• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Elimu

I























































SEKTA YA ELIMU  

Idara ya Elimu inalo jukumu la kusimamia utoaji wa Elimu katika ngazi za Awali, Msingi, Sekondari, Elimu ya Watu Wazima na Elimu ya Juu. Taasisi za elimu, zilizopo Mkoani hadi sasa ni kama inavyoonekana katika jedwali hapa chini:-

UANDIKISHAJI WA WANAFUNZI 

Katika mwaka 2017, uandikishaji wa wanafunzi katika madarasa ya awali, darasa la kwanza na kidato cha kwanza ni kama ifuatavyo:-

 Jedwali 2: Uandikishaji wa wanafunzi

DARASA

LENGO

HALISI

WAV

WAS

JUMLA

WAV

WAS

JUMLA

%

AWALI

31796

31905

63701

35828

35317

71145

111.7

DARASA LA I

38566

36918

75484

45146

43416

88554

117.3

KIDATO CHA I

12560

13600

26160

10664

11360

22024

86

JUMLA

82922

82423

165345

91638

90093

181723

109.9

Chanzo:Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Uandikishaji wa wanafunzi madarasa ya awali na darasa la kwanza umeongezeka kutoka asilimia 83 mpaka asilimia 117.3  kwa darasa la kwanza, na asilimia 78 mpaka 117.7 kwa madarasa ya awali. Ongezeko hili limetokana sera ya utoaji wa elimu msingi bila malipo iliyoanza kutekelezwa katika kipindi cha mwaka  2016.

 

IDADI YA WANAFUNZI KWA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI ZA SERIKALI NA BINAFSI 2017

Mahudhurio ya wanafunzi darasani yameongezeka toka asilimia 86 Kwa mwaka 2016 hadi asilimia 95 kwa mwaka 2017, hii imetokana pia na kuondolewa shuleni kwa michango mbalimbali waliyokuwa wanatozwa wazazi.  Pamoja na mahudhurio hayo yanayoridhisha bado wapo wanafunzi wanaokatiza masomo yao kwa utoro. Halmashauri kwa kushirikiana na Kamati   na bodi za shule wanaendelea kuchukua hatua kwa wazazi wanaosababisha utoro kwa watoto wao kwa mujibu wa sheria.

Uwiano wa mwalimu na mwanafunzi ni 1: 57 kwa sasa badala ya 1:40 kama inavyotakiwa kwa mujibu wa sera ya elimu. Halmashauri zinafanya jitihada za kurekebisha ikama kwa shule zenye upungufu mkubwa kila zinapopata fedha za kuhamisha. Tunaiomba serikali ione uwezekano wa kutoa ajira kwa walimu   ili kuziba mapengo yaliyopo katika shule zilizo nyingi.

Jedwali 6: Mahitaji ya Walimu Shule za Sekondari

S/N

MAHITAJI YA WALIMU

MAHITAJI

WALIOPO

PUNGUFU/ZIADA

1

SANAA

3135

3848

+713

2

SAYANSI NA HISABATI

1869

1231

744

Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017

Kwa shule za sekondari upungufu upo kwa walimu wa sayansi na hisabati, lakini kuna ziada ya walimu wa masomo ya sanaa kama inavyoonekana katika jedwali. Hata hivyo tunaishukuru sana serikali kwa kutuletea  walimu wa sayansi 152 kwa kipindi cha 2016/2017  idadi hii ya walimu imeongeza nguvu kazi katika shule na matarajio ni wanafunzi kufaulu mitihani yao kwa kiwango cha juu kwa kuwa sasa wanapata vipindi kwa masomo yote.

 MIUNDOMBINU YA SHULE ZA MSINGI NA SEKONDARI

Takwimu zinaonesha kwamba upo upungufu mkubwa wa miundombinu katika shule za msingi na sekondari Mkoani. Jitahada zinaendelea kufanyika kuhakikisha kwamba  miundombinu katika shule inatosheleza mahitaji. Jitihada hizi ni pamoja na

  • Kuhamasisha jamii kuchangia nguvu kazi  kama vile kufyatua tofali, kukusanya mawe , mchanga n.k
  • Halmashauri kutenga fedha  katika bajeti zake za vyanzo vya ndani na nje ili kuweza kukamilisha majengo ambayo yameanzishwa na wananchi
  • Kuomba wahisani wa ndani na nje kusaidia ujenzi wa miundombinu ya shule.

