Watu 22 wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la Melela Kibaoni Mkoani Morogