Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka watumishi wa Wilaya ya Mlimba Mkoani humo kuacha kutumia kigezo cha uwepo wa mazingira magumu katika maeneo yao ya kazi kushindwa kutoa huduma nzuri kwa wananchi.
Mhe. Malima ametoa agizo hilo hivi karibuni alipofanya ziara ya kikazi katika halmashauri hiyo ya mlimba Wilayani Kilombero na kukutana na watumishi hao ikiwa ni siku yake nne ya ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo.
"... kwenye mazingira hayo magumu isiwe kisingizio cha kutoa huduma mbovu kwa wananchi.." amesema Adam Malima.
Mkuu huyo wa Mkoa amesema anatambua uwepo wa mazingira magumu ya watumishi wa wilaya hiyo hata hivyo kamwe isichukiwe kuwa ni adhabu au wao sababu ya kutotoa huduma nzuri kwa wananchi badala yake amewataka watumishi hao wajitathimini katika utendaji kazi wao ili waweze kuleta maendeleo katika wilaya ya Mlimba.
Hata hivyo amewapongeza kwa kazi nzuri waliokwishaifanya mpaka sasa huku akidai kuendelea kuongeza juhudi kwani maendeleo yaliyopo sasa na fursa zilizopo hazilingani mafanikio yanayotarajiwa na wengi
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.