Afisa Mtendaji wa Mji mdogo wa Mikumi Wilayani Kilosa Mkoani Morogoro Bw. Omari Jaka amesimamishwa kazi ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya fedha na madaraka.
Omari Jaka amesimamishwa kazi Februari 18 mwaka huu na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare siku ya pili ya ziara yake Wilayani Kilosa wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya bustanini vilivyoka katikati ya mji huo.
Kaimu DC Gairo Albinus Mgonya ambaye alimwakilisha DC Gairo akiwasilisha taarifa za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Mji Mdogo Mikumi.
Katika Mkutano huo Bw. Jaka amenyooshewa vidole na wananchi mara kadhaa kumtuhumu kutumia vibaya fedha mbalimbali zinazochangwa na wananchi kwa ajili ya maendeleo ya mji huo ikiwa ni pamoja na kujenga kituo cha mabasi.
Aidha, Mtendaji Jaka anatuhumiwa kuwa na matumizi yasiyoeleweka ya fedha zinazopatikana kwenye mikataba ya minara ya simu makampuni zaidi ya manne ambapo kwa mwaka zinakusanywa takribani shilingi milioni saba ingawa matumizi yake yamekuwa hayako wazi.
Mbunge wa Jimbo la Mikumi Denis Londo akitoa pongezi kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare kwa namna ambavyo anawasaidia wananchi wa Jimbo lake katika kutatua kero mbalimbali za wananchi.
Kutokan na tuhuma hizo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amechuua hatua ya kumsimamisha kazi Bw. Jaka kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili baada ya kutolewa na wananchi wa mji huo.
“nasema tena TEO atasimamishwa, Mkurgenzi ataunda tume itapitia hayo na ripoti hiyo nitapewa na mimi nijiridhishe, mambo hayaende kabisa kwenye mji huu” alisisitiza Loata Sanare.
Kwa upande wake Omari Jaka amesema kwa mjibu wa uendeshaji wa Serikali za mitaa Mamlaka ya miji midogo haina kasma, kwa hiyo haiwezi kutoa fedha benki na kutumia bila kuhamishiwa kwenye mfuko mkuu wa halmashauri na Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri kuidhinisha matumizi yake.
Kwa msingi huo, kazi ya miji midogo ni kukusanya fedha pekee na si kutumia, na endapo wanataka kutumia lazima waandike madokezo ya kuomba fedha za kutumia kwa Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri.
Baadhi ya wananchi kutoka Mji Mdogo Mikumi waliohudhuria katika mkutano wa hadhara kumsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata sanare ameagiza viongozi wote wa Serikali ndani ya Mkoa huo kuendelea kusikiliza kero za wananchi kwa kutekeleza sheria, taratibu na kanuni zote ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya mara kwa mara ili kupunguza maswali kwa wananchi.
Mwisho
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.