SEHEMU YA UCHUMI NA UZALISHAJI
Sekta ya Kilimo
Malengo na utekelezaji wa mazao ya chakula na biashara.
Mkoa wa Morogoro una eneo la hekta 2,226,396 linalofaa kwa Kilimo na kati ya eneo hilo zaidi ya hekta 862,092 ndizo zinazolimwa kwa sasa sawa na asilimia 39. Eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 1,510,339.51 na eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni hekta 40,558 sawa na asilimia tatu. Mkoa una Mito 143 inayotitirisha maji mwaka mzima, una udongo mzuri na mabonde mengi ambayo bado hayajaendelezwa. Wananchi wa Mkoa wa Morogoro (75%) wanategemea zaidi kilimo kwa ajili ya ajira, kipato na chakula. Mazao ya chakula yanayolimwa kwa wingi ni Mahindi, Mpunga, Mtama, Mihogo, Viazi vitamu, Maharage na Ndizi. Mazao makuu ya biashara ni Miwa, Alizet, Ufuta, Korosho na Pamba.
Tija katika mazao ya Mahindi na Mpunga
Tija ya uzalishaji imekuwa ikibadilika kutoka mwaka hadi mwaka, hii ni kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa ya kila mwaka. Ongezeko la tija kwa zao la mahindi ni kutoka tani 1.9/he mwaka 2014/2015 hadi tani 2.3/he mwaka 2016/2017. Kwa zao la mpunga tija imepungua kutoka tani 3.3/he mwaka 2014/2015 na kufikia tani 3.2/he mwaka 2016/2017 Jedwali.
Jedwali: Uzalishaji na tija ya mazao ya Mahindi na Mpunga kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2016/2017
Mwaka
|
Eneo lililolimwa (hekta)
|
|||||
Mahindi
|
Mpunga
|
|||||
Utekelezaji hekta
|
Mavuno tani
|
Tija (tani/he)
|
Utekelezaji hekta
|
Mavuno tani
|
Tija (tani/he)
|
|
2014/2015
|
200,347.25
|
384,004.95
|
1.9
|
268,179.4
|
875,812.40
|
3.3
|
2015/2016
|
208,340.65
|
334,491.59
|
1.6
|
213,043.12
|
586,022.45
|
2.8
|
2016/2017
|
299,426
|
683,293
|
2.3
|
290,237
|
941,508
|
3.2
|
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri za Mkoa wa Morogoro
Katika msimu wa 2016/2017 Mkoa ulilenga kulima hekta 736,723.59 ili kuvuna tani 2,895,823.19 za mazao ya chakula, mazao ya biashara Mkoa umelenga kulima hekta 210,363.17 ili kuvuna tani 3,289,168.55.
Utekelezaji wake hekta 738,282 zililimwa sawa na asilimia 100 na kuvuna tani 2,298,859 sawa na asilimia 79 ya lengo kwa mazao ya chakula, mazao ya biashara zililimwa hekta 123,811 sawa na asilimia 59 na kuvunwa tani 1,567,289 sawa na asilimia 48 ya lengo.
Jedwali: Malengo na Utekelezaji katika msimu wa 2011/2012 – 2017/2018.
Mwaka
|
|
|
Chakula
|
% ya lengo
|
Biashara
|
% ya lengo
|
2014/2015
|
Lengo
|
Hekta
|
713,882
|
|
174,887.00
|
|
Tani
|
2,691,282.00
|
|
3,183,072.00
|
|
||
Utekelezaji
|
Hekta
|
589,231.00
|
83%
|
152,459.50
|
87%
|
|
Tani
|
1,877,942.10
|
70%
|
3, 050,065.58
|
96
|
||
2015/2016
|
Lengo
|
Hekta
|
756,294.50
|
|
199,526.1
|
|
Tani
|
2,762,316.70
|
|
3,272,708.28
|
|
||
Utekelezaji
|
Hekta
|
563,826.18
|
76%
|
123,148.70
|
62%
|
|
Tani
|
1,597,895.65
|
58%
|
2,324,629.19
|
71%
|
||
2016/2017
|
Lengo
|
Hekta
|
736,723.59
|
|
210,363.17
|
|
Tani
|
2,895,823.19
|
|
3,289,168.55
|
|
||
Utekelezaji
|
Hekta
|
738,282
|
100%
|
123,811
|
59%
|
|
Tani
|
2,298,859
|
79%
|
1,567,289
|
48%
|
||
2017/2018
|
Lengo
|
Hekta
|
867,666.53
|
|
168,294.06
|
|
Tani
|
2,878,865.62
|
|
2,910,377.74
|
|
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri
Hali ya upatikanaji wa chakula
Katika Mkoa wa Morogoro kumekuwepo na ongezeko la uzalishaji wa mazao ya chakula kwa ziada kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2016 / 2017. Kwa mujibu wa matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 idadi ya watu ilikuwa 2,218,492 ambapo ongezeko la watu ni asilimia 2.4 kwa mwaka. Hivyo kulingana ongezeko la watu na uhitaji wa chakula kwa kila mwaka, kuanzia mwaka 2014/2015 hadi 2016/2017 mwenendo wa uzalishaji na ziada katika Mkoa wa Morogoro ni kama inavyo onekana katika jedwali.
