye wanyama wengi.
Pori la Akiba la Seous limepata jina lake kutokana na mwindaji na mtaalamu wa mazingira asilia Friderick courtney Selous aliyeuawa mwaka 1917 Mto Rufiji katika vita na Wajerumani.Selous alizikwa katika pori hili na kaburi lake linaweza kuonekana kwa kufuata barabara ya Beho Beho-Matambwe
Pori Tengefu la Kilombero (Kilombero Game Controlled Area): Ni kiini cha eneo la ardhi-oevu ambalo ni RAMSAR site.
Hifadhi za jamii (Community Wildlife Management Areas): Mkoa una hifadhi za jamii za Wami-Mbiki, ILUMA na JUKUMU. Hifadhi hizi zimeidhinishwa (Authorized Association) na kupewa Hati ya matumizi (User Rights). Utalii upo kidogo lakini mipango kwa kuzitangaza ili kupata wawekezaji inaendelea.
3. Changamoto za Utalii Mkoani Morogoro
5. Vivutio vinavyopatikana Mkoani Morogoro
S/N
|
ENEO LA KIVUTIO
|
AINA YA
UTALII |
VIVUTIO
|
1.
|
Msitu wa Kimboza-unapatikana Matombo katika Wilaya ya Morogoro vijijini.
|
-Kuona (Game viewing)
-Kupiga picha |
-Chemichemi za asili,
-Pango la choka –Wahawi (Eneo la kihistoria mahali wachawi walipokuwa wanachomewa) -Dago la njiwa (mahali njiwa wanapooga kiangazi na masika) -Pango la Tambiko -Dimbwi lenye nyoka wa maajabu -Eneo la kuzalishia vipepeo -Garko (Gwanko wiliamsii)-aina ya mijusi ambayo haipatikani sehemu nyingine duniani. -Mimea adimu, wanyamapori (Black Rhino) na wadudu |
2.
|
Hifadhi ya Mazingira Asilia ya Uluguru katika Wilaya ya Morogoro
|
-Kuona
-Kupiga picha |
-Vinyonga wenye pembe tatu ambao
Wanapatikana katika milima hii pekee: hawapatikani mahali pengine popote. -Mimea adimu-135 -Ndege wa pekee anayeitwa Wami-mbizi. -Ndege (Ulugruru Violet-backed sunbird -Maporomoko (Hululu and Kibwe falls) -Mapango -Tegetero trails -Uwanda wa Lukwangule -Lupanga Peak trail -Kimhandu Peak -Morning site -Bunduki Corridor na - Bondwa peak -Mimea ambayo ni adimu na pekee-Africam violet – Saintpaulia |
3.
|
Hifadhi ya Mazingira Asilia Kilombero
|
-Kuona
-Kupiga picha |
-Maporomoko yanayozalisha umeme-Mbingu
-Mbega wekundu -Ndege wa aina mbalmbali -Mimea ya aina mbalimbali -Mandhari ya kupendeza (Scenery beauty) |
4.
|
Hifadhi ya Mazingira Asilia Mkingu katika Wilaya ya Mvomero
|
-Kuona
-Kupiga picha |
-Mapango ya milima ya Nguru Kusini (South Nguru), ambapo ndani ya mapango haya kuna Mercury (Hg). Pia ndani ya mapango haya kuna maji ambayo ukirusha kitu kinarudishwa kilikotoka.
-Maporomoko ya maji -Mimea ya aina mbalimbali inayokadiriwa kufikia spishi 793 -Wanyama mbalimbali wanaokisiwa kufikia spishi 329 (Mamalia 34, ndege 214, reptilia 43, amphibian 38) -Mandhari ya kupendeza (Scenery beauty) -Safu ya Mlima Nguru moja kati ya safu za milima ya Tao la Mashariki yenye unyevunyevu mkubwa na bio-anuai nyingi |
5.
|
Hifadhi ya Taifa Mikumi
|
-Kuona
-Upigaji wa picha |
-Mbuga yenye wanyama wengi (simba, chui, nyumbu, ngiri, pundamilia, tembo, swala, twiga, nyati, kuro n.k.)
-Ndege wa aina mbalimbali zaidi ya spishi 300. -Uwanda wenye mandhari ya kupendeza. |
6.
|
Hifadhi ya Taifa Udzungwa
|
-Kuona
-Upigaji wa picha Kupanda mlima (Hiking) |
-Aina 12 za wanyama aina ya primata kati yao 2 (Ngolapa wa Sanje na Mbega wekundu wa Iringa) na aina za Komba ni wa pekee hawapatikani pengine popote duniani.
-Mandhari nzuri (Scenery beauty) yenye maporomoko ya maji, miti mirefu, maua na vilele vya milima. -Makumbusho ya kale yenye rasilimali za kitamaduni na kidini (Mapango ya Bokela, Mwanaluvele na Nyumbanitu) -Vyanzo vya mito ambayo hupeleka maji Ruaha Mkuu na Kilombero na hatimaye Rufiji na pia hutumika kuzalisha umeme, kilimo na uvuvi. -Magombera Chameleon na aina nyingine za mimea na vipepeo -Aina nyingi za ndege. |
7.
|
Pori la Akiba la Selous
|
-Kuona
-Uwindaji wa Kitalii -Upigaji wa picha (Photographic safari) |
- Ni mbuga kubwa Africa na ina tembo zaidi ya 70,000
-Idadi kubwa ya wanyamapori na wale adimu kama mbwa mwitu na faru. -Maporomoko ya Stigglers’ Gorge ambayo yanatarajiwa kuzalisha umeme. -Mandhari ya kupendeza. |
8.
