TAARIFA YA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
(GOVERNMENT COMMUNICATION UNITY- GCU)
RS- MOROGORO
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini (GCU) katika Sekretarieti za Mikoa ni kitengo kipya kimuundo ambacho kimeanza rasmi baada ya marekebisho ya muundo mpya wa Sekretarieti hizo na kuidhinishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan January 29, 2022 na kuanza kutumika rasmi Julai, 2022.
Awali Afisa Habari katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa au katika Sekretarieti za Mikoa alikuwa akitekeleza majukumu yake akiwa chini ya Idara ya Utawala na Utumishi (AAS - SS).
Kitengo hiki kinatekeleza Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977 Sura ya Kwanza Sehemu ya tatu ibara ya 18 (d) inayosema:
“Kila mtu anayo haki ya kupewa taarifa wakati wote kuhusu matukio mbalimbali muhim kwa maisha na shughuli za wananchi na pia kuhusu masuala muhim kwa jamii”.
MUUNDO:
Kimuundo, katika Sekretarieti ya Mkoa, kitengo hiki kinahitaji kuwa na watumishi watatu (3) wa taaluma ya Habari na kinatakiwa kuongozwa na Afisa mwenye cheo cha Afisa Habari Mkuu.
Lengo la Kitengo:
Jukumu la kitengo hiki ni kushauri kitaalamu Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa (Menejimenti) kuhusu masuala yote yanayohusu Habari na Mawasiliano.
Majukumu ya kitengo:
Kuandaa nyaraka mbalimbali kama vile vipeperushi, majarida na Makala na kuutarifu umma juu ya shughuli zinazotekelezwa na Serikali ndani ya Mkoa wa Morogoro.
Kuratibu maandalizi ya Mikutano ya Mkuu wa Mkoa na waandishi wa Habari (Press Conference) itakayokuwa inafanywa na Mkuu wa Mkoa.
Kuhuisha taarifa mbalimbali katika tovuti za Sekretarieti za Mikoa husika kama Morogoro ni www.morogoro.go.tz.
Kushiriki midahalo inayoandaliwa kwa ajili ya mambo mbalimbali yanayofanyika Mkoani.
Kutoa taarifa mbalimbali juu ya maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kijamii zilizopo ndani ya Mkoa.
Kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo katika kutoa taarifa juu ya maendeleo ya shughuli za kiuchumi na kijamii zilizopo ndani ya Mkoa.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.