Jedwali: Uzalishaji na mahitaji ya chakula 2014/2015 hadi 2016/2017
Mwaka
|
Eneo lililo limwa (He)
|
Uzalishaji
(Tani) |
Mahitaji ya chakula (Tani)
|
Ziada
(Tani) |
2014/2015
|
616,127.80
|
1, 877,942.1
|
549,910.20
|
1,328,031.9
|
2015/2016
|
563,826.18
|
1,597,895.65
|
563,108.00
|
1,034,787.65
|
2016/2017
|
675,306.08
|
2,298,859.00
|
596,915.30
|
1,701,944.00
|
Pembejeo za Ruzuku Msimu wa 2017/2018
Katika kutekeleza azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na Uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo mwaka 2025 juhudi kubwa imefanyika ili kutimiza malengo ya kimkakati kuelekea kilimo cha kibiashara. Moja ya mikakati hiyo ni kuhakikisha mkulima anapata pembejeo za kilimo hususani; mbegu bora, mbolea na viuatilifu. Katika utekelezaji wa mkakati huo kumekua na mafanikio kwa baadhi ya maeneo kama vile upatikanaji wa mbegu mpya za mazao mbalimbali zinazozalishwa na vituo vya utafiti wa kilimo hapa nchini na ongezeko la uzalishaji wa mazao mfano, kilimo shadidi katika zao la mpunga. Pamoja na mafanikio hayo kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo bei kubwa ya pembejeo na gharama kwa serikali katika utoaji wa ruzuku.
Wizara ya kilimo kwa kushirikiana na wadau wake ilifanya marekebisho ya Kanuni za mbolea za mwaka 2011 kupitia the fertilizer (amendment) regulations, 2017 ambayo moja ya marekebisho hayo ni kuhakikisha bei ya mbolea inadhibitiwa kwa kutoa bei elekezi.
Katika marekebisho hayo kanuni ya 56, Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania inawajibu wa kutangaza bei elekezi ya mbolea kwa muuzaji wa mbolea kwa rejareja (muuzaji wa mwisho) ambapo aina zote za mbolea zinatakiwa kuuzwa kwa bei hiyo au chini ya hiyo .
Mamlaka ya udhibiti wa Mbolea Tanzania imetangaza bei elekezi kwa mbolea za kupandia (DAP) na ya kukuzia (Urea). Kwa ujumla bei hiyo elekezi ya mbolea imepangwa kwa kuzingatia gharama za ununuzi wa mbolea kutoka kwenye chanzo (free on board), usafirishaji wake kwa meli, tozo mbalimbali, pamoja na faida ya wafanyabiashara. Aidha, bei za mbolea zimepangwa kwa kuzingatia umbali na aina ya usafiri utakaotumika; hususani usafirishaji kwa njia ya reli isipokuwa kwa maeneo ambayo hakuna miuondombinu ya reli. Bei elekezi iliyopangwa katika Mkoa wa Morogoro ni kama ifuatavyo;
DAP indicative farm gate prices by means of transport
Stockpoint
|
Road
|
Railway
|
Observed Price
|
BPS
Saving |
Morogoro
|
50,878
|
51,043
|
68,500
|
26%
|
Gairo
|
50,818
|
|
|
|
Ifakara
|
|
51,236
|
|
|
Kidatu (TRL)
|
50,983
|
|
|
|
Kilosa
|
51,143
|
|
|
|
Kisaki
|
50,208
|
|
|
|
Mang’ula
|
51,082
|
|
|
|
Mikumi
|
50,818
|
|
|
|
Mlimba
|
51,440
|
|
|
|
Morogoro DC
|
50,158
|
|
|
|
Morogoro MC
|
50,158
|
|
68,500
|
27%
|
Msolwa
|
51,011
|
|
|
|
Mvomero DC
|
50,400
|
|
|
|
Ulanga (Mahenge)
|
51,792
|
|
|
|
UREA indicative farm gate price by means of transport |
||||
Stockpoint
|
Road
|
Railway
|
Observed Price
|
BPS
Saving |
Morogoro
|
38,299
|
38,464
|
52,000
|
26%
|
Gairo
|
38,239
|
|
|
|
Ifakara
|
|
38,657
|
38,657
|
|
Kidatu (TRL)
|
38,404
|
|
|
|
Kilosa
|
38,564
|
|
|
|
Kisaki
|
37,629
|
|
|
|
Mang’ula
|
38,503
|
|
|
|
Mikumi
|
38,239
|
|
|
|
Mlimba
|
38,861
|
|
|
|
Morogoro DC
|
37,579
|
|
|
|
Morogoro MC
|
37,579
|
|
52,000
|
28%
|
Msolwa
|
38,432
|
|
|
|
Mvomero DC
|
37,821
|
|
|
|
Ulanga (Mahenge)
|
39,213
|
|
|
|
Hata hivyo, utaratibu wa kutangaza upya bei elekezi kwa mbolea ya DAP na UREA unaandaliwa baada ya kupata umbali halisi kutoka kila Halmashauri.
