Mfuko wa CHF iliyoboreshwa umedhamiria kuongeza wanufaika wa Mfuko huo kwa kueleza umuhim wake na kuwahamasisha wanufaika kufikia 10% ifikapo 2022 kutoka asilimia 5 ya sasa.
Afisa Habari kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Andrew Chimesela(kushoto) akibadilishana mawazo na Afisa TEHAMA Geita wakati wa mapumziko
Hayo yameelezwa na Bi. ziada Nkinda kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI wakati akifungua Kikao kazi cha Siku moja Cha Waratibu wa CHF, Maafisa TEHAMA na Maafisa Habari wa Mikoa kinachofanyika hii leo Mei 29 katika Ukumbi wa BEACO Jijini Mbeya.
Rhobison wambura Afisa TEHAMA Mkoa wa Morogoro akiwa nje ya Ukumbi wa BEACO wakati wa mapumziko.
"Tumeona umuhimu wa maafisa habari katika kutangaza CHF ILIYOBORESHWA kwani hata mratibu akifanya vizuri bilateral kuyaandika hayo mazuri hayawezi kufika kwa walengwa ndio maana tumeona umuhimu wenu na tunaamini mtaitangaza CHF ili iwafikie watu wengi zaidi," amesema Bi. Ziada
Aidha, amesema hadi Kufikia Aprili 2021 jumla ya watu milioni 3 wamejiunga na Mfuko huo na kufanikiwa kukusanya shilingi bilioni 18 ambapo jumla ya shilingi bilioni 7 zimerudishwa katika vituo vya kutolea huduma za afya kwa ajili ya kuboresha huduma za afya kwa wananchi.
Katika hatua nyingine waratibu wa CHF ILIYOBORESHWA ngazi ya mikoa wameshauriwa kushirikiana katika kufanya kazi zao badala ya kujifungia ndani huku akisema kuwa kila mtu kwa nafasi yake anaweza kuinua Mfuko wa CHF ILIYOBORESHWA sehemu alipo.
Semina ya siku moja ya CHF ILIYOBORESHWA inafanyika mkoani Mbeya kwa lengo la kuweka mikakati ya pamoja ya kuhamasishaji Jamii kujiunga na CHF iliyoboreshwa ambapo lengo la taifa ni kufikia 30% ya wanufaika Kujiunga ifikapo 2025.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.