Kutokana wingi wa Mifugo katika Mkoa wa Morogoro, RCC iliyofanyika tarehe 27/2/2015 na tarehe 26/2/2016 kiliazimia Mkoa kutoa tamko la kusitisha uingizaji mifugo kutoka nje ya mkoa. Agizo hilo pia lilisisitiziwa na kikao cha Halmashauri ya Mkoa ya CCM iliyoketi tarehe 7/8/2015. Maagizo hayo yalipelekea Mkuu wa Mkoa kutoa tamko la kusitisha uingizaji wa mifugo kutoka nje ya Mkoa wa Morogo mnamo tarehe 20/5/2016.
Tamko la Mkuu wa Mkoa limezingatia sheria zifuatazo za mifugo;
a) Sheria ya Magonjwa ya Mifugo Na. 17 ya mwaka 2003 kifungu cha 43
b) Sheria ya Nyanda za Malisho na Rasilimali ya Vyakula vya Mifugo Na.13 ya mwaka 2010 kifungu cha 20.
c) Sheria ya Usajili, Utambuzi na Ufuatiliaji wa Mifugo Na. 12 ya mwaka 2010 kifungu cha 12 na 24
Baada ya Tamko hilo, Mkoa ulisimamia kwa dhati utekelezaji wa Tamko hilo. Shughuli kubwa iliyofanyika ni ya Utambuzi na Ufuatiliaji wa mifugo. Utambuzi wa mifugo ulifanywa kwa kuweka alama ya Chapa ya Moto kwa Ng’ombe wote walioko ndani ya Mkoa. Zoezi hilo lilianza tarehe 1 Juni, 2016 na lilikuwa endelevu.
Kuanzia 1/6/ 2016 Halmashauri zote zimekuwa zikitoa Elimu kwa njia ya mikutano ya hadhara kwa Wafugaji. Baada ya hapo wafugaji walisajiliwa na mifugo yao kupigwa Chapa. Wafugaji waliosajiliwa walipewa Vitambulisho.
Hadi kufikia 1/12/ 2016 jumla ya Ng’ombe 351,406 walipigwa chapa kati ya Ng’ombe 894,504 sawa na asilimia 39% kama jedwali linavyoonesha hapa chini.
NA
|
HALMASHAURI
|
MAKADIRIO YA IDADI YA MIFUGO
|
WALIOPIGWA CHAPA
|
ASILIMIA
|
1 |
Malinyi
|
79709
|
106130
|
133%
|
2
|
Ulanga
|
26119
|
44434
|
170%
|
3
|
Morogoro
|
164691
|
2479
|
1.5%
|
4
|
Manispaa
|
5320
|
3020
|
57%
|
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.