Jedwali Na : 7 Miundombinu ya Shule za Msingi na Sekondari

AINA

MSINGI

SEKONDARI

MAHITAJI

YALIYOPO

PUNGUFU

MAHITAJI

YALIYOPO

PUNGUFU

MADARASA

11700

5268

6432

2286

2057

229

NYUMBA ZA WALIMU

12729

1812

10917

4845

494

4351

MATUNDU YA VYOO

20415

7812

12603

3489

2043

1446

MADAWATI

162248

160695

1553

71568

70359

1209

OFISI ZA WALIMU

843

0

843

187

49

138

MAABARA

0

0

0

549

272

277

Chanzo: Ofisi ya Mkuu wa Mkoa 2017

Tunaishukuru sana Serikali ya awamu ya tano kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia kwa kutuletea vifaa vya maabara kwa shule zote za sekondari Mkoani, hadi sasa watahiniwa wote wa kidato cha nne (4) wamefanya mitihani ya “real practical” na sio “altenative to practical” kwa kuwa shule sasa zina vifaa vya kutosha. Mkoa unaendelea kuhimiza  na kusimamia ukamilishaji wa ujenzi wa maabara kwa shule zote ifikapo JUNI 2018.

MAENDELEO YA UTOAJI WA TAALUMA 

Mkoa unaendelea kusimamia utoaji wa taaluma katika shule za msingi na sekondari na umeendelea kufanya vizuri katika matokeo ya mitihani mbalimbali ya kitaifa. Mfano kwa mwaka 2016 katika mtihani wa darasa la saba mkoa ulikuwa na wastani wa alama hamsini na nane  (58)  na kushika nafasi ya 23 kitaifa , kwa mwaka 2017 Mkoa umepata wastani wa alama   sabini (70.78) na kushika nafasi ya kumi na moja  (11)  Kitaifa.

Mkoa umeweka mikakati ifuatayo ili kuendelea kuimarisha utoaji wa taaluma katika shule za msingi na sekondari:-

Mikakati ya kuboresha taaluma Mkoani.

  • Kusimamia ufundishaji wa masomo  shuleni kwa madarasa yote
  • Kudhibiti utoro wa rejareja kwa wanafunzi na walimu
  • Kurekebisha ikama katika shule zenye upungufu mkubwa wa walimu.
  • Kufanya ukaguzi wa shule wa mara kwa mara
  • Kutoa mafunzo ya ziada kwa wanafunzi wenye uwezo mdogo darasani na wale wa madarasa yenye mitihani
  • Kuwajengea uwezo Walimu ili waweze kuandaa masomo ipasavyo na hatimaye kufundisha ipasavyo
  • Kuwasimamia Waratibu Elimu Kata kwa dhati ili waweze kusimamia ipasavyo ufundishaji madarasani katika shule zilizoko kwenye kata wanazosimamia
  • Kuendelea kuhimiza uchangiaji wa chakula cha mchana kwa wanafunzi wote ili waweze kupokea maarifa ipasavyo
  • Kuwawezesha Wathibiti Ubora wa shule ili waweze kukagua shule nyingi na kuwajengea uwezo walimu.
  • Kuendelea kuhamasisha jamii kuchangia ujenzi wa miundo mbinu ya shule ili wanafunzi waweze kusoma katika mazingira mazuri.
  • Halmashauri kuendelea kutenga katika bajeti zake fedha kwa ajili ya kuimarisha miundombinu ya shule  katika shule zenye upungufu mkubwa.

UTEKELEZAJI WA UTOAJI WA ELIMU MSINGI BILA MALIPO MKOANI

Mkoa umeendelea kutekeleza utaoaji wa elimu msingi bila malipo kwa kutoa elimu kwa wadau wote wa elimu ili kila mmoja awe na uelewa wa nini kinatakiwa kufanyika, Elimu hiyo inatolewa kupitia vikao mbalimbali kuanzia ngazi za mitaa hadi Mkoa. Vile vile idara ya elimu imesambaza nyaraka zote muhimu zinazotoa maelekezo kuhusu elimu  ya msingi bila malipo sambamba na kutoa ufafanuzi wa Sera hiyo pale panapohitajika. Hadi sasa shule zote za Msingi na Sekondari  zinaendelea kutekeleza sera hiyo bila matatizo. Pale ambapo imeonekana viongozi ngazi ya shule kwenda kinyume na sera, hatua zimechukuliwa  dhidi yao mara moja.

