Sekta ya Kilimo
Utangulizi.
Mkoa wa Morogoro una eneo la hekta 2,226,396 linalofaa kwa Kilimo ambapo eneo linalolimwa kwa sasa ni wastani wa Hekta 960,034 sawa na asilimia 43. Eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji ni hekta 1,510,339.51 na eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni wastani wa hekta 79,429 sawa na asilimia 5. Mkoa una Skimu za Umwagiliaji 106 (asili na zilizoendelezwa) zinazotambulika zenye ukubwa wa hekta 323,758.15.
Asilimia 75 ya Wananchi wa Mkoa wa Morogoro wanategemea kilimo kwa ajili ya Ajira, Kipato na Chakula. Mazao ya Chakula yanayozalishwa kwa wingi ni Mpunga, Mahindi, Ndizi, Viazi vitamu, Muhogo, Mtama na Maharage. Mazao ya biashara yanayozalishwa kwa wingi ni Miwa, Ufuta, Alizeti, Mkonge, Korosho, Pamba, Kokoa, Matunda, Viungo na Mboga mboga.
Mkoa wa Morogoro una jumla ya Maafisa Ugani Kilimo 462, mahitaji ni 960 na hivyo upungufu ni watumishi 498 kama ilivyo kwenye jedwali namba 20.
Jedwali Na. 1: Idadi ya Watumishi wa Kilimo Waliopo Kwenye Halmashauri
H/Wilaya |
Mahitaji ya Maafisa Ugani Kilimo |
Waliopo |
Upungufu |
Gairo
|
55 |
29 |
26 |
Mji Ifakara
|
78 |
49 |
29 |
Kilosa
|
184 |
89 |
95 |
Mlimba
|
81 |
34 |
47 |
Malinyi
|
65 |
23 |
42 |
Morogoro MC
|
34 |
33 |
1 |
Morogoro DC
|
192 |
73 |
119 |
Mvomero
|
179 |
102 |
77 |
Ulanga
|
87 |
26 |
61 |
RS Morogoro
|
5 |
4 |
1 |
Jumla
|
960 |
462 |
498 |
Katika msimu wa Kilimo wa mwaka 2021/2022, Mkoa ulilenga kulima hekta 940,509.07 ili kuvuna tani 3,035,485.96 za mazao ya chakula. Kwa mazao ya biashara Mkoa ulilenga kulima hekta 205,083.83 ili kuvuna tani 2,704,383.95.
Utekelezaji wake mazao ya chakula, Mkoa ulilima hekta 681,550.68 sawa na asilimia 72 ya lengo na kuvuna tani 1,775,511.71 sawa na asilimia 58 ya lengo. Kwa mazao ya biashara, Mkoa ulilima hekta 155,773.76 sawa na asilimia 76 ya lengo na kuvuna tani 1,743,853.87 sawa na asilimia 64 ya lengo. Kwa msimu wa 2021/2022-unyeshaji wa mvua uliathiri uzalishaji wa mazao kwani Mvua zilianza kwa kuchelewa na hazikunyesha kwa mtawanyiko mzuri na pia ziliwahi kuisha hivyo, kusababisha kutofikia malengo tuliyojiwekea.
Kwa msimu wa mwaka 2022/2023, Mkoa umelenga kulima hekta 938,448.30 ili kuvuna tani 3,068,101.58 za mazao ya chakula na Mazao ya biashara Mkoa umelenga kulima hekta 226,900.73 ili kuvuna tani 2,909,321.78.
Jedwal Na. 2: Mchanganuo wa Eneo Linalofaa kwa Kilimo na Eneo Linalolimwa
Halmashauri |
Eneo linalofaa kwa Kilimo |
Eneo linalo lengwa kulimwa kwa sasa |
% Eneo faa vs lengwa |
Mazao Makuu 5 yanayolimwa kwa wingi kwa sasa |
Mazao ya Kipaumbele |
Gairo
|
111,080.4
|
100,610.72
|
91%
|
Mahindi, Viazi vitamu, Maharage, Alizeti na Mbaazi. |
Mahindi na Alizeti. |
Ifakara (TC)
|
131,271.4
|
46,965.40
|
36%
|
Miwa, Mpunga, Mahindi, Ndizi na Muhogo |
Mpunga na Miwa. |
Kilosa
|
417,210
|
262,830.00
|
63%
|
Miwa, Mahindi, Mpunga, Viazi Vitamu na Mkonge. |
Mkonge na Mpunga. |
Malinyi
|
127,761.06
|
72,291.70
|
57%
|
Mpunga, Mahindi, Ufuta, Korosho na Viazi vitamu. |
Korosho, Ufuta/ Mpunga |
Manispaa (M)
|
8,004
|
6,145.33
|
77%
|
Mahindi, Ndizi, Nyanya, Vitunguu na Viungo |
Nyanya na Mahindi |
Morogoro (DC)
|
447,000
|
216,241.50
|
48%
|
Mpunga, Ndizi, Mahindi, Muhogo, Ufuta na Viungo |
Mpunga na Ufuta/ Viungo |
Mlimba
|
383,884.4
|
159,850.60
|
42%
|
Mpunga, Ndizi, Ufuta, Kokoa na Mahindi |
Mpunga na Ufuta/ Kokoa |
Mvomero
|
549,375
|
202,977.00
|
37%
|
Mpunga, Mahindi, Miwa, Maharage na Nyanya. |
Mpunga/ Malisho |
Ulanga
|
245,600
|
97,436.78
|
40%
|
Mpunga, Ufuta, Pamba, Kunde na Mahindi. |
Korosho na Ufuta/ Karanga Miti |
Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri, (2022)
Hali ya chakula kwa msimu wa 2022/2023 ni ya wastani katika Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro kutokana na mavuno ya msimu wa 2021/2022 ambapo Mkoa ulivuna tani 1,775,511.71 sawa na asilimia 58 ya lengo la kuvuna tani 3,035,485.96 ya mazao yote ya chakula. Uzalishaji wa Mazao ya chakula ulishuka kwa asilimia 42 ya lengo kutokana na mvua kuchelewa kuanza, kuwa na kipindi kirefu cha jua na mvua kuisha mapema wakati mazao bado hayajakomaa. Hata hivyo, Halmashauri zote zilivuna Mazao ya chakula kwa utoshelevu hadi ziada.
