MIFUGO
Mkoa wa Morogoro kwa sasa unakadiriwa kuwa na jumla ya ng’ombe 840,944 Mbuzi 356,169, Kondoo 125,652, Punda 9,867, Nguruwe 45,238, Mbwa 46,396, Paka 45,766, Kanga 83,654, Bata 61,443, Kuku wa asili 5,244,894.
Idadi ya watumishi
Mkoa wa Morogoro una jumla ya watumishi 251 wa sekta ya Mifugo kama jedwali linavyoonesha hapo chini
NA |
KADA
|
WALIOPO
|
MAHITAJI
|
UPUNGUFU
|
1 |
Madaktari wa Mifugo
|
10 |
16 |
6 |
2 |
Maafisa Mifugo
|
41 |
59 |
18 |
3 |
Maafisa Mifugo wasaidizi
|
200 |
543 |
343 |
JUMLA |
251 |
618 |
367 |
Miundombinu ya Mifugo
Mkoa una jumla ya Minada 27 Majosho 69 malambo 50 mabanio 23 Machinjio 9 Makaro 63 Mabanda ya ngozi 8, Maabara 2, vituo vinavyotoa huduma ya mifugo (vet centre) 28 na Hospitali ya mifugo 1
Uzalishaji wa maziwa
Jumla ya lita 6,600,000 za maziwa zenye thamani ya Tsh 6,600,000,000/= Zilizalishwa katika Mkoa wa morogoro kwa kipindi cha Januari hadi Novemba,2017.
Uzalishaji mayai
Jumla ya Trei za mayai 342,521 yenye thamani ya Tsh. 2,568,907,500/= yalizalishwa na kuuzwa katika Mkoa wa morogoro kwa kipindi cha Januari hadi Novemba,2017.
Jumla ya ng’ombe 108,649 wenye thamani ya Tsh. 43,459,600,000 mbuzi 10,340 wenye thamani ya Tsh. 517,000,000 na kondoo 29,777 zikiwa na thamani ya Tsh. 1,488,850,000 waliuzwa katika minada kwa kipindi cha Januari hadi Novemba,2017.
Mauzo ya Ngozi
Vipande vya ngozi kwa ipindi cha Januari hadi Novemba 2017 ni kama ifuatavyo; ngozi za ng’ombe vipande 5841 vyenye thamani ya shilingi 269,205,000 mbuzi vipande 28015 vyenye thamani ya shilingi 28,015,000 na kondoo vipande 13390 vyenye thamani ya shilingi 13,390,000.
Mauzo ya Kuku
Kwa kipindi cha Januari 2017 hadi desemba 2017 jumla ya kuku 577,000 wenye thamani ya shilingi 5,770,000,000 waliuzwa.
Jumla ya ngombe 196 wamepandishwa kwa njia ya chupa na jumla ya ndama 175 wamezaliwa kwa njia ya chupa kwa kipindi cha Januari hadi Novemba 2017.
Kwa mwaka huu 2017 Shirika la Land O’ Lakes kwa kushirikiana na Kampuni ya ABEA wanatoa huduma ya uhimilishaji na elimu kwa wafugaji juu ya uboreshaji wa koosafu za ng’ombe katika Halmashauri zote 9 za Mkoa wa Morogoro. Wafugaji wamehamasishwa kuvuna mifugo yao na kununua madume bora ya Boran kwa ajili ya kuboresha koosafu za mifugo yao ambapo hadi hivi sasa jumla ya wafugaji 10 wamenunua madume wapatao 50 wa aina ya Borani.
Utekelezaji wa Utambuzi wa Mifugo hadi kufikia Tarehe 15 Januari 2018
Katika kutekeleza zoezi la Usajili, Utambuzi na Ufuatiliaji wa mifugo, hadi kufikia tarehe 15/1/2018 jumla ya ng’ombe 703,753 wamepigwa Chapa kati ya ng’ombe 841,044 waliosajiliwa sawa na asilimia 84%. Utekelezaji kwa kila Halmashauri ni kama ifuatavyo;
Na |
HALMASHAURI |
WAFUGAJI WALIOSAJILIWA. |
IDADI YA NG’OMBE WALISAJILIWA/ LENGO |
IDADI YA NG’OMBE WALIOPIGWA CHAPA |
ASILIMIA YA NG’OMBE WALIOPIGWA CHAPA % |
1 |
Morogoro DC
|
1,481 |
116,173 |
81,710 |
70 |
2 |
Manispaa
|
465 |
9,377 |
8,187 |
87 |
3 |
Mvomero
|
2,929 |
189,708 |
161,030 |
85 |
4 |
Kilosa
|
6,558 |
208,279 |
147,218 |
70 |
5 |
Malinyi
|
5,154 |
122,776 |
122,776 |
100 |
6 |
Ifakara TC
|
252 |
5,720 |
7,030 |
100 |
7 |
Kilombero
|
5,853 |
91,314 |
91,314 |
100 |
8 |
Gairo
|
2,181 |
50,927 |
37,718 |
74 |
9 |
Ulanga
|
2,503 |
46,770 |
46,770 |
100 |
JUMLA KIMKOA |
27,376 |
841,044
|
703,753 |
84 |
Mikakati ya kutatua changamoto katika Sekta ya Mifugo
Kusimamia Sheria na 12 ya mwaka 2010 ya Utambuzi, Usajili na Ufuatiliaji mifugo kwa kupiga chapa ng’ombe.
Kila Halmashauri imeweka katika bajeti ya mwaka 2017/2018 fedha kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mifugo ili kuboresha afya za mifugo.
Zoezi la mpango wa matumizi bora ya ardhi linaendelea katika Halmashauri za Wilaya ya Ulanga, Malinyi na Kilombero, zoezi hili litaainisha maeneo kwa ajili ya malisho
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.