Kuhamasisha matumizi na upatikanaji wa zana za Kilimo Mkoani.
Mkoa wa Morogoro una matrekta 1,055 sawa na ongezeko la asilimia 7 kutoka matrekta 990 mwaka 2014/2015, upungufu ni 551 sawa na Asilimia 34% ya mahitaji. Mkoa pia una power tiller 438 na majembe ya kukokotwa na wanyamakazi 18,616. Kutokana na upungufu wa matrekta 551 Mkoa umewasilisha maombi ya matrekta 543 ya mkopo toka Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa SUMA- JKT mkakati unaendelea hivyo tunatarajia kuyapokea utaratibu utakapo kuwa tayari. Aidha, eneo la hekta 315,033 linalolimwa kwa kutumia Matrkta na Powertillers na eneo la hekta 892,011.96 linalimwa kwa kutumia wanyama kazi.
Mifugo na Uvuvi
-Kukabiliana na magonjwa yanayoenezwa na kupe katika halmashauri za Mkoa wa Morogoro.
Vifo vya mifugo vinavyosababishwa na kupe vimepungua kwa 80% kutokana na wafugaji kutumia madawa ya kuogesha kutoka kwenye vituo binafsi vya kutolea huduma za mifugo.
Kuboresha koosafu za mifugo
Kuanzia mwaka 2015 hadi hivi sasa kuna wataalam 60 wanaotoa huduma ya uhimilishaji wa ng’ombe kwa ajili ya kuboresha koosafu.
Jumla ya ng’ombe 400 wamepandishwa kwa njia ya chupa na jumla ya ndama 350 wamezaliwa kwa njia ya chupa. Kwa mwaka huu 2017 Shirika la Land O’ Lakes kwa kushirikiana na Kampuni ya ABEA wanatoa huduma ya uhimilishaji na elimu kwa wafugaji juu ya uboreshaji wa koosafu za ng’ombe katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro. Wafugaji wamehamasishwa kuvuna mifugo yao na kununua madume bora ya Boran kwa ajili ya kuboresha koosafu za mifugo yao ambapo hadi hivi sasa jumla ya wafugaji 10 wamenunua madume wapatao 50 wa aina ya Borani.
Kutoa elimu kwa wafugaji juu ya ufugaji bora
Tangu mwaka 2015 hadi 2017 Jumla ya wafugaji wapatao 600 wamepata mafunzo ya ufugaji bora kupitia kwa maafisa ugani.
Kupunguza migogoro ya wakulima na wafugaji na kasi ya wafugaji kuhamahama.
Kwa kipindi cha 2016 hadi 2017 Mkoa umesimamia kwa ukamilifu Utekelezaji wa Sheria ya Utambuzi na Usajili wa mifugo Na. 12 ya mwaka 2010 kwa lengo kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji inayotokana na wafugaji kuhama hama kiholela. Hadi hivi sasa jumla ya ng’ombe 6627438 kati ya 894504 sawa na asilimia 70 wamesajiliwa na kupigwa chapa.
Kwa kipindi hiki migogoro baina ya wafugaji na wakulima imepungua kwa kiasi kikubwa ukilinganisha miaka ya nyuma.