Jedwal Na. 3: Uzalishaji wa mazao ya chakula kwa kila Halmashauri 2021/2022
Halmashauri |
Malengo |
Utekelezaji wa Malengo |
||||
Eneo lengwa (ha) |
Makisio ya uzalishaji (tani) |
Eneo lililolimwa (ha) |
% ya lengo la hekta |
Uzaliishaji (tani) |
% ya uzalishaji |
|
Gairo
|
79,727.67 |
218,233.14 |
61,161.29 |
77% |
84,787.43 |
39% |
Ifakara
|
39,295.60 |
180,507.40 |
32,965.70 |
84% |
86,146.90 |
48% |
Mlimba
|
135,565.50 |
419,519.30 |
121,171.50 |
89% |
385,099.00 |
92% |
Kilosa
|
191,077.00 |
579,610.00 |
111,260.00 |
58% |
265,373.00 |
46% |
Malinyi
|
73,995.70 |
219,696.08 |
61,973.00 |
84% |
132,597.45 |
60% |
Morogoro (DC)
|
174,547.00 |
564,142.70 |
158,870.00 |
91% |
448,819.17 |
80% |
Morogoro (MC)
|
5,751.16 |
23,085.62 |
5,648.88 |
98% |
13,104.84 |
57% |
Mvomero
|
163,177.00 |
545,837.00 |
73,456.00 |
45% |
211,604.00 |
39% |
Ulanga
|
77,372.44 |
284,854.72 |
55,044.31 |
71% |
147,979.93 |
52% |
Mkoa
|
940,509.07 |
3,035,485.96 |
681,550.68 |
72% |
1,775,511.72 |
58% |
Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri, 2022
Aidha, kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi ya Mwaka 2022 idadi ya watu katika Mkoa wa Morogoro ni 3,197,104. Kutokana na idadi hiyo ya watu mahitaji ya Chakula kwa mwaka 2022/2023 yalikadiriwa kuwa tani 758,512.92 na kufanya Mkoa kuwa na ziada ya chakula tani 1,016,998.79 bila Mlinganisho wa Nafaka. Kuanzia Mwaka 2014/2015 hadi 2021/2022 Mkoa umekuwa ukijitosheleza kwa chakula na kuwa na ziada ni kama ifuatavyo.
Jedwal Na. 4: Uzalishaji na Mahitaji ya Chakula 2014/2015 Hadi 2021/2022
Mwaka |
Eneo lililo limwa (He) |
Uzalishaji (Tani) |
Mahitaji ya chakula (Tani) |
Ziada (Tani) |
2014/2015
|
589,231.00 |
1,877,942.1 |
565,779.35 |
1,312,162.75 |
2015/2016
|
563,826.18 |
1,597,895.65 |
578,446.05 |
1,019,449.60 |
2016/2017
|
738,282.00 |
2,298,859.00 |
591,112.76 |
1,707,746.24 |
2017/2018
|
808,669.00 |
2,262,227.00 |
603,779.46 |
1,658,447.54 |
2018/2019
|
784,320.90 |
2,229,745.92 |
616,446.16 |
1,613,299.76 |
2019/2020
|
758,568.90 |
2,016,332.20 |
629,112.86 |
1,387,219.34 |
2020/2021
|
735,230.97 |
2,113,776.38 |
651,573.91 |
1,462,202.47 |
2021/2022
|
681,550.68 |
1,775,511.71 |
758,512.92 |
1,016,998.79 |
2022/2023
|
Mkoa umelenga kulima Hekta 938,448.30 ili kuvuna tani, 3,068,101.58 za mazao ya chakula.
|
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri za Mkoa wa Morogoro 2014/2015 Hadi 2022/2023
Jedweli Na. 5: Wastani wa Bei za Vyakula Sokoni
Aina ya mazao |
Bei (Tsh.) Desemba, 2022 |
Bei (Tsh.) Januari 2023 |
Bei (Tsh.) Februari 2023 |
Gunia la Mahindi (Kg 100)
|
120,245/= |
120,245/= |
105,450/= |
Gunia la Mpunga (Kg 100)
|
132,812.50/=- |
187,500/= |
187,500/= |
Unga wa Sembe (Kg 1)
|
2,000/= |
2,000/= |
2,000/= |
Unga wa Ngano (Kg)
|
2,000/= |
2,000/= |
2,000/= |
Mchele (Kg 1)
|
2,800/=-3,400/= |
2,800/=3,400/= |
2,800/=3,400/ |
Maharage (Kg 1)
|
3,000/= |
3,200/= |
3,200/=-3,400/= |
Mkungu wa Ndizi
|
15,000/= |
15,000/= |
15,000/= |
Viazi mviringo (Kg 1)
|
1,000/= |
1,000/= |
1,200/= |
Viazi vitamu (Fungu)
|
2,000-3,000/= |
2,000-5,000/= |
2,000-5,000/= |
Uzalishaji wa Mazao ya Chakula 2021/2022
Mvua za Vuli na Masika msimu wa 2022/2023 zilitabiriwa kuwa za Chini ya Wastani hadi Wastani. Mvua hizo zilitabiriwa kuanza kwa kuchelewa, zenye mtawanyiko usioridhisha na kuambatana na vipindi virefu vya ukavu. Mvua hizo zlinyesha kama ilivyotabiriwa ambapo mvua za vuli zilianza kwa kuchelewa mwishoni mwa mwezi Novemba, 2022 na hazikua na mtawanyiko mzuri na kuambatana na vipindi virefu vya ukavu (jua) hivyo, kusababisha wakulima wachache kuanza kilimo katika kipindi hicho.
Hata hivyo, kuanzia wiki ya pili ya Mwezi Desemba, 2022 hadi wiki ya tatu Mwezi Januari, 2023 mvua ziliongezeka na kufanya wakulima wengi kuandaa mashamba na kupanda mazao mbalimbali. Hata hivyo, Mwezi Februari hadi mwishoni mwa Mwezi Machi, 2023 mvua ilisimama na kusababisha Mazao yaliyopandwa kunyauka na jua.
