• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Huduma za maji
      • Miundombinu
      • Huduma za Ugani
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Kilombero
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za maji
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Mvomero yapokea gari ya Wagonjwa, RC aonya matumizi yasiyosahihi.

Posted on: January 5th, 2021

Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro imepata msaada wa gari ya kubebea wagonjwa (Ambulance) kutoka shirika lisilo la kiserikali  Family Federation for World Peace ili  kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Dkt. John Pombe Magufuli ya kuboresha Sekta ya Afya, hivyo kupunguza vifo visivyo vya lazima kwa wananchi wa Wilaya hiyo.

Makabidhiano ya gari hilo la wagonjwa yamefanyika leo Januari 5 katika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare na kwamba litatumika katika kituo cha Afya cha Manza kilichopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Loata Sanare amekabidhiwa gari hilo na Mwenyekiti Taifa wa Family Federation For World Peace Ndg. Stylos Simbamwene huku akibainisha kuwa  Shirikisho lake lilianza kuunga jitihada za Serikali kwa kujenga Zahanati ya Manza iliyopo Wilaya ya Mvomero na sasa wamefikia hatua ya kutoa gari hilo baada ya kuombwa ili kuboresha huduma ya Afya katika Zahanati hiyo inayotegemewa sasa kuwa Kituo cha Afya.

“Kama tunavyoona tumeletewa Hosptali ya Wilaya ya Mvomero, sisi tunazidi kuchangia maeneo madogo madogo ili huduma hiyo iwe bora zaidi, kwa hiyo kama kiongozi wa Family Federation nilipokea ombi la kuchangia gari, leo nimetekeleza” amesema Simbamwene.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, amesema, Mkoa huo umejipanga vizuri katika kuhakikisha huduma za Afya zinaboreshwa kwa kuwa Serikali tayari imeshatoa pesa nyingi kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Wilaya zote za Mkoa huo, hivyo kazi iliyobaki ni kila Kata kuwa na Kituo cha Afya.

Aidha, Sanare amesema gari hilo litasaidia kuwafikisha wagonjwa katika hospitali ya Rufaa kwa muda muafaka pale ambapo wanapewa rufaa ya matibabu katika hospitali zingine hali ambayo itasaidia kuokoa maisha ya wagonjwa.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa Sanare ametoa onyo kwa Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero kutotumia gari kwa shughuli ambazo hazijakusudiwa kutumika na gari hilo. “Sasa mkalitunze, haiwezekani Mhe. Mkurugenzi gari mkapewa mkaendelea kuhudumiwa na mfadhili aliyewapa, ni mali yenu sasa gari hili lisitumike kubeba vitu vya hovyo, wakati mwingine mnabebea vitu vya hovyo tunaona katika vyombo vya habari” amesema Sanare.

Naye, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Yusuph Mahunja amemuahidi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro kusimamia vizuri matumizi ya gari hilo kwa kufanya kazi ambazo zinazohitajika na kwa kutimiza malengo yake ya kuwahudumia wananchi wa Kituo hicho cha Afya na Halmashauri yote kwa jumla.

Family Federation for World Peace yenye Makao yake Makuu nchini Korea na hapa nchini  yakiwa Jijini Dar es Salaam ndiyo waliyojenga zahanati ya Manza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kwa sasa wanaendelea kuiboresha zahanati hiyo kuwa kituo cha Afya.

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA UTAMILIFU(MOCK) KIDATO CHA NNE MEI-2019 MOROGORO July 29, 2019
  • Karibu kuwekeza Mkoani Morogoro September 26, 2019
  • Ifahamu Miongozo ya uazishwaji wa minada ya mifugo, uuzaji wa mifugo katika minada, ukusanyaji wa mapato kupitia minada, nyaraka zinazohitajika katika kusafirisha mifugo n.k Bofya hapa.. February 14, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 - MKOA WA MOROGORO December 07, 2019
  • View All

Habari Mpya

  • Miradi 67 ya maji kutekelezwa Morogoro.

    January 15, 2021
  • Maafisa Ugani Morogoro watakiwa kuongeza jihudi, wapatiwa pikipiki.

    January 14, 2021
  • Mwenyekiti wa Kijiji mbaroni kwa kuuza Ardhi..

    January 13, 2021
  • RC Morogoro atembelea soko Kuu la Manispaa, atoa maelekezo.

    January 12, 2021
  • View All

Video

Anayetaka kumuheshimu Rais amuheshimu Mwananchi - RC Sanare
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2020 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.