Kufufua na kuendeleza sekta na viwanda vya ngozi
Katika mkakati wa kufufua na kuendeleza Sekta na viwanda vya ngozi tangu mwaka 2015 hadi 2017 Wadau wapatao 80 na Maafisa Ugani wapatao 30 wamepatiwa mafunzo ya jinsi ya kuboresha zao la ngozi.
Uzalishaji wa maziwa
Jumla ya lita 41,217,000 za maziwa zimezalishwa kwa mwaka 2015 hadi 2017 Baadhi ya maziwa yanayozalishwa hununuliwa na Makampuni yanayosindika maziwa ambayo ni Tanga Fresh na Shambani Graduates. Makampuni hayo hununua maziwa na kusindika katika viwanda vyao na kuyasambaza sehemu mbalimbali ambako kuna soko la maziwa.
Uvuvi
Mkoa wa Morogoro umejaliwa kuwa na mito na mabwawa yenye samaki wengi. Sehemu kubwa ya uvuvi hufanyika kutokea kwenye kambi za wavuvi kandokando ya mto Kilombero. Kuna aina zaidi ya 52 ambapo zaidi ya 90% ya samaki wote wanapatikana kutokea mto Kilombero. Uvuvi mwingine kwa kiwango kidogo hufanyika katika mabwawa ya asili, ya kuchimbwa na mito imwagayo maji yake katika bonde la mto Rufiji. Kutokana na vyanzo hivyo vyote, kila mwaka mkoa unakadiriwa kuzalisha samaki zaidi ya tani 350.
Ufugaji wa samaki
Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri umeendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kufuga samaki katika mabwawa ya kuchimbwa ili kuongeza upatikanaji wa samaki Mkoani na pia kupunguza utegemezi katika vyanzo vya asili. Kutokana na uhamasishaji huo mabwawa ya kuchimbwa yameongezeka kutoka mabwawa 491 mwaka 2015 hadi kufikia mabwawa 654 Juni, 2017. Mchanganuo wa mabwawa ya samaki kwa kila Halmashauri ni kama inavyoonyesha katika jedwali Na. 1 hapo chini.
Jedwali Na. 1: Mabwawa ya samaki katika Halmashauri
Na.
|
HALMASHAURI
|
IDADI
|
1.
|
Ifakara Mji
|
29
|
2.
|
Kilombero
|
94
|
3.
|
Kilosa
|
100
|
4.
|
Malinyi
|
55
|
5.
|
Morogoro MC
|
66
|
6.
|
Morogoro DC
|
171
|
7.
|
Mvomero
|
83
|
8.
|
Ulanga
|
56
|
9.
|
Gairo
|
-
|
JUMLA
|
654
|
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri
Uzalishaji wa samaki
Katika kuongeza uzalishaji wa samaki Mkoani, elimu ya ufugaji wa samaki imekuwa ikitolewa kwa wananchi na udhibiti wa uvuvi haramu kwenye vyanzo vya asili umekuwa ukifanyika kwa kutumia doria, elimu na vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya uvuvi (BMUs). Hivyo kutokana na vyanzo vilivyopo Mkoani uzalishaji umeongezeka kutoka tani 254.9 zenye thamani ya shilingi 1,450,125,394 mwaka 2015/2016 hadi kufikia tani 282.4 zenye thamani ya shilingi 1,568,543,045.5 mwaka 2016/2017. Mchanganuo wa uzalishaji kwa kila Halmashauri kwa kipindi cha miaka 2 ni kama inavyoonyesha katika jedwali Na. 2 hapo chini.
Jedwali Na. 2: Mavuno ya samaki kwa msimu wa mwaka 2015/2016 na 2016/2017 katika Halmashauri
Na.
|
HALMASHAURI
|
2015/2016
|
2016/2017
|
||
UZITO (tani)
|
THAMANI (Tsh)
|
UZITO (tani)
|
THAMANI (Tsh)
|
||
1.
|
Kilombero
|
149.7
|
874,294,020
|
187.8
|
1,039,985,692.25
|
2.
|
Kilosa
|
-
|
-
|
1.7
|
9,801,500
|
3.
|
Morogoro MC
|
20.7
|
157,191,000
|
5.3
|
41,814,000
|
4.
|
Ulanga DC
|
35.9
|
153,484,450
|
25.1
|
101,980,200
|
5.
|
Mvomero
|
-
|
-
|
6.1
|
33,715,000
|
6.
|
Morogoro DC
|
0.1
|
520,000
|
2.5
|
10,000,000
|
7.
