Sekta ya Uvuvi
Utangulizi.
Katika Mkoa wa Morogoro sehemu kubwa ya uvuvi hufanyika kutokea kwenye kambi za wavuvi kandokando ya mto Kilombero. Kuna aina zaidi ya 52 ambapo zaidi ya 90% ya samaki wote wanapatikana kutokea mto Kilombero. Baadhi ya aina hizo ni Kitoga, Kambale, Perege, Njege, Ndungu, Bura, Ningu, Mgundu, Mbala, Mjongwa, Ngulufi, Mbewe, Ngogo, Sulusulu na Mkunga. Uvuvi mwingine kwa kiwango kidogo hufanyika katika mabwawa ya asili, ya kuchimbwa na mito imwagayo maji yake katika bonde la mto Rufiji.
Mkoa umeendelea kutoa elimu na kuhamasisha wananchi kufuga samaki katika mabwawa ya kuchimbwa ili kuongeza upatikanaji wa samaki Mkoani na pia kupunguza utegemezi katika vyanzo vya asili. Kutokana na uhamasishaji huo Mkoa kwa sasa una jumla ya mabwawa ya kuchimbwa 857 yanayokadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 30 kwa mwaka. Mchanganuo wa mabwawa ya samaki kwa kila Halmashauri ni kama inavyoonyesha katika jedwali Na. 1 hapo chini.
Jedweli Na. 20: Mabwawa ya Samaki katika Halmashauri
Na. |
HALMASHAURI |
IDADI |
1.
|
Ifakara
|
37 |
2.
|
Mlimba
|
25 |
3.
|
Kilosa
|
230 |
4.
|
Malinyi
|
15 |
5.
|
Morogoro MC
|
175 |
6.
|
Morogoro DC
|
146 |
7.
|
Mvomero
|
104 |
8.
|
Ulanga
|
90 |
9.
|
Gairo
|
35 |
JUMLA |
857 |
Chanzo: Taarifa kutoka Halmashauri
Katika kuongeza uzalishaji wa samaki Mkoani, elimu ya ufugaji wa samaki imekuwa ikitolewa kwa wananchi na udhibiti wa uvuvi haramu kwenye vyanzo vya asili umekuwa ukifanyika kwa kutumia doria, elimu na vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya uvuvi (BMUs). Hivyo kutokana na vyanzo vilivyopo Mkoani, msimu wa mwaka 2021/2022 uzalishaji ulikuwa tani 192.3 zenye thamani ya shilingi 972,555,110 ikilinganishwa na mwaka 2020/2021 ambapo uzalishaji ulikuwa tani 279.5 zenye thamani ya shilingi.1,307,018,617.75.
Uzalishaji umepungua kwa kiasi kikubwa kwa sababu sehemu kubwa ya bonde la Mto Kilombero lilikuwa pori tengefu na sasa limekuwa pori la akiba na hivyo kusababisha wavuvi wengi kushindwa kuingia kuvua samaki kutokana na masharti yaliyowekwa hususani viwango vya tozo ambavyo wengi wao wanashindwa kuvimudu. Mchanganuo wa uzalishaji kwa kila Halmashauri kwa kipindi cha miaka 2 ni kama inavyoonyesha katika jedwali Na. 2 hapo chini.
Jedweli Na. 21: Mavuno ya Samaki kwa Msimu wa Mwaka 2020/2021 ikilinganishwa na Mwaka 2021/2022 katika Halmashauri
Na. |
HALMASHAURI |
2020/2021 |
2021/2022 |
||
UZITO (tani) |
THAMANI (Tsh) |
UZITO (tani) |
THAMANI (Tsh) |
||
1. |
Mlimba |
89.2 |
369,178,217.75 |
32.6 |
125,333,110 |
2. |
Kilosa |
47.6 |
237,930,000.00 |
51 |
305,340,000 |
3. |
Morogoro MC |
12.1 |
72,357,500.00 |
11 |
20,389,500 |
4. |
Ulanga |
32.9 |
132,228,250.00 |
22 |
111,881,150 |
5. |
Mvomero |
4.4 |
21,930,000.00 |
3.8 |
23,279,000 |
6. |
Morogoro DC |
2.1 |
11,312,000.00 |
1.3 |
7,608,000 |
7. |
Ifakara Mji |
41.4 |
239,144,200.00 |
43.8 |
251,912,500 |
8. |
Malinyi |
49.8 |
222,938,450.00 |
26.8 |
126,811,850 |
9. |
Gairo |
0 |
0 |
0 |
0 |
|
JUMLA |
279.5 |
1,307,018,617.75 |
192.3 |
972,555,110 |
Kuna changamoto nyingi ambazo zinajitokeza katika sekta ya uvuvi. Miongoni mwa changamoto hizo ni kama ifuatavyo:
Upungufu au ukosefu wa wataalamu wa Uvuvi katika mamlaka za Serikali za Mitaa unapunguza ufanisi katika kutekeleza majukumu. Mahitaji ya wataalamu wa uvuvi katika Makao Makuu ya Halmashauri ni 18, waliopo ni 12, hivyo upungufu ni 6. Aidha mahitaji katika ngazi ya kata ni 214, waliopo 3 na hivyo pungufu ni 211.
Ukosefu wa vitendea kazi hususani magari na boti za doria kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa unakwamisha ufanisi katika kutekeleza majukumu.
Matumizi ya zana au njia haramu za uvuvi yaani makokoro, nyavu zenye macho madogo na matumizi ya sumu vinatishia ustawi wa samaki
Uhaba wa maji ya kutosha hususani wakati wa kiangazi husababisha mabwawa mengi ya kufugia samaki kuwa ya msimu.
Halmashauri kutorejesha 5% ya mapato yatokanayo na shughuli za uvuvi kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za uvuvi.
Halmashauri ziendelee kuomba kibali cha kuajiri Maafisa Uvuvi angalau kila Kata iwe na Afisa Uvuvi ili elimu ya kutosha kuhusu rasilimali hii ya samaki isambazwe kwenye maeneo yote Mkoani.
Wakurugenzi wasisitizwe kutenga bajeti za ununuzi wa boti za doria katika mipango yao.
Kuendelea kutoa elimu za mara kwa mara kwa wavuvi na wafugaji wa samaki ili watambue umuhimu wa kuwepo kwa rasilimali ya samaki kwa kizazi cha sasa na kijacho.
Kuendelea kuhamasisha jamii kuchimba mabwawa ya kufugia samaki na hatimaye kupunguza utegemezi katika vyanzo vya asili.
Kuendelea kusisitiza Halmashauri kuendesha doria mara kwa mara hasa katika maeneo yenye uharibifu mkubwa wa mazingira ili kuhakikisha sheria na kanuni zinafuatwa.
Kuendelea kutoa elimu kwa wakulima kupandikiza vifaranga bora na pia kutumia chakula bora cha samaki ili wazalishe kwa tija.
Kuimarisha vikundi vya ulinzi wa rasilimali ya uvuvi (BMUs) katika maeneo yote ya uvuvi.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.