Mazao yaliyoathirika zaidi ni nafaka (hasa Mahindi) ambayo yalipandwa kipindi cha mvua za vuli na masika. Halmashauri zinazozalisha mahindi kwa wingi kama Gairo, Kilosa, Morogoro na Mvomero ndizo zimeathirika sana ukilinganisha na Halmashauri zinazozalisha zao la mpunga kwa wingi ambazo ni Mlimba, Malinyi, Ulanga na Ifakara ambapo baada ya Mvua kuanza kunyesha mwezi Aprili Mpunga umeimarika.
Aidha, Eneo lililokuwa limelengwa kulimwa mazao ya chakula ni hekta 938,448.30 ambapo hadi kufikia tarehe 31 Machi, 2023 eneo lililokuwa limelimwa ni hekta 746,668.26 sawa na asilimia 79 ya lengo na kati ya eneo lililolimwa hekta 225,151.98 sawa na asilimia 30.2 zimeathirika na athari za Ukavu wa muda mrefu.
Jedweli Na. 6: Tathimini ya eneo lililoathirika kwa Mazao ya Chakula katika Halmashauri
Halmashauri |
Eneo lengwa (Ha) |
Eneo lililolimwa |
Eneo lililoathirika (Ha) |
Asilimia ya Eneo lililoathirika |
Gairo
|
79,527.65
|
55,195.85
|
23,894.4
|
43% |
Ifakara
|
39,295.60
|
26,322
|
490.2
|
2% |
Mlimba
|
148,279.00
|
143,067.8
|
32,190.26
|
22% |
Kilosa
|
190,191.00
|
162,447
|
61,442
|
38% |
Malinyi
|
69,104.00
|
66,313
|
17,241.38
|
26% |
Morogoro (DC)
|
168,710.00
|
112,948
|
28,719.2
|
25% |
Morogoro (MC)
|
5,792.16
|
5,075.61
|
2,537.8
|
49% |
Mvomero
|
163,254.00
|
114,278
|
53,253.5
|
46.6% |
Ulanga
|
74,294.89
|
61,021
|
5,383.24
|
9% |
Jumla Mkoa
|
938,448.30
|
746,668.26
|
225,151.98
|
30.2 |
Hali ya chakula tarajiwa kwa msimu wa 2022/2023 kutokana na tathmini hiyo, Halmashauri zote za Mkoa wa Morogoro zinatarajiwa kuwa na utoshelevu wa chakula hadi ziada isipokuwa Halmashauri za Gairo, Kilosa na Mvomero zinaweza kuwa na upungufu wa chakula kwa baadhi ya Kata zinazotegemea sana zao la Mahindi kama zao kuu la chakula. Hata hivyo, maeneo mengi Wakulima walishauriwa kufyeka Mahindi yaliyoathirika zaidi na kupanda upya mazao ya muda mfupi pamoja na mazao jamii ya mizizi baada ya Mvua kuanza kunyesha mwezi Aprili.
Halmashauri zilishauriwa kuwanunulia wakulima mbegu za mazao ya muda mfupi na kupandwa kwenye maeneo yaliyoathirika zaidi na ukame. Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero ilinunua jumla ya tani 3 za Mbegu za Mahindi ya muda mfupi (DK 777) na kugawa kwa Wakulima 750 wa Vijiji vya Kata ya Kibati.
Kuendelea kutoa elimu ya uhifadhi na matumizi bora ya chakula kwa mazao yatakayovunwa ili kujihakikishia usalama wa chakula kwa Msimu ujao.
Kuhamasisha Wakulima kulima mazao yenye kustahimili ukame na yanayo komaa kwa muda mfupi kama vile Viazi Vitamu, Mihogo, Mikunde, Mtama na Mahindi ya muda mfupi.
Kuwashauri Wakulima wafugaji kupunguza mifugo kwa kuuza na kununua chakula.
Kubaini Maeneo/kaya zilizoathirika zaidi na ukame ili kushirikiana na Wizara ya kilimo kuangalia uwezekano wa Maeneo/kaya hizo kupata mahindi ya chakula kwa bei nafuu kutoka kwa Wakala wa Hifadhi ya Chakula nchini (NFRA) kwa ajili ya kupunguza makali ya bei ya vyakula katika maeneo husika. Ambapo, Mwezi Machi, 2023 Halmashauri ya Wilaya ya Gairo ilipokea jumla ya tani 65 za Mahindi ya bei nafuu.
Wizara ya Kilimo kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania (Tanzania Fertilizer Regulatory Authority –TFRA) imeandaa utaratibu wa mfumo wa kielektroniki katika kutoa ruzuku ya mbolea kwa lengo la kuongeza ufanisi wa utoaji wa ruzuku, kupunguza mianya ya udanganyifu na gharama za usimamizi. Mfumo huo unatumia programu maalum ya kidigitali kusajili wakulima, wasambazaji/wazalishaji, mawakala pamoja na kuratibu usambazaji wa mbolea kwa wakulima na malipo ya mbolea ya ruzuku.
Mkoa wa Morogoro umepokea jumla ya Vitabu 3,120 kwa ajili ya kusajili Wakulima ambapo kitabu kimoja kina uwezo wa kusajili (kuandikisha) wakulima 384 hivyo, Mkoa umepokea vitabu vyenye uwezo wa kusajili wakulima 1,198,080. Mkoa umelenga kusajili Wakulima 388,928 ambapo hadi kufikia Aprili 18, 2023, jumla ya wakulima 124,860 walikuwa wamesajiliwa sawa na asilimia 32 ya lengo ambapo kati yao Wakulima 15,752 wamenufaika na Ruzuku ya Mbolea sawa na asilimia 13 ya wakulima waliosajiliwa hata hivyo, usajili wa Wakulima bado unaendelea.
Mkoa una jumla ya Makampuni 4 (ETG, Minjingu, TFC na ITRACOM) na mawakala 24 wanaosambaza na kuuza Mbolea kwa Wakulima kwa bei ya Ruzuku isiyozidi shilingi 70,000/= kwa mfuko wa Mbolea wa kilo 50. Vilevile kuna Vyama vya Ushirika 8 vinavyojishughulisha na Kilimo cha miwa katika Bonde la Kilombero ambavyo vinasambaza mbolea. Mahitaji ya mbolea katika Mkoa wa Morogoro kwa msimu wa kilimo 2022/2023 yalikuwa jumla ya tani 27,440.