|
Ifakara Mji
|
48.5
|
294,635,924
|
50.4
|
310,546,653.25
|
8.
|
Malinyi
|
-
|
-
|
3.5
|
20,700,000
|
9.
|
Gairo
|
-
|
-
|
-
|
-
|
|
JUMLA
|
254.9
|
1,450,125,394
|
282.4
|
1,568,543,045.5
|
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri
Ushirika
Kuandikisha, kufuta na kusimamia ufilisi wa vyama vya ushirika
Jumla ya vyama vya ushirika 415 vimeandikishwa hadi kufikia Oktoba 2017 kutoka vyama 363 vilivyokuwepo Oktoba 2015 ikiwa ni ongezeko la 14%. ambapo hakuna chama kilichofutwa wala kufilisiwa hadi kufikia mwaka 2017.
Kusimamia utekelezaji wa sheria ya vyama vya ushirika
Mikutano ya vyama vya ushirika 78 ilisimamiwa kufikia Oktoba 2017 ikilinganishwa na vyama 125 ilivyosimamiwa Juni 2015. Maelekezo na nyaraka mbalimbali vilitolewa kwa vyama 300 vikielekeza utekelezaji wa sheria za vyama vya Ushirika Na 6 ya mwaka 2013 .
Kutayarisha sera na mikakati ya maendeleo ya ushirika
Jumla ya sera mbalimbali 78 ikiwemo sera ya fedha, Mikopo, utumishi na utawala ziliwasilishwa na kuidhinishwa na vyama mbalimbali vya Ushirika kufikia Oktoba 2017 ikilinganishwa na sera 47 zilizokuwepo Juni 2015, ni sawa na 66% ya ongezeko.
Kutoa huduma za ushauri na kuweka mazingira muafaka yatakayowezesha ukuaji na uendelezaji wa ushirika
Kwa kushirikiana na PASS, CRDB Bank Plc, na wadau wengine jumla ya Maandiko ya Miradi ya Vyama vya Ushirika 43 yalitayarishwa kufikia Oktoba 2017 ikilinganishwa na Maandiko 76 yalivyotayarishwa Oktoba 2015
Kuhimiza na kusaidia utafiti katika maendeleo ya ushirika
Jumla ya vyama vya ushirika 112 vilifanyiwa utafiti na Taasisi mbalimbali ikiwemo Shirikisho la Vyama vya Ushirika Tanzania (TFC), Chama Kikuu cha Vyama vya Akiba na Mikopo (SCCULT- 1992 Ltd) na Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi (MoCU). MoCU kupitia matawi yake ya mikoani na kikanda yaliyopo nchi nzima na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) walishirikiana kufanya tafiti za mara kwa mara na kutambua mahitaji ya wakati husika kwenye Vyama vya Ushirika kufikia Juni 2015.
Kufanya uchunguzi na ukaguzi kuhusu uendeshaji wa shughuli za ushirika
Jumla ya Vyama vya Ushirika 132 vilikaguliwa kufikia Oktoba 2017 kwa kuzingatia matakwa ya Sheria ya Vyama vya Ushirika Na 6 ya Mwaka 2013 ikilinganishwa na vyama 125 vilivyokaguliwa kufikia Juni 2015. Hili ni ongezeko la 5.6% ya mafanikio ya ukaguzi wa kawaida. Aidha, ukaguzi wa Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa vyama vya Ushirika ( COASCO) iliweza kukagua vyama vya Ushirika 41 kufikia Oktoba 2017 ikilinganishwa na ukaguzi na vyama vya ushirika 24 vilivyokaguliwa hadi kufikia Juni 2015. Hii ni sawa na ongezeko la 70% ya mafanikio.
Maliasili
Wanyamapori
Utekelezaji wa sera na sheria umezingatiwa katika kulinda mbuga za wanyamapori katika Hifadhi za Taifa (Mikumi, Udzungwa) Pori la Akiba la Selous, Pori Tengefu la Kilombero, Hifadhi za wananchi (Wildlife Management Area,s). Kesi mbalimbali zimefunguliwa Mahakamani na kutolewa ushahidi kwa waliokiuka.
Kwa kuzingatia Sera jumla ya Hifadhi tatu (3) za wananchi za uhifadhi wa Wanyamapori zimeanzishwa na wananchi wameanza kujipatia kipato. Hifadhi hizo (Wildlife Management Areas’s) ni zile za Jukumu, Wami –Mbiki, na ILUMA.
