Ili kuongeza uzalishaji msimu wa 2016/17 Mkoa umeendelea kusimamia shughuli mbali mbali za kilimo
1.Usambazaji wa pembejeo za ruzuku ambapo mkoa umepokea Mbolea ya kukuzia tani 1,080, Mahindi tani 162 na Mpunga tani 120. (Kaya 21,600 Mbolea, 24,200- Mbegu)
2.Mradi wa kuendeleza skimu ndogo za umwagiliaji (SSIDP) ambapo mkoa ulipokea jumla ya Tshs. 2, 740, 000,000/= Kwa ajili ya kuendeleza skimu 4 ambazo ni Kiroka na Tulo Kongwa (Morogoro) Wami Luhindo (Mvomero), Lumuma (Kilosa) na Minepa (Ulanga).
3. Mradi wa Kuongeza tija na uzalishaji wa zao la mpunga (Expanding Rice Production Project –ERPP). Mradi huu utaendeleza ujenzi wa skimu tano za mkoa wa Morogoro ambazo ni Kigugu na Mbogo kwa Mtonga (Mvomero), Mvumi (Kilosa), Njage na Msolwa ujamaa (Kilombero). Kila skimu itajengea ghala. Pia mradi utatoa mafunzo ya Kilimo shadidi kwenye skimu 40 za Mkoa wa Morogoro.
4,Mradi wa MIVARF unaofadhiliwa na Banki ya Afrika. Unajenga maghala ya kuhifahi mazao katika Halmashauri za Wilaya ya Mvomero, Kilombero, Ulanga na Malinyi. Mradi pia utatoa mashine za kukoboa na kupanga Mpunga kwenye madaraja Kwa wilaya hizo isipokuwa Kilombero
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.