Wananchi wa Msogenzi Wilayani Ulanga wajawa na furaha
Wananchi wa Kijiji cha Msogezi Tarafa ya Vigoi Wilaya ya Ulanga Mkoani Morogoro wamejawa na furaha baada Serikali ya awamu ya sita kuwapelekea mradi wa Barabara ya Makanga hadi Mafingi yenye urefu wa km 10 ambayo hadi kukamilika kwake itagharimu kiasi cha shilingi milioni 489.
Wananchi wa Msogezi wakiwa katika furaha na kucheza ngoma ya asili
Furaha za wananchi hao zimedhihirika mara baada ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kuwasili katika kijiji hicho akiendelea na ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi ikiwa ni siku ya nne ya ziara yake.
Furaha ya wananchi wa kijiji hicho baada ya ahadi iliyotolewa na Mkuu wa Mkoa huo kuwahakikishia kuwa barabara hiyo ambayo imekuwa changamoto kwao kwa kipindi kirefu kukamilika ifikapo mwezi Oktoba ,mwaka huu ambapo pia kwa niaba yao amemshukuru Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo za kujenga barabara hiyo.
Katika hatua nyingine Martine Shigela amemuagiza Meneja wa TARURA Wilaya ya Ulanga kuhakikisha bajeti ijayo wanatenga fedha za kumalizia barabara hiyo kwa kuwa amesema kipande hicho cha barabara hata kikikamilika bado kitakuwa hakina umaana sana endapo barabra hiyo haitaungana na barabara nyingine zinazopitika.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (katikati) akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ulanga Ngollo Malenya (kulia) pamoja na Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe.Salim Alaudin Hasham wakiangalia ngoma ya asili iliyokuwa inachezwa na wananchi wa Msogezi kuonesha furaha yao
Ngollo Malenya, Mkuu wa Wilaya ya Ulanga amesema barabara hiyo itakapokamilika itakuza uchumi wa Wilaya hiyo kwa kuwa kutakuwa na mwingiliano kibiashara baina ya wilaya yake na Wilaya jirani za Kilombero na Malinyi.
Naye mbunge wa Jimbo la Ulanga Mhe. Salim Alaudin Hasham amesema ilikuwa ni ahadi yake kuona wananchi wa Msogezi wanapata barabara, hata hivyo amesema lengo kubwa si tu barabara hiyo kufika Majengo bali kufika Iragua hivyo ataendelea kupambana hadi ndoto yake itimie huku akimshukuru Mhe. Rais kwa kuwaongezea bajeti ya barabara wananchi wa Ulanga.
Kwa mujibu wa maelezo ya Meneja wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini TARURA Wilaya ya Ulanga, barabara hiyo itakayojengwa kwa kiwango cha changarawe itahusisha vijiji vya Makanga, Mdindo, Msogezi na Iragua huku msogezi hadi iragua.
Aidha ametaja baadhi ya manufaa ya mradi huo kwa wananchi wa maeneo tajwa kuwa ni pamoja na kuongeza Ukuaji wa uchumi kwa viijiji vinavyopitiwa na barabara hiyo lakini pia itakuwa njia mbadala ya kutoka mahenge mjini kwenda Iragua badala ya ile ya mlima Ndororo.
Barabara hii imeanza kujengwa tangu Januari 20 mwaka huu na ilitakiwa kukamilika Julai 22 mwaka huu, na haikukamilika kwa sababu ya mvua hivyo sasa inatarajiwa kukamilika Mwezi Oktoba mwaka huu ambapo ujenzi wake uko 45%.
Meneja huyo wa TARURA Wilaya ya Ulanga amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongeza bajeti ya ujenzi wa barabara za Wilaya hiyo kutoka milioni 514 kwa mwaka wa fedha uliopita hadi kufikia shilingi 2.2 Bil. Sawa na ongezeko la asilimia 312.
Mhe. Shigela akiwa katikati ya wananchi wakimshangilia kwa kufanya ziara katika kijiji cha Msogezi
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.