Hifadhi ya Jukumu inajumuisha vijiji 23 vya Wilaya ya Morogoro, Wami- Mbiki vijiji 24 vya Wilaya za Mvomero, Morogoro, Pwani na ILUMA vijiji 14 vya Wilaya za Kilombero na Ulanga.
Katika kusimamia ardhioevu (Wetlands) katika bonde la Ramsar la Kilombero ambalo sehemu yake ni Pori Tengefu la Kilombelo jumla ya Mifugo zaidi ya laki tano iliondolewa kwa kuendesha Operesheni maalum “Okoa Bonde la Kilombero”. Vyanzo vya maji vilivyokuwa vimekauka kwa sasa vimeanza kurudia hali yake ikiwa ni pamoja na Mito na Mabwawa ya asili. Kiasi cha Samaki pia kimeanza kuongezeka ambapo ni tegemeo kubwa kwa wananchi wazawa wa maeneo hayo. Pia maji katika bonde hilo yanategemewa kwa uzalishaji wa umeme, Kilimo cha Mashamba makubwa na madogo, Mifugo, Wanyama Pori na Matumizi ya nyumbani.
Kushiriki na kushauri utatuzi wa migogoro ya mipaka kati ya wananchi na Hifadhi zinazopakana nao. Jumla ya migogoro mitatu imeshashughulikiwa kati ya Hifadhi ya Mikumi na kijiji cha Maharaka Wilayani Mvomero, Hifadhi ya Mikumi na vijiji vya Lumango, Kielezo, Ruhembe na Mikumi Wilayani Kilosa pamoja na Hifadhi ya Taifa ya Milima ya Udzungwa na vijiji 11 vinavyopakana na hifadhi hiyo.
Misitu na Nyuki
Kusimamia sheria na Sera ya Misitu ikiwa ni pamoja na Upandaji miti, uvunaji, uhifadhi wa vyanzo vya maji na uanzishwaji wa Misitu ya jamii (PFM) kwa njia shirikishi. Jumla ya misitu ya jamii ipatayo 58 yenye ukubwa wa Ha 69,879 inayowanufaisha zaidi ya watu 74,073 ilianzishwa.
Shughuli za Ufugaji wa Nyuki
Shughuli za ufugaji nyuki kama njia mojawapo ya utunzaji wa mazingira na kujipatia kipato kwa wananchi zinafanyika maeneo tofauti ingawa bado ni kwa kiasi kidogo katika kila Halmashauri za Wilaya. Hadi kufikia 2017, Mkoa wa Morogoro umefikia kuwa na jumla ya mizinga ya ufugaji Nyuki ipatayo 17,299, kati ya hiyo mizinga 10,705 ni ya kisasa na 6,594 ni ya kienyeji. Halmashauri ya Wilaya yenye mizinga mingi zaidi ni Mvomero (mizinga 7550) ikifuatiwa na Kilombero (mizinga 2947).
Kwa kiasi kikubwa mazao ya nyuki yanayozalishwa mkoani Morogoro ni asali. Wastani wa uzalishaji wa asali kwa mwaka 2016/2017 ni kilogramu 48,721 ambapo wastani wa uzalishaji kwa mzinga mmoja ni kg 3.25. Wastani huo wa uzalishaji kwa mzinga ni chini kiwango cha kawaida cha uzalishaji kwa mzinga (kg 10-15 kg) kwa mizinga ya kisasa. Pamoja na uzalishaji kuwa bado ni mdogo, shughuli za ufugaji nyuki huzalisha ajira kwa watu takribani elfu tano ambao hujipatia wastani wa sh. 487,210,000/= kwa mwaka hivyo kuongeza kipato kwa wananchi
Kufuatilia mienendo ya kesi za ujangili na mara nyingine kutolea ushahidi mahakamani pamoja na kusaidia taasisi na Halmashauri uzuiaji wa ujangili.
Doria mbalimbali zilifanyika Wilayani na Taasisi zote za maliasili.
Wahalifu wa nyara na rasilmali zote za maliasili walikamatwa aidha kutozwa faini na kufunguluwa kesi mahakamani.
Biashara na Viwanda
Viwanda
Viwanda vilivyojengwa na Serikali
Jumla ya viwanda 16 vilijengwa na Serikali Mkoani Morogoro ambapo 14 vilibinafsishwa, 2 havikubinafsishwa. Viwanda ambavyo havikubinafsishwa ni:- Mzinga Corporation; na Tanzania Railway Workshop.