|
Pango la Matombo Wilayani Morogoro
|
-Kuona
|
-Mapango yenye chuchu kama za binadamu
-Mapango ya kihistoria chanzo cha jina la Matombo |
9.
|
Kisaki-Ndalanda Wilayani Morogoro
|
-Kuona
|
-Chemichemi ya maji moto (Hot water springs) ambayo inaweza kutoa umeme
|
10.
|
Msitu wa Hifadhi wa Mkulazi Wilayani Morogoro
|
-Kuona
-Kupiga picha |
-Makazi ya wanyama kutoka Selous wakati maskani yao yamejaa maji katika bonde la Ukutu.
|
11.
|
Hifadhi ya Jumuiya ya wanyamapori Wami-Mbiki katika Wilaya ya Mvomero na Morogoro
|
-Uwindaji wa wenyeji na Kitalii
-Kuona |
-Ni Hifadhi ambayo njia ya watumwa ilipitia.
-Kuna wanyama mbalimbali kama tembo, simba, swala, pundamilia nk. -Ni kiungo cha shoroba ziendazo Hifadhi ya Mikumi, Saadani, Tarangire na Selous |
12.
|
Hifadhi ya Jumuiya ya wanyamapori Ukutu katika Wilaya ya Morogoro
|
Uwindaji wa wenyeji na Kitalii
-Kuona |
Kuna wanyama mbalimbali kama Tembo, Chui, Nyati, Viboko, Twiga, Pundamilia, Simba, Swala, Pundamilia nk
|
13.
|
Uhifadhi wa nyoka (Snake Park) eneo ka Mlama-Dakawa Wilayani Mvomero
|
-Kuona
-Kujifunza |
-Kuna nyoka wa aina mbalimbali wenye sumu (Venom) na wasio na sumu
|
14.
|
Milima ya Kanga Wilayani Mvomero
|
-Kuona
-Kupanda (hiking) |
-Viumbe pekee (Unique species) kama aina ya miti ijulikanayo kama Mrs Ibaz trees.
|
15.
|
Makutano ya mito miwili iitwayo Wami-Mbulumi.
|
-Kuona
|
-Idadi kubwa ya mamba
|
16.
|
Kilombero Game Controlled Area
|
-Kuona
-Uwindaji wa Kitalii -Upigaji wa picha -Utalii wa kuvua-Sport fishing -Kuangalia ndege (Bird watching) -Kupanda milima (Hiking), -Utalii wa ndani (Eco-tourism) |
-Baadhi ya wanyama ni kama vile sheshe (Kobus vardonii) ambao inakadiriwa kuwa 75% duniani wanapatikana hapa.
-Wanyama wakubwa ni pamoja na nyati, tembo, viboko, sable antelope, kongoni, pofu, mbega wekundu wa Sanje, ngiri, kuro, pundamilia, mamba na kenge -Kuna vitalu vinne vya uwindaji wa Kitalii (Mnyera, Kilombero Kaskazini- Mlimba, Kilombero Kaskazini-Mngeta na Matundu -Ndege wa aina mbalimbali. -Viumbe wanaopatikana tu Kilombero (endemic sp) mfano Vyura wa Kihansi, Udzungwa forest patridge, Rufous winged sunbird, Long tailed cisticola, Kilombero cisticola, Kilombero weaver. Primata kama vile Sanje crested mangabey, samaki kama vile Mgundu and Mbala. Baadhi ya spishi ni adimu kama vile Fish eagle. |
17.
|
Kijiji cha Msovero kwa Chief Mangungo katika Wilaya ya Kilosa
|
Kuona
|
- Historia ya kusainiwa kwa mkataba wa ulaghai wa Carl Peter’s
-Njia ya watumwa katika eneo la Mamboya. |
18.
|
Pori la wanyamapori la Twatwatwa na Kidoma katika Wilaya ya Kilosa
|
-Kuona
-Uwindaji |
-Tembo, Simba, Swala, Mbwa mwitu, Tandala, Nyati, Kuro, Chui, Twiga, Pundamilia, Ngiri, Dikidiki, Mbawala, Dondoro, Nungunungu, Nungura, Mamba, Nyumbu,
- Ndege wa aina mbalimbali -Aina 70 ya miti asili inayopatikana nchini. |
19
|
Maeneo ya Kihitoria na Kiikolojia Wilayani Ulanga maeneo ya Nawenge, Nambiga, Sali, Mzelezi, Myowe na Ligamba kwa upande wa misitu na Pori Tengefu la Kilombero kwa upande wa wanyamapori.
|
-Kuona
-Kupiga picha |
-Mapango ya mawe na makaburi ya vita vya majimaji yanayopatikana Mahenge na Mbangayao yenye ukubwa wa kilomita za mraba 1.2
- Maporomoko ya maji, Mapango na Msitu mnene wenye uasili/usioharibiwa katika kijiji cha Sali -Mito 40 ya kudumu yenye maji mwaka mzima na mabwawa ya asili yapatayo 96. - Kuna vitalu vitano (5) vya uwindaji wa kitalii. Mahenge Open Area South, Mahenge Open Area North, Furua Open Area, Kilombero Game Controlled Area South, Kilombero Game Controlled Area North, Mwatisi Open Area South na Mwatisi Open area North) |
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.