• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

Gairo kuanza kuhamasisha kilimo biashara.

Posted on: September 25th, 2025



Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro imeendelea na maonesho ya kilimo ambayo hufanyika kila mwaka kwa ajili ya kutoa elimu ya kilimo kwa wakulima na mara hii imejipanga zaidi kuhamasisha kilimo biashara lengo likiwa ni wakulima kuondokana na kilimo chakula ili kuongeza uchumi kwa wakulima.

Hayo yamebainishwa Septemba 24, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Mhe. Adam Kighoma Malima wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari wakati akitoa taarifa rasmi ya maonesho hayo yanayojulikana kama “Samia Kilimo Biashara Expo 2025" yatakayofanyika wilayani Gairo kuanzia Septemba 28, mwaka huu.


Mhe. Malima amesema Wilaya ya Gairo imekuwa ya mfano katika kutekeleza mapinduzi ya kilimo biashara kwa vitendo, jambo ambalo limeongeza mapato na kuwawezesha wakulima kunufaika moja kwa moja, kwa sababu hiyo, wilaya hiyo imechaguliwa kuendelea kuwa mwenyeji wa maonesho hayo.


" ......katika haya mapinduzi ya kilimo, namba moja ni Gairo...” amesema Mhe. Adam Malima.


Akifafanua zaidi, Mkuu wa Mkoa huyo amesema mkoa pamoja na Wilaya hiyo wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi kuwa kila zao linaweza kuwa zao la biashara endapo tu litazalishwa kwa wingi ama zaidi ya mahitaji ya chakula na hivo kuondokana na kilimo CHAKULA.


Aidha, Maonesho hayo yatakwenda kutoa Elimu ya kilimo biashara hususan matumizi ya  mbinu za kisasa za uzalishaji, matumizi ya teknolojia, usindikaji wa mazao, pamoja na kujenga mitandao ya kibiashara.


Katika hatua nyingine Adam Malima amesema,  Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo imeendelea kuhakikisha Mkoa wa Morogoro unakuwa kinara wa mapinduzi ya kilimo.


Hivyo, ametoa wito kwa wakulima, wafugaji, wavuvi na wadau wote wa sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi kujitokeza kwa wingi kushiriki maonesho hayo ili wapate elimu ya mbinu bora za kilimo, teknolojia za kisasa na fursa za masoko zitakazoongeza tija na kipato chao.


Katika hatua nyingine, Mhe. Malima ametumia fursa hiyo kuwataka wananchi kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, na kwamba uchaguzi siyo vita bali ni suala la kikatiba katika kuwapata viongozi watakaowaletea wananchi maendeleo yao na kuwataka wanahabari kutumia kalamu zao kuhamasisha uchaguzi huo kuwa wa AMANI, SALAMA na KISTAARABU.


Maonesho ya SAMIA KILIMO BIASHARA EXPO 2025 yatazinduliwa Septemba 28, 2025 na kufungwa Oktoba 4 mwaka huu.



Mwisho

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • Morogoro kuanzisha jarida la programu ya PJT–MMMAM

    September 30, 2025
  • Viongozi wa Serikali Mkoani Morogoro watakiwa kulinda UHAI wa Bonde la Kilombero.

    September 26, 2025
  • Gairo kuanza kuhamasisha kilimo biashara.

    September 25, 2025
  • Gairo kuanza kuhamasisha kilimo biashara.

    September 25, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.