Hadi kufikia tarehe 18 Aprili, 2023, jumla ya tani 7,976.300 zenye thamani ya shilingi 18,281,872,993 zilinunuliwa kupitia mpango wa Ruzuku kati yake Shilingi 7,522,980,993 ni Mchango wa Serikali (Ruzuku) na Shilingi 10,758,892,000 ni mchango wa Wakulima. Uwepo wa Ruzuku kwenye Mbolea umesababisaha Mahitaji ya Mbolea kuongezeka kutoka tani 27,440 mwaka 2022/2023 hadi tani 36,406 kwa mwaka ujao wa 2023/2024 kama majedwali ya Mahitaji ya Mbolea yanavyoonesha hapo chini.
Jedweli Na. 7: Taarifa ya Matumizi ya Mbolea kwa Mwaka 2021/22 na Makisio ya Mahitaji ya Mbolea kwa Mwaka 2022/23
Halmashauri |
Aina ya Mbolea |
Matumizi 2021/22 (Tani) |
Makadirio ya Mahitaji 2022/23 (Tani) |
KILOSA
|
DAP
|
600 |
1,195 |
UREA
|
750 |
1,354 |
|
NPK
|
58 |
100 |
|
CAN
|
18 |
20 |
|
SA
|
4 |
5 |
|
Jumla ndogo
|
1,430 |
2,674 |
|
MALINYI
|
DAP
|
5 |
42 |
UREA
|
43 |
102 |
|
NPK
|
6 |
16 |
|
CAN
|
16 |
30 |
|
SA
|
5 |
30 |
|
Jumla ndogo
|
76 |
220 |
|
MVOMERO
|
DAP
|
1,336 |
2,162 |
UREA
|
1,829 |
3,120 |
|
SA
|
528 |
1,306 |
|
Yara Cereal
|
15 |
50 |
|
Yara mila winner
|
12 |
40 |
|
Yara Nitrabor
|
6 |
20 |
|
Yara sulfan
|
12 |
40 |
|
Yara Amidas
|
45 |
150 |
|
Yara Otesha
|
15 |
50 |
|
Samadi
|
131 |
130 |
|
Booster
|
228 |
351 |
|
Jumla ndogo
|
4,157 |
7,419 |
|
Gairo
|
DAP
|
23 |
100 |
UREA
|
43 |
100 |
|
CAN
|
17 |
50 |
|
Jumla ndogo
|
83 |
250 |
|
MOROGORO
|
DAP
|
54 |
1,000 |
UREA
|
120 |
1,000 |
|
CAN
|
96 |
200 |
|
NPK
|
- |
5 |
|
YARA CEREAL
|
55 |
30 |
|
YARA AMIDAS
|
48 |
30 |
|
Jumla ndogo
|
373 |
2,265 |
|
MLIMBA
|
DAP
|
6 |
851 |
UREA
|
14 |
1,898 |
|
CAN
|
10 |
1,265 |
|
YARA VELA AMIDAS
|
32 |
1,582 |
|
Yara Otesha
|
20 |
681 |
|
SA
|
14 |
949 |
|
Booster
|
3 |
10 |
|
YARA CEREAL
|
3 |
633 |
|
MOP
|
5 |
316 |
|
Jumla ndogo
|
108 |
8,185 |
|
MANISPAA
|
UREA
|
290 |
295 |
DAP
|
150 |
215 |
|
CAN
|
70 |
80 |
|
SA
|
45 |
45 |
|
YARAWINNER
|
|
195 |
|
YARACEREAL
|
|
30 |
|
YARAOTESHA
|
|
145 |
|
OCP
|
|
90 |
|
SULFANI
|
|
45 |
|
MOP
|
10 |
10 |
|
MAGNISIUM
|
10 |
10 |
|
CALICINITY
|
30 |
35 |
|
NITRABOR
|
30 |
35 |
|
AMIGRAN
|
20 |
25 |
|
AMIDAS
|
|
25 |
|
KYNOPLAS
|
10 |
10 |
|
Jumla ndogo
|
665 |
1,290 |
|
IFAKARA
|
DAP
|
115 |
834 |
UREA
|
492 |
1,050 |
|
SA
|
9 |
50 |
|
CAN
|
55 |
100 |
|
YARA AMIDAS
|
35 |
101 |
|
YARA CEREAL
|
50 |
99 |
|
Jumla ndogo
|
755 |
2,234 |
|
ULANGA
|
DAP
|
210 |
401 |
UREA
|
650 |
898 |
|
CAN
|
460 |
665 |
|
SA
|
600 |
649 |
|
NPK
|
290 |
290 |
|
Jumla ndogo
|
2,210 |
2,903 |
|
JUMLA KUU
|
9,857 |
27,440 |
Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2021/2022
Jedweli Na. 8: Mchanganuo wa Mahitaji ya Mbolea kwa Msimu ujao wa 2023/2024
NA. |
HALMASHAURI |
AINA YA MBOLEA (TANI) |
|||||||
DAP |
UREA |
CAN |
SA |
NPK |
MINJINGU |
ITRACOM |
JUMLA |
||
1.
|
GAIRO
|
1,611 |
2,025 |
741 |
565 |
73 |
- |
- |
5,016 |
2.
|
IFAKARA
|
699 |
6,515 |
2,764 |
- |
323 |
285 |
- |
10,586 |
3.
|
KILOSA
|
973 |
3,676 |
767 |
10 |
151 |
- |
3 |
5,579 |
4.
|
MALINYI
|
47 |
127 |
30 |
- |
- |
- |
- |
204 |
5.
|
MANISPAA
|
447 |
705 |
100 |
15 |
345 |
4 |
- |
1,616 |
6.
|
MOROGORO
|
765 |
765 |
- |
- |
20 |
- |
- |
1,550 |
7.
|
MLIMBA
|
817 |
1,597 |
286 |
78 |
155 |
193 |
- |
3,125 |
8.
|
MVOMERO
|
2,162 |
4,324 |
- |
1,081 |
- |
33 |
- |
7,600 |
9.
|
ULANGA
|
185 |
785 |
75 |
30 |
55 |
- |
- |
1,130 |
JUMLA MKOA
|
7,706 |
20,520 |
4,763 |
1,778 |
1,121 |
515 |
3 |
36,406 |
Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2022/2023
Mahitaji ya Mbegu bora za Mazao ya chakula na Biashara ni kama ilivyo kwenye Jedwali lifuatalo hapo Chini.
Jedweli Na. 9: Mahitaji ya Mbegu bora za Mazao kwa Msimu wa 2022/2023
Mbegu bora ya Zao la |
Mahitaji ya Mbegu (Tani/Miche) |
Mpunga |
5,538.88 |
Mahindi |
8,942.21 |
Ufuta |
136.99 |
Alizeti |
320.10 |
Korosho |
Miche 639,275 |
Mkonge |
Miche 52,005,600 |
Karafuu |
Miche 1,480,867 |
Kokoa |
Miche 1,625,312.5 |
Nyanya |
1.5 |
Chanzo: Takwimu kutoka Halmashauri 2021/2022
Katika msimu wa Kilimo 2022/2023, Mkoa umekabiliwa na uwepo wa visumbufu vya mazao aina ya Panya waharibifu, Viwavijeshi na viwavijeshi vamizi ambavyo vimeshambulia mazao mbalimbali. Mkoa uliomba kiasi cha lita 40,500 aina ya Powercron 720 EC (Profenofos 720g/l) kutoka Wizara ya Kilimo (Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu - TPHPA) ambapo kiasi cha lita 8,400 zilipokelewa katika Halmashauri za Gairo (lita 3,000), Kilosa (lita 1,400) na Morogoro DC (lita 4,000). Aidha, Wataalam kutoka Wizara ya Kilimo kitengo cha Udhibiti wa panya waharibifu wa Mazao baada ya kupokea taarifa ya Uwepo wa Panya katika Mkoa wa Morogoro walifika katika Halmashauri za Ulanga, Mlimba na Malinyi kwenda Kudhibiti Panya waharibifu wa Mazao.
Mkoa una eneo linalofaa kwa Kilimo cha Umwagiliaji lenye ukubwa wa hekta 1,510,339.51. Eneo linalomwagiliwa kwa sasa ni wastani wa hekta 79,429 sawa na asilimia 5. Mkoa una Skimu za Umwagiliaji 106 (asili na zilizoendelezwa) zinazotambulika zenye ukubwa wa hekta 323,758.15.
Kwa mwaka wa fedha 2022/2023, Mkoa unaendelea na utekelezaji wa miradi minne (4) ya Umwagiliaji katika Wilaya tatu (3) kama jedwali linavyoonesha hapo chini.
Jedweli Na. 10: Mchanganuo wa Miradi ya Umwagiliaji iliyopata Fedha katika Mkoa wa Morogoro
Wilaya |
Mradi |
Hatua ya Utekelezaji |
Kiasi |
Kilosa |
Ujenzi wa skimu ya Rudewa |
Mradi umefikia 25%. Mkandarasi yuko eneo la kazi na anaendelea na ujenzi. |
7,202,268,404.00 |
Mvomero |
Ujenzi wa skimu Kijiji cha Lukenge |
Mradi unaendelea na utekelezaji. Mita 1200 kati ya 2750 sawa na 43% zimesakafiwa. Changamoto kubwa ni mahitaji ya pampu ili mradi uweze kutumika. |
632,050,865.00 |
Mvomero |
Ukarabati wa skimu ya Mgongola |
Mradi umefikia 35%. Mkandarasi yuko eneo la kazi na anaendelea na ujenzi. |
5,645,751,182.00 |
Kilombero |
Ukarabati wa skimu ya Idete |
Mradi umefikia 13% badala ya 55% iliyotarajiwa. Mkandarasi bado yuko kwenye hatua za awali za utekelezaji. Kasi ya utekelezaji hairidhishi |
2,321,015,160.00 |
JUMLA |
15,801,085,611.00 |
Chanzo: Taarifa za Kilimo Mkoa 2022/2023
Aidha, tarehe 28 Machi, 2023 Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imetangaza zabuni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mingine minne (4) ambayo mchakato wa manunuzi ya Wakandarasi bado unaendelea. Miradi hii ni Itete uliopo Halmashauri ya Malinyi, Tulo/Kongwa, Kiroka na Mbalangwe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro. Gharama za miradi zitafahamika baada ya mchakato wa manunuzi kukamilika.
Mkoa wa Morogoro unajumla ya trekta 1,515, trekta ndogo (power tiller) 624 na maksai (majembe ya kukokotwa na wanyamakazi) 16,915 zinazotumika kulima wastani wa hekta 920,680.1. Kati ya hizo, hekta 578,061.80 zinalimwa kwa kutumia trekta, hekta 153,189.90 zinalimwa kwa Maksai, hekta 145,853.00 zinalimwa kwa jembe la mkono na hekta 43,575.40 zinalimwa kwa trekta ndogo. Takwimu hizi zinaashiria mwamko mkubwa kwa wananchi katika matumizi ya trekta katika uandaaji wa mashamba.
Jedweli Na. 11: Mchanganuo wa Zana kwa Halmashauri ni Kama Unavyoonekana Kwenye Jedwali
Na. |
H/Wilaya |
Matrekta |
Powertiller |
Maksao |
1.
|
Gairo |
42 |
8 |
47 |
2.
|
Ifakara TC |
227 |
104 |
816 |
3.
|
Kilosa |
274 |
143 |
1,872 |
4.
|
Malinyi |
106 |
42 |
2,696 |
5.
|
Morogoro MC |
250 |
11 |
5,000 |
6.
|
Morogoro DC |
153 |
35 |
181 |
7.
|
Mlimba
|
174 |
194 |
194 |
8.
|
Mvomero
|
239 |
87 |
278 |
9.
|
Ulanga
|
50 |
- |
5,831 |
JUMLA |
1,515 |
624 |
16,915 |
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri 2022/2023
Mkoa una Jumla ya maghala 842 yenye uwezo wa kuhifadhi Jumla ya tani 476,726.8. Kati ya maghala hayo ya Serikali ni 79 na watu binafsi ni 763.
