Wilaya ya Gairo.
Wilaya ya Gairo ilianzishwa kwa Tangazo la Serikali Na 75 la tarehe 02/03/2012 kufuatia kugawanywa kwa Wilaya ya Kilosa na baadae utekelezaji wa shughuli za Halmashauri ulianza rasmi Julai mwaka 2013. Eneo la Wilaya ya Gairo ni Kilometa za mraba 1,851.34.
Gairo inakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 193,011 wanaume ni 93,206 na wanawake ni 99,805, hii ni kwa mujibu wa Sensa ya watu na Makazi ya mwaka 2012. Wastani wa watu kwa kaya ni 5:2 sawa na ongezeko la asilimia 2.6 kwa mwaka.
Wilaya inaundwa na Tarafa mbili, Kata 18, vijiji 50 na vitongoji 304 Aidha, kuna jimbo moja la uchaguzi la Gairo. Kwa maelezo zaidi bonyeza http://www.gairodc.go.tz/
Haki Miliki © 2018 Mkoa wa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa