WATUMISHI WA MKOA
Utekelezaji wa majukumu ya Sekretariati unaongozwa kwa mujibu wa sheria ya Tawala za Mikoa Na. 19 ya mwaka 1997 ambayo inatambua uwepo wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuainisha majukumu ya Ofisi hiyo. Ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yaliyoainishwa na sheria hiyo, Serikali iliunda muundo wa kiutawala wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa kuzingatia sekta mbalimbali. Muundo huo unajumuisha Sehemu (Sections) nane na vitengo (units) vitano
Kwa mujibu wa Sheria hiyo shughuli au majukumu ya Mkoa yanatekelezwa na kuongozwa na Mkuu wa Mkoa kwa kushirikiana na Katibu Tawala wa Mkoa ambaye ni Mtendaji Mkuu na Afisa Masuuli (Accounting Officer). Chini ya Viongozi hao wawili (2) kuna Wakuu wa Sehemu nane (8) na Vitengo vitano (5) na kwa pamoja husimamia utekelezaji wa majukumu/ utendaji mzima unaoelekezwa au unaotakiwa kufanywa kwa kila siku. Sehemu na Vitengo vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ni kama ifutavyo;
Sehemu
Sehemu ya Utawala na Rasilimali watu
Sehemu ya Mipango na Uratibu
Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Mali
Sehemu ya Miundo Mbinu
Sehemu ya Menejimenti ya Serikali za Mitaa
Sehemu ya Maji
Sehemu ya Afya
Sehemu ya Elimu
Vitengo
Uhasibu
Sheria
Ugavi
Ukaguzi wa Ndani
Tehama
Nafasi za wakuu wa sehemu na baadhi ya vitengo katika Sekretarieti ya Mkoa zimekwisha jazwa. Vitengo ambavyo wakuu wake wanakaimu ni kitengo cha sheria, Tehama na Kitengo cha manunuzi, pia yapo mapungufu na nafasi wazi ya baadhi ya wataalam. Jumla ya watumishi wanaotakiwa ni 1,111 kati ya hao waliopo ni 818 na pungufu ni 276 ambayo ni upungufu wa asilimia 14.8. Mpaka tarehe 31 Januari, 2017, idadi ya Watumishi wote katika Sekretarieti ya Mkoa na Serikali za Mitaa ni 24,467 Mchanganuo wa watumishi waliopo na Ikama ya Watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ni kama ifuatavyo;-.
Ikama ya Watumishi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro hadi Machi, 2016
NA.
|
SEHEMU/KITENGO
|
IKAMA
|
WALIOPO
|
UPUNGUFU
|
1
|
Utawala na Utumishi
|
71
|
52
|
19
|
2
|
Mipango na Uratibu
|
8
|
8
|
0
|
3
|
Miundombinu
|
9
|
8
|
2
|
4
|
Serikali za Mitaa
|
10
|
7
|
3
|
5
|
Huduma za Maji
|
5
|
3
|
2
|
6
|
Huduma za Elimu
|
7
|
5
|
2
|
7
|
Uchumi na Uzalishaji
|
19
|
17
|
2
|
8
|
Huduma za Afya na Ustawi wa Jamii.
|
8
|
8
|
0
|
9
|
Uhasibu na Fedha
|
12
|
11
|
1
|
10
|
Sheria
|
2
|
2
|
0
|
11
|
Ukaguzi wa Ndani
|
3
|
3
|
0
|
12
|
Manunuzi na Ugavi
|
3
|
3
|
0
|
13
|
TEHAMA
|
6
|
3
|
2
|
14
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Morogoro
|
48
|
19
|
29
|
15
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilosa
|
53
|
26
|
27
|
16
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kilombero
|
43
|
24
|
19
|
17
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mvomero
|
38
|
13
|
25
|
18
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Ulanga
|
40
|
9
|
31
|
19
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gairo
|
28
|
7
|
21
|
20
|
Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Malinyi
|
18
|
6
|
12
|
21
|
Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
|
680
|
584
|
79
|
|
Jumla
|
1,111
|
818
|
276
|
Jedwali Na.3 Idadi ya Watumishi katika Mkoa
Mkoa/Halmashauri
|
Mahitaji
|
Waliopo
|
Upungufu
|
Mkoa
|
1,111
|
818
|
276
|
H/Manispaa Morogoro
|
4018
|
4137
|
+73
|
Morogoro DC
|
3299
|
2870
|
429
|
Mvomero
|
4180
|
3239
|
941
|
Kilosa
|
3039
|
2861
|
178
|
Kilombero
|
1545
|
968
|
577
|
Ulanga
|
2695
|
1754
|
941
|
Gairo
|
1858
|
1427
|
451
|
Malinyi
|
1626
|
887
|
680
|
Ifakara TC
|
1096
|
998
|
99
|
JUMLA
|
24,467
|
19,965
|
4583
|
Chanzo: Taarifa za Mkoa na Wilaya ,2017
HALI YA UTUMISHI NA UTAWALA KATIKA SEKRETARIETI YA MKOA
Watumishi katika Sekretariati ya Mkoa inawajumuisha Watumishi waliopo Makao Makuu ya Mkoa, Ofisi za Wakuu wa Wilaya 7 na Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. Kwa mujibu wa Ikama ya Mkoa wetu wanahitajika Watumishi 1,111 hadi taarifa hii inapowasilishwa kuna Jumla ya Watumishi/Viongozi wa kuteuliwa katika kada/ngazi mbalimbali 789 hivyo kuwa na upungufu wa watumishi 322
Majukumu yaliyotekelezwa
Idara inaendelea kutekeleza jukumu muhimu la usimamizi na uendelezaji wa Rasilimali watu ambalo limesaidia kuimarisha utendaji kazi wa watumishi, ustawi na hali zao mahali pa kazi ambao umefanikisha kwa kipindi chote huduma bora kwa wananchi.