Jedweli Na. 12: Mchanganuo wa Maghala ya Kuhifadhia Mazao katika Halmashauri
Na. |
H/Wilaya |
Idadi ya Maghala |
Uwezo wa Kuhifadhi (Tani) |
|
Gairo |
175 |
13,418 |
|
Ifakara TC |
151 |
241,355 |
|
Kilosa |
111 |
15,561 |
|
Malinyi |
59 |
14,545 |
|
Morogoro MC |
9 |
1,825 |
|
Morogoro |
26 |
3,921 |
|
Mlimba |
159 |
95,087 |
|
Mvomero |
56 |
27,080 |
|
Ulanga |
96 |
63,934.5 |
JUMLA
|
842 |
476,726.5 |
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri 2022/2023
M – Kilimo ni mfumo wa kielektroniki unaotoa huduma za ugani na masoko kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau mbalimbali kwa kutumia simu ya mkononi. Lengo la mfumo huu ni kutatua changamoto ya uhaba wa Maafisa Ugani, upatikanaji wa masoko na kuunganisha wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wengine katika mnyororo wa thamani. Kwa kutumia mfumo huu, wakulima wanapata fursa ya kuuliza maswali kuhusu changamoto wanazokabiliana nazo na kupata majibu ya hapo kwa papo kutoka kwa Wataalam husika. Ili Mkulima aweze kutumi mfumo anapiga simu na. x152x00#.
Wizara ya Kilimo iliweka lengo la kusajili wakulima 419,776 kwa Mkoa wa Morogoro, mpaka kufikia Januari, 2023, wakulima 445,331 sawa na asilimia 106 ya lengo. Wanunuzi waliosajiliwa ni 1196, wauzaji 1,676 na wataalam wa Kilimo 503.
Katika kuhakikisha lengo la Wizara ya Kilimo la kukuza kilimo kwa asilimia 10 ifikiapo 2030 linafikiwa, moja ya eneo ambalo linatiliwa mkazo ni kuhamsisha kilimo cha Mashamba Makubwa kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kushiriki katika Kilimo. Hili linatekelezwa kupitia mradi wa Jenga Kesho Bora (Building a Better Tomorrow – BBT) ambapo Mkoa utatumia fursa ya mashamba yaliyofutwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dr. Samia Suluhu Hassan ili kuwawezesha Vijana kupata Ardhi ya Kilimo.
Hadi kufikia Aprili 2023, Mkoa wa Morogoro umepokea jumla ya vijana 124 katika vituo vya mafunzo vitatu; MATI Katrin Vijana 52, Chuo cha Sukari Kilombero vijana 15, MATI Ilonga vijana 57 ambapo wanapata mafunzo ya kilimo biashara katika mnyororo wa thamani wa mazao mbalimbali ya kilimo kabla ya kukabidhiwa ardhi kwa ajili ya kilimo.
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, mama yetu Samia Suluhu Hassan mnamo tarehe 2021 aliridhia ufutaji wa mashamba kumi na moja (11) yenye ukubwa wa ekari 24,119 yaliyopo katika Wilaya ya kilosa na Mashamba 2 (ekari 11,310) katika Halmashauri ya Mvomero. Aidha, Mhe. Rais aliridhia ugawaji wa mashamba 49 yaliyopo katika vijiji 23 Wilayani Kilosa yenye ukubwa wa ekari 45,788.5 ambayo milki zake zilitwaliwa na kubatilishwa katika vipindi mbalimbali ambayo uhakiki ulibaini sehemu kubwa ya mashamba hayo yanatumiwa na wananchi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kilimo na ufugaji. Wananchi wanaogawiwa sharti wawe wamejiunga kwenye vikundi ili kuondoa tabia ya wananchi kuuza maeneo.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha mazao ya viungo kwa wingi kama vile karafuu, iliki, mdalasini, vanilla na pilipilimanga. Katika kuendeleza mazao ya viungo, Mkoa kwa kushirikiana na Halmashauri ya Morogoro wamefanya tathmini ya hali ilivyo kwa kukusanya takwimu za majina ya wakulima wa karafuu, ukubwa wa maeneo yanayolimwa, hali ya uzalishaji, bei, mahitaji ya miche na kubaini maeneo ya wazi kwa ajili ya kilimo cha mazao ya viungo. Jumla ya ekari 84,024 zimebainika kuwa zinafaa kwa kilimo cha mazao ya viungo. Takwimu zinaonyesha kuwa jumla ya ekari 17,219 zimepandwa karafuu, eneo linaloweza kulimwa Karafuu ni ekari 5,931, mdalasini ni ekari 2,263, iliki ni ekari 589 na pilipilimanga ni ekari 1,299. Mahitaji ya miche ya Karafuu ni 1,459,785. Mpaka mwishoni mwa Aprili 2023, Mkoa kwa kushirikiana na Kampuni Viridium na WWF imetoa miche ya karafuu 27,000 katika Halmashauri ya Morogoro na kusambazwa kwa wakulima bure katika msimu wa 2022/2023.
Mkoa wa Morogoro ni moja kati ya Mikoa inayolima korosho nchini na umeendelea na utekelezaji wa Mpango wa maendeleo ya zao la Korosho katika Halmashauri nane kati ya tisa zilizopo na jumla ya wakulima 1,653 wamesajiliwa na Bodi ya korosho Tanzania kwa ajili ya kupewa vitambulisho vya wakulima wa zao la Korosho. Halmashauri za Wilaya zinazolima zao la Korosho ni Gairo, Kilosa, Malinyi, Morogoro, Mlimba, Mvomero Ulanga pamoja na Halmashauri ya Mji wa Ifakara. Mkoa una jumla ekari 36,840 zenye jumla ya Mikorosho 1,550,504. Kati ya hiyo, mikorosho 408,159 imeanza kuzaa.
Katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 Mkoa ulizalisha jumla ya tani 325.07 za Korosho na kuuzwa kwa mfumo wa stakabadhi ghalani.
Mkoa umejipanga kuongeza uzalishaji wa zao la Korosho kutoka tani 231 hadi kufikia tani 858.5 ifikapo mwaka 2025/2026 kama inavyoonekana katika jedwali.
