Wilaya ya Ulanga
Wilaya ya Ulanga ni mojawapo ya Wilaya saba (7) za Mkoa wa Morogoro ambazo ni Mvomero,Morogoro, Gairo, Kilosa, Kilombero, Malinyi na Ulanga yenyewe.
Wilaya ya Ulanga iko umbali wa Kilometa 512 kutoka Jiji la Dar es Salaam. Ipo kati ya Latitudo 4.5 Kusini na Longitudo 37.4 Mashariki. Ipo kiasi cha futi 1,600 kutoka usawa wa bahari.Ulanga inapakana na milima ya Uluguru, pia imepakana na Mkoa wa Iringa, Songea, na wilaya ya Malinyi na Kilombero.
Wilaya ya Ulanga ina eneo la Kilometa za Mraba 14,423 sehemu kubwa ni mapori ya Hifadhi na Misitu, Hifadhi ya Selous kwa upande wa kusini Mashariki.
Wilaya ya Ulanga ina wastani wa nyuzi joto 180C hadi 260C wakati wa baridi (Julai– Novemba) mvua za vuli huanza mwezi wa Octoba hadi Februari, mvua za masika kuanzia mwezi machi hadi Mei. Mvua hizo hunyesha kwa wastani wa kati ya milimita 800 hadi 1,600. Kwa maelezo zaidi bonyeza http://www.ulangadc.go.tz/
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.