Ili kutekeleza adhma ya Serikali ya kuhakikisha watumishi wa umma wapo kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu na kudhibiti ajira zisizostahili, Watumishi 31 wameondolewa katika utumishi wa Umma kutokana na kubainika kughushi vyeti na 2 kwa sababu za kimuundo yaani kutokuwa na vyeti vya kidato cha nne wakati masharti ya ajira zao zinahitaji wawe na sifa hiyo. Aidha, watumishi 2 walibainika kuwa ni hewa wakati wa zoezi la kuhakiki watumishi.
Tunashukuru Serikali kwa utekelezaji wa masuala mbalimbali ambayo yatasaidia kuboresha hali ya utumishi na motisha kwa watumishi wake yakiwemo yafuatayao;
Kuanza kutoa vibali vya ajira mpya ambavyo hadi sasa wamepatikana watumishi 5 (4 wa Afya na 1 Utawala) kati ya 22 walioombwa katika kibali cha mwaka 2015/2016. Vipaombele vya watumishi ni katika eneo la Afya na maeneo mapya ya Utawala yaani Wilaya ya Malinyi na Gairo.
Kulipa madeni mbalimbali ya watumishi katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Kulipa madeni ya gharama za samani kwa viongozi ya kiasi cha shilingi 112,000,000
Kutoa nafasi ya kuwapandisha vyeo watumishi 82 wanaostahili
Utekelezaji wa jukumu hili katika Mkoa umejikita kwenye usimamizi wa milki na vifaa vinavyotumika na watumishi na viongozi katika ngazi ya Mkoa na Wilaya. Serikali imetekeleza wajibu wake kwa kiasi kikubwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa muhimu vinavyotumika na watumishi/viongozi ili kutekeleza majukumu yao. Pamoja na hatua hizo zilizochukuliwa na Serikali bado kuna changamoto ya uchakavu wa vifaa na miundombinu ya muda mrefu pamoja kuanzishwa kwa maeneo mapya ya Utawala ya Wilaya ya Malinyi na Gairo.
Maeneo ya kipekee yanayohitaji kushughulikiwa kwa haraka ni yafuatayo;
|
Eneo
|
Hali kwa sasa
|
Njia mbadala
|
1
|
Ununuzi wa Gari la Mkuu wa Mkoa
|
Liliharibika baada ya kupata ajali
|
Kuazima la Mkuu wa Wilaya Mvomero
|
2
|
Ununuzi wa Gari la Katibu Tawala wa Mkoa
|
Liliharibika
|
Kutumia la Idara
|
3
|
Ununuzi wa Gari la Mkuu wa Wilaya Malinyi
|
Halikuwahi kununuliwa
|
Kuazimwa la Idara japo ni bovu
|
|
Ujenzi wa nyumba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Malinyi
|
Wilaya mpya
|
Kuazimwa vyumba 3 katika Hospitali ya Lugala
|
4
|
Ujenzi wa nyumba na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Gairo
|
Wilaya iliyoanzishwa mwaka 2012
|
Kutumia sehemu ya Jengo la Mamlaka ya Mji Mdogo Gairo na Resti house ya Halmashauri
|
5
|
Ununuzi wa Gari la Mkuu wa Wilaya Kilosa
|
Lililopo ni chakavu hivyo kuwa na gharama kubwa za matengenezo
|
Kulikarabati mara kwa mara.
|
Pamoja hali iliyoelezwa hapo juu utekelezaji wa majukumu kwa viongozi hao na wengine wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na Wakuu wa Wilaya zimeendelea kutekelezwa ipasavyo.
Mkoa wa Morogoro kwa ushirikiano na Halmashauri za Wilaya , wananchi, Wadau, Wahisani na Asasi mbalimbali wote kwa pamoja wanatekeleza majukumu yao kikamilifu katika kujiletea Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii. Mafanikio yaliyopatikana katika Serikali ni matokeo ya Uongozi wa pamoja, uwajibikaji na uwazi katika kuleta maendeleo stahimili.
Tutaendeleza juhudi mbalimbali za kuvutia wawekezaji katika maeneo mbalimbali katika Mkoa wa Morogoro ili kufanikisha mapinduzi ya uchumi wa viwanda. Mafanikio ya juhudi hizo yatakuwa chachu ya ongezeko la ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Azma ya Mkoa ni kuhakikisha kuwa mazingira bora ya utoaji huduma kwa wananchi yanaendelea kuboreshwa. Mkoa unahitaji ujitosheleze kwa chakula kwa malengo aliyopewa kwa malengo aliyopewa na kuboresha hali ya mazingira yake. Kuongezeka kwa vitendo vya uharibifu wa mazingira kutachochea zaidi kuongezeka kwa umaskini miongoni mwa wanamorogoro. Kwa ujumla azma ya kuleta maendeleo endelevu kwa wananchi ikifikiwa basi lengo la kufikia uchumi wa kati na kumpatia maisha bora mwananchi wa Mkoa wa Morogoro ifikapo 2025 itafanikiwa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.