   i.   MAPOKEZI YA FEDHA ZA ELIMU MSINGI BILA MALIPO  

Hadi kufikia Oktoba 2017, halmashauri zimepokea kiasi cha Tshs  2,731,302,76  kama inavyoonekana katika jedwali lifuatalo:-

Jedwali Na.8 Mapokezi ya fedha za Elimu Msingi kwa  mwaka 2017/2018

S/N

HALMASHAURI

MSINGI

SEKONDARI

SHULE ZA BWENI/MAALUM

JUMLA

1

KILOMBERO

130,970,344

95,819,585

0

226,789,929

2

KILOSA

291,973,500

859,521,897

881,999,549

226,789,929

3

MOROGORO

205,945,559

118,952,863

0

453,579,858

4

MANISPAA

87,148,594

150,385,749

126,270,127

907,159,716

5

ULANGA

65,002,597

38,168,110

90,984,011

194,154,718

6

MVOMERO

212,192,893

65,786,961

96,970,795

374,950,649

7

GAIRO

67,771,750

27,247,270

0

95,019,020

8

MALINYI

43,915,726

22,966,896

0

66,882,622

9

IFAKARA

65,081,520

59,645,352

61,249,448

185,976,320

10

JUMLA MKOA

1,170,002,483

1,438,494,683

1,257,473,930

2,731,302,761

Chanzo:-Halmashauri za Wilaya 2017

Angalizo:-Fedha hizi ni kwa ajili ya uendeshaji wa shule, ukarabati mdogo mdogo, chakula kwa shule za bweni na watoto wenye mahitaji maalumu .Fedha hizi  huingizwa katika akaunti za shule moja kwa moja.

ii.   MAPOKEZI YA FEDHA ZA UJENZI WA SHULE ZA SEKONDARI NA UKARABATI

Tunaishukuru sana serikali ya awamu ya tano kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu kwa shule za sekondari. Tunayo furaha kukujulisha kwamba tayari tumepokea fedha kama ifuatavyo:-

  • Halmashauri ya Ifakara  shule ya  sekondari Ifakara Tshs 1,334,298,216. kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa, mabweni na maabara. Ukarabati unaendelea.
  • Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro  shule ya sekondari Kilakala Tshs 935,584,126.72 kwa ajili ya ukarabati wa mabweni, madarasa, maabara za sayansi, jiko na bwalo la chakula pamoja na miundombinu ya shule. Shughuli za ukarabati zinaendelea.
  • Halmashauri ya wilaya ya Mvomero shule ya sekondari Sokoine Memorial Tshs 1,704,000,000.00. kwa ajili ya ujenzi wa shule ya kidato cha tano na sita  inayotarajia kufunguliwa mwaka 2018. pamoja na ukarabati wa shule ya sekondari Mzumbe Tshs 999,739,458.81. Shughuli za ukarabati na ujenzi zinaendelea katika maeneo yote mawili.
  • Shule ya sekondari Mafiga Tshs 109, 000,000.00 kwa ajili na ujenzi wa maabara, vyumba vya madarasa, na matundu ya vyoo. Ujenzi umekamilika.

3.1.7     USIMAMIZI WA MASLAHI YA WALIMU MKOANI

i.  Madeni ya walimu

Mkoa umeratibu zoezi la uhakiki wa madeni ya walimu Mkoani na jumla ya madai ya walimu ni Tshs 3,107,986,281.99. yakiwemo madai ya Uhamisho ,likizo,Matibabu.

ii. Upandishwaji madaraja ya walimu

Mkoa  umewasilisha kwa Katibu Mkuu OR-TAMISEMI  jumla ya walimu 5288 wakiwemo wa shule za msingi 4240 na sekodari 1048 wanaostahili kupanda madaraja kwa mwaka 2017 kama ilivyoelekezwa na Katibu Mkuu OR-TAMISEMI









Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • MAONESHO YA NANENANE July 27, 2022
  • View All

Habari Mpya

  • WAALIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA USALAMA NA MALEZI BORA KWA WANAFUNZI.

    January 28, 2023
  • MAAFISA ELIMU WAAGIZWA KUSIMAMIA MATUMIZI YA FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO

    January 28, 2023
  • RC FATMA MWASSA AWAAPISHA WAKUU WA WILAYA WAWILI.

    January 27, 2023
  • REA MKOANI MOROGORO KUMCHUKULIA HATUA MKANDARASI WA KAMPUNI YA HXJDL.

    January 26, 2023
  • View All

Video

Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.