Kitengo cha Sheria kina kazi ya Kutoa utaalamu wa kisheria na huduma kwa Katika Sekretariati ya Mkoa.
shughuli za Kitengo ni: -
Sheria za mifugo;
Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Na. 17 ya mwaka 2003 kifungu cha 43. Sheria hii inawataka wafugaji wote kupata kibali cha kuhamisha mifugo kutoka eneo moja hadi lingine kama ilivyoelekezwa katika sheria.
Sheria ya Nyanda za Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo Na.13 ya mwaka 2010 kifungu cha 20. Sheria hii inawataka Wafugaji kufuga idadi ya mifugo kulingana na uwezo wa eneo la malisho.
Sheria ya Usajili, Utambuzi na Ufuatiliaji wa Mifugo Na. 12 ya mwaka 2010 kifungu cha 12 na 24. Sheria hii inawataka wafugaji kusajili mifugo yao kwa mujibu wa sheria husika.
Kwa kutumia sheria tajwa hapo juu hadi kufikia Januari 30, 2018 Jumla ya ng’ombe 703,753 wamepigwa chapa ya moto kati ya ng’ombe 841,044 waliolengwa sawa na asilimia 84.
Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.