Jedweli Na. 13: Mpango wa Uzalishaji zao la Korosho kwa miaka mitano ijayo 2021/2022 hadi 2025/2026
S/N
|
HALMASHAURI
|
MAKADIRIO YA UZALISHAJI (T) |
|||||
2021/2022 |
2022/2023 |
2023/2024 |
2024/2025 |
2025/2026 |
|||
1
|
Gairo
|
5 |
7 |
9 |
13 |
34 |
|
2
|
Ifakara
|
2.3 |
8.6 |
10.7 |
24.0 |
53.5 |
|
3
|
Kilosa
|
30 |
45 |
60 |
90 |
120 |
|
4
|
Malinyi
|
91 |
108 |
125 |
135 |
150 |
|
5
|
Mlimba
|
22.5 |
25.8 |
55 |
75 |
100 |
|
6
|
Morogoro
|
41 |
62 |
91 |
137 |
158 |
|
7
|
Mvomero
|
|
17 |
25 |
42 |
103 |
|
8
|
Ulanga
|
40 |
60 |
85 |
110 |
140 |
|
Jumla
|
231.8 |
333.4 |
460.7 |
626 |
858.5 |
Katika Mkoa wa Morogoro Wilaya zinazozalisha zao la Pamba ni Kilosa, Gairo, Malinyi, Morogoro, Mvomero na Ulanga. Katika msimu wa 2021/2022 jumla ya hekta 2,565 zililimwa na kuzalisha jumla ya tani 1943.49. Pamba yote ilinunuliwa na Bodi ya pamba kwa wastani wa bei ya shilingi 1560 kwa kila Kilo ya Pamba. Katika Msimu wa 2022/2023 Mkoa umelenga kulima hekta 4,357 ili kuvuna tani 3481.20.
Mkoa wa Morogoro ni Miongoni mwa Mikoa inayozalisha kwa wingi zao la Mkongo nchini. Halmashauri zinazozalisha Mkonge katika Mkoa wa Morogoro ni Kilosa, Morogoro, Mvomero na Gairo. Hata hivyo, Halmashauri za Gairo na Mvomero hazijaanza kuvuna Mkonge zipo kwenye hatua ya kuhamasisha Wakulima na upandaji wa Mkonge. Maeneo yanayolimwa Mkonge ni wastani wa Hekta 10,573.55 na kuvuna wastani wa tani 12,216.91 kwa mwaka.
Jedweli Na. 14: Wazalishaji wakubwa na wakati wa zao la Mkonge katika Mkoa wa Morogoro ni kama ifuatavyo
Na. |
Jina la Shamba |
Mahali lilipo |
Ukubwa wa shamba (Hekta) |
Eneo lenye Mkonge |
Wastani wa Mavuno kwa mwaka |
|
Pangawe Highland Estate
|
Mkambarani Pangawe – Morogoro vijijini
|
3,698 |
1,472.65 |
2,061.71 |
|
FATEMI (Mohamed Enterprises Tanzania Limited) |
Kidugalo – Morogoro Vijijini
|
6,412 |
3,637 |
5,819.2 |
|
M/S New kimamba Fbres Co. Ltd
|
Kimamba – kilosa
|
2,947 |
2,323.5 |
1,409 |
|
China State Farms Ltd
|
Rudewa – Kilosa
|
5,300 |
2,480 |
2,573 |
|
New Msowero Farm
|
Msowero – Kilosa
|
1,360 |
440 |
354 |
|
Igembe Nsabo - AMCOS
|
Rudewa – Kilosa
|
21.4 |
8.8 |
0 |
|
Josephat Rwezaura
|
Mkonowamara – Morogoro Vijijini
|
40 |
20 |
0 |
|
Mohamed Ramadhani
|
Mkonowamara – Morogoro Vijijini
|
80 |
80 |
0 |
|
Clement Munish ambae
|
Mkonowamara – Morogoro Vijijini
|
32 |
32 |
0 |
|
Wami Sokoine
|
Mvomero
|
40 |
40 |
|
|
Kimambila
|
Mvomero
|
11.2 |
11.2 |
|
|
Vianzi
|
Mvomero
|
20 |
20 |
|
|
Gairo
|
Gairo
|
8.4 |
8.4 |
|
JUMLA |
19,970.00 |
10,573.55 |
12,216.91 |
Katika Wilaya ya Kilosa Ipo pia AMCOS ya Lukwambe ambayo imepatiwa na Serikali eneo la kulima Mkonge upandaji unaendelea. Aidha wananchi wanaendelea kugawiwa maeneo ili wajiunge kwenye AMCOS kwa ajili ya kilimo cha Mkonge.
Zao la Kahawa lilikuwa linalimwa Katika Wilaya za Mvomero, Morogoro Gairo na Ulanga. Aina ya kahawa inayolimwa katika Mkoa wetu ni Robusta na Arabica. Ili kuhakikisha kuwa zao la Kahawa linafufuliwa Mkoa unashirikiana na Watafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa kahawa Tanzania – TACRI na kutoa elimu ya kuzalisha zao la Kahawa kwa wataalam. TACRI kwa kushirikiana na Halmashauri za Ulanga, Gairo, Mvomero, Morogoro inatoa mbegu na miche kwa wakulima ili kuendeleza zao hilo. Jumla ya kata 28 na wakulima 2,104 wametambuliwa kuwa wakulima wa kahawa Kimkoa.
Mkoa unashirikiana na wadau mbalimbali kutekeleza programu ya sekata ya kilimo katika Mkoa. Baadhi ya wadau hao ni SAGCOT, USAID, CAU, SAT, MVIWATA, MINJINGU nk.
Katika kuhakikisha sekta ya kilimo inakuwa na tija pamoja na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, Serikali imeweka mikakati mbalimbali ya kuimarisha na kuboresha huduma za ugani nchini kwa kugawa vitendea kazi zikiwemo pikipiki, vifaa vya kupima afya ya udongo, vishikwambi na visanduku vya ugani kwa Maafisa Ugani kilimo nchini.
Mpango huu ulizinduliwa na Mheshimiwa Dr. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 4 Aprili, 2022. Mnamo mwezi Februari, 2023 Mkoa wa Morogoro ulipokea jumla ya pikipiki 436 kwa ajili ya Maafisa Ugani Kilimo kama ilivyo kwenye mchanganuo ufuatao (Jedwali Na. 23).