Orodha ya viwanda vilivyobinafsishwa na ubinafsishaji uliofanyika ni ifuatayo:-
Na
|
Jina la Kiwanda
|
Uuuzaji Ulivyofanyika
|
1
|
21 Century Textile Mill Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
2
|
Kilombero Sugar Co. Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Hisa
|
3
|
Mtibwa Sugar Estates Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Hisa
|
4
|
Tanzania Tobacco Processors Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
5
|
Ushirikiano Wood Products
|
Kilibinafsishwa kwa kupitia ufilisi-
orderly liquidation |
6
|
Tanzania Packaging Manufacturers – TPM (1998) Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kupitia Ufilisi-
orderly liquidation |
7
|
Morogoro Tanneries Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Hisa
|
8
|
MOPROCO – Kiwanda cha Mafuta ya Kula
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
9
|
Morogoro Canvas Mill Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
10
|
Morogoro Ceramics Ware Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali moja moja –
assets striping |
11
|
Morogoro Shoe Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Hisa na kufilisiwa
baada ya kuungua |
12
|
Mang’ula Mechanical & Macine Tools (MMMT) Ltd
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
13
|
Dakawa Rice Mill Complex
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
14
|
New Morogoro Rice Mill
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
Old Morogoro Rice Mill
|
Kilibinafsishwa kwa kuuza Mali
|
Kati ya viwanda hivyo 14 vilivyobinafsishwa, viwanda 5 vinafanya kazi vizuri ambavyo ni:- 21st Century Textile Mill Ltd, Kilombero Sugar Company Ltd, Mtibwa Sugar Estates Ltd, Tanzania Tobacco Processors Ltd; na Morogoro Rice Mills.
Viwanda 4 vilivyobinafsishwa vilivyofungwa hadi sasa ni:- Morogoro Canvas Mill Ltd, Dakawa Rice Mill Complex Ltd, Ushirikiano Wood Products; na Mang’ula Mechanical and Machine Tools (MMMT) Ltd.
Viwanda 2 vilivyobinafsishwa ambavyo kwa sasa ni majengo au eneo tu bila mitambo ni:- Morogoro Ceramics Ware Ltd; na Morogoro Shoe Ltd.
Kiwanda kimoja ki
lichokuwa kimefungwa ambacho kimefufuliwa ni Kiwanda cha Mafuta ya Kula MOPROCO, kwa sasa kinaitwa Abood Seed Oil Ltd.
Viwanda 2 vilivyobinafsishwa vinavyofanya kazi kwa kusuasua ni:- Morogoro Tanneries Ltd – Ace Leather Ltd; na Tanzania Packaging Manufacturers Ltd.
Idadi ya Viwanda Mkoani Morogoro
Kwa mujibu wa takwimu za NBS – National Bureau of Statistics, Mkoa wa Morogoro una viwanda vikubwa 20, Viwanda vya Kati 14, Viwanda Vidogo 302; na Viwanda Vidogo Sana 3,038. Mgawanyo wa viwanda hivyo kiwilaya ni kama ifuatavyo:-
Na.
|
Halmashauri
|
Viwanda Vikubwa
|
Viwanda vya Kati
|
Viwanda Vidogo
|
Viwanda Vidogo sana
|
Jumla
|
1
|
Morogoro Manispaa
|
10
|
3
|
120
|
587
|
720
|
2
|
Kilombero DC na Mji
|
4
|
4
|
59
|
764
|
831
|
3
|
Morogoro DC
|
2
|
1
|
14
|
374
|
391
|
4
|
Kilosa
|
1
|
3
|
45
|
614
|
663
|
5
|
Ulanga na Malinyi
|
1
|
1
|
30
|
272
|
304
|
6
|
Mvomero
|
2
|
2
|
19
|
265
|
288
|
7
|
Gairo
|
0
|
0
|
15
|
162
|
177
|
Jumla
|
20
|
14
|
302
|
3,038
|
3,374
|
Mwelekeo wa ujenzi wa Viwanda Vpya Mkoani Morogoro
Kufuatia Kongamano la Uwekezaji la Mkoa wa Morogoro lililofanyika tarehe 29 na 30 Septemba 2016, wawekezaji wamejitokeza na kuonesha nia ya kuwekeza Mkoani Morogoro. Wawekezaji hao watawekeza kwenye viwanda vifuatavyo:-
i) Kiwanda cha kutengeneza Sigara – Philip Morris (T) Ltd. – Wilayani Morogoro
ii) Kiwanda cha Kuchakata Nyama – Nguru Hills Ranch Ltd., eneo la Nguru ya Ndege, Mvomero (Ufadhili wa LAPF)
iii) Kiwanda cha Kufungasha Mikunde aina ya Choroko, Dengu, Kunde na Mbaazi – Mahashree Agro Processing Ltd.
