Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Erasto Ole Sanare ametoa salamu za pole kwa wakazi wa Mkoa wa Morogoro na watanzania wote kwa jumla kwa msiba mkubwa uliotokea wa kuondokewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli aliyefariki Dunia jana 17/3/2021.
Sanare ametoa pole hizo leo Machi 18, 2021 wakati akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake na kwamba msiba huo umewakumba watanzania wote huku akiwataka wanamorogoro na watanzania wote kuwa watulivu hususan katika kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa.
BWANA ALITOA, BWANA AMETWAA, JINA LAKE NA LIHIMIDIWE
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.