Jedweli Na. 15: Mchanganuo wa Maafisa Ugani Kilimo na Mgawanyo wa Pikipiki
Na. |
H/Wilaya |
Maafisa Waliopo |
Wenye Pikipiki kutoka Taasisi za Kilimo/Halmashauri |
Pikipiki zilizoletwa na mh Rais |
|
RS Morogoro
|
4 |
1 |
3 |
1.
|
Gairo
|
29 |
3 |
26 |
2.
|
Mji Ifakara
|
49 |
2 |
52 |
3.
|
Kilosa
|
89 |
4 |
87 |
4.
|
Mlimba
|
34 |
3 |
34 |
5.
|
Malinyi
|
23 |
3 |
20 |
6.
|
Morogoro MC
|
33 |
6 |
20 |
7.
|
Morogoro DC
|
73 |
3 |
68 |
8.
|
Mvomero
|
102 |
3 |
99 |
9.
|
Ulanga
|
26 |
1 |
27 |
Jumla
|
462 |
29 |
436 |
Pikipiki zote 436 zimefungwa GPS ili kufuatilia utendaji kazi wa Maafisa ugani katika maeneo yao ya kazi ambapo Afisa ugani anapaswa kuitumia Pikipiki hiyo katika kituo chake cha Kazi na endapo atataka kutoka nayo nje ya Kituo chake cha kazi anapaswa kuomba ruhusa kwa Mkuu wake wa Idara.
Wito kwa Maafisa Ugani wote wa Mkoa wa Morogoro ni kuhakikisha wanazitumia Pikipiki hizo kwa shughuli za Ugani pekee ili kuhakikisha kuwa kilimo katika Mkoa wetu kinaboreshwa zaidi na kuchangia katika uchumi wa Mtu mmoja na Taifa kwa ujumla.
Upungufu na Ubovu wa Miundombinu ya Umwagiliaji iliyopo, inachangia wakulima wengi kutegemea kilimo cha Mvua ambayo huwa haitabiriki na kusababisha wakulima wengi kushindwa kufikia malengo.
Upungufu wa Watumishi katika Idara za Kilimo, unaokwamisha utendaji kazi kwani baadhi ya maeneo muhimu hasa katika maeneo ya Kata na Vijiji hakuna Wataalam.
Uhaba wa Fedha za Ufuatiliaji, Fedha za usimamizi wa shughuli za Kilimo zinatolewa kidogo sana ukilinganisha na Mahitaji hasa katika ngazi ya Halmashauri.
Baadhi ya Halmashauri kutotoa asilimia 20 ya fedha za Mapato ya Ndani yanayotokana na Kilimo kw ajili ya uendelezaji wa Sekta ya Kilimo (miundombinu ya Umwagiliaji, Mbegu bora, Maghala na WARC) kitendo hicho kinachangia Sekta ya Kilimo kuonekana siyo kipaumbele wakati ndio inategemewa katika ukusanyaji wa Mapato ya Halmashauri hizo.
Kutokuwa na Mafunzo Rejea (On Job Training) kwa Wataalam wa Kilimo hivyo, kusababisha baadhi ya Wataalam kutoendana na teknolojia za kisasa hivyo, kulalamikiwa na Wananchi.
Mikopo kwa Wakulima, taasisi za mkopo (Mabenki) kuwa na masharti yasiyorafiki kwa Wakulima hivyo, kusababisha Wakulima kuendelea kunyonywa na Madalali ambao Wakati wa Kulima na Palizi kipindi ambacho wakulima hawana hela wanakopeshwa fedha na madalali kwa kigezo kuwa Mkulima akivuna mazao atamlipa Mazao badala ya fedha hasa kwa zao la mpunga.
Kutokuwa na bei ya kueleweka ya mazao ya Nafaka (Kupanda na kushuka kwa bei bila mpangilio) Price fluctuation. Kunasababisha wakulima kushindwa kupanga bei ya mazao ili wapate faida.
Maeneo ya kuhifadhia mazao (Maghala) ni machache hivyo, kusababisha wakulima kuuza bila mpangilio.
Uingizaji wa Mbegu za mazao za Nafaka kutoka nje ya nchi kunachangia kupotea kwa mbegu nzuri za asili.
Baadhi ya mawakala waliosajiliwa kupitia mfumo wa Mbolea ya Ruzuku kupitia TFRA kutokuwa na uwezo wa kimtaji wa kuuza mbolea kusababisha wakulima wengi kufuata mbolea kwa umbali mrefu maeneo ya Mjini na kuona kuwa ni kero.
Kuimarisha AMCOS kwa ili wakulima waweze kuhifadhi mazao kwa pamoja na kutafuta masoko ili kuuza mazao kwa bei nzuri.
Kuimarisha Miundombinu ya Kuhifadhia mazao (Maghala) ambapo Halmashauri zimeshauriwa kutumia mapato ya ndani (asilimia 20 ya mapato yanayotokana na kilimo) kujenga maghala angalau kila Kata kuwe na ghala na vifaa vyote muhimu vinavyo hitajika ikiwemo kipima unyevu (Moisture meter) ili wakulima waweze kuhifadhi mazao na kuuza kwa pamoja.
Kutumia fursa ya Mhe. Rais kutoendeshwa na Wahisani (Donors) kwa kupigania Sera zetu badala ya kufuata wanachotaka wao.
Kutozuia mazao ya Chakula kuuzwa nje ya Mkoa na nje ya nchi ili wakulima kuuza kwa faida.
Kuwe na vituo maalum vya kuuzia Nafaka kwa kila Kijiji/Kata ili kudhibiti Madalali na ubora wa mazao ya Nafaka.
Kutoa elimu kwa wakulima ili wauze mazao yao kwa njia ya Minada ya Soko la bidhaa (TMX) badala ya kuuza mmoja mmoja.
Kuainisha Vituo vya Kuuzia Mbolea kulingana na Mahitaji ili Msimu wa Kilimo wa 2023/2024 Wakulima wapelekewe Mbolea katika Maeneo yao.
Pamoja na changamoto hizo, tunamshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa Vitendea kazi (Pikipiki) kwa Maafisa Ugani Kilimo na Ruzuku ya Mbolea kwa Wakulima, kwani mwamko umekuwa mkubwa sana Wakulima wengi wamelima mazao mbalimbali kutokana na kupunguziwa bei ya Mbolea pia Wataalam wanawafikia Wakulima kwa urahisi kutatua changamoto zao.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.