iv) Viwanda vya Sukari Mkulazi 1(Ngerengere); na Mkulazi 2 (Mbigiri): Kampuni ya Mkulazi Holdings Ltd. (NSSF)
v) Kiwanda cha Sukari – kitaanzishwa na mwekezaji Jigish Kumar, Wilayani Kilosa.
vi) Kiwanda cha Kuyeyusha chuma – kitaanzishwa na mwekezaji Jigish Kumar, Wilayani.
vii) Kiwanda cha Kuunganisha Matrekta – kitaanzishwa na Wawekezaji kutoka Jamhuri ya Beralus.
viii) Kiwanda cha Kutengeneza Hamira (yeast) – kitaanzishwa na Sinapis Investment (pvt) Holdings Ltd, Zimbabwe.
ix) Kiwanda cha Sukari – kitaanzishwa na Morogoro Sugar Industry Ltd. , Wilaya ya Morogoro, eneo la Kisaki.
x) Kiwanda cha kutengeneza bidhaa za pamba (Pedi, gauze, pamba za hospitali) – Sinapis na Mifuko ya Jamii.
xi) Kiwanda cha kusindika Nyama – Sinapis na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
xii) Kiwanda cha Kusindika Maziwa - Sinapis na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
xiii) Kiwanda cha Kutengeneza Ethanol - Sinapis na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
xiv) Kiwanda cha Kutengeneza Alcohol - Sinapis na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
xv) Kiwanda cha Kutengeneza Industrial sugar - Sinapis na Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
xvi) Kiwanda cha Kutengeneza Premix kwa ajili ya Mikate.
xvii) Kiwanda cha kutengeneza Ethanol – ILLOVO
Biashara
Kwa kipindi cha miaka miwili ya Serikali ya Awamu ya Tano kumekuwa na ongezeko la urasimishaji wa shughuli za biashara ikilinganishwa na miaka miwili ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Nne. Shughuli za biashara zilizorasimishwa zimechangia kwenye ongezeko la ajira kwa wananchi wa Mkoa wa Morogoro.
Ongezeko hilo kwa ulinganisho ni sawa na 12.23%. Urasimishaji huo wa shughuli za biashara unajitokeza katika utoaji wa leseni za biashara kwa kila Mamlaka ya Serikali za Mitaa kama inavyoonekana kwenye jedwali lifuatalo:-
Mwaka |
H A L M A S H A U R I
|
Jumla |
||||||||
Ulanga
|
Kilombero
|
Kilosa
|
Mvomero
|
Morogoro
|
Manispaa
|
Gairo
|
Malinyi
|
Ifakara
|
||
2013/2014
|
272
|
1,308
|
1,293
|
707
|
429
|
3,605
|
471
|
0
|
0
|
8,085
|
2014/2015
|
468
|
1,404
|
1,627
|
1,012
|
515
|
5,923
|
554
|
0
|
0
|
11,503
|
Jumla A
|
740
|
2,712
|
2,920
|
1,719
|
944
|
9,528
|
1,025
|
0
|
0
|
19,588
|
2015/2016
|
309
|
1,342
|
1,626
|
1,141
|
1,136
|
4,257
|
598
|
0
|
0
|
10,409
|
2016/2017
|
302
|
696
|
1,403
|
1,307
|
327
|
4,800
|
525
|
875
|
1,340
|
11,575
|
Jumla B
|
611
|
2,038
|
3,029
|
2,448
|
1,463
|
9,057
|
1,123
|
875
|
1,340
|
21,984
|
Pamoja na viwanda vilivyopo, jitihada zaidi zinafanyika kubaini maeneo mengine ya uzalishaji wa viwanda vingine vidogo na vya kati vyenye kutumia teknolojia rahisi na sahihi kutokana na kuwepo kwa fursa kubwa ya viwanda vya usindikaji wa mazao ya Kilimo na Mifugo Mkoani humu.
Endapo Sekta ya Viwanda itasimamiwa na kuendelezwa kikamilifu Mkoani Morogoro, ni dhahiri kwamba, umaskini wa kipato miongoni mwa wananchi wa Mkoa huu utapungua kwa kiasi kikubwa na hivyo, kuwawezesha kuwa na maisha bora.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.