HALI YA CHAKULA MOROGORO
Pamoja na ziada kuna maeneo ya kanda za milimani za Halmashauri ya Mvomero yanaweza kuwa na upungufu kutokana na matokeo ya uchambuzi wa masuala ya Chakula uliofanyika Septemba 2016. Mkoa umejaliwa kuwa na mito na mabwawa mengi yenye samaki wengi. Zaidi ya 90% ya samaki wote wanapatikana kutokea mto Kilombero. Kwa msimu wa mwaka 2015/2016 Tani 255 za samaki zenye thamani ya shilingi 1,450,125,394 zimezalishwa. Mkoa una mabwawa 764, (120 ni ya asili 644 ni ya kuchimbwa.) Mwaka 2015/2016, Mkoa ulikuwa na jumla ya Mizinga 14,997, Uzalishaji wa mazao ya nyuki ikiwemo asali na nta kwa mkoa wa Morogoro ni lita 16240.6 kwa mwaka. Wastani wa uzalishaji kwa kila mzinga ni lita 3.25 ambapo ni chini ya wastani ambao ni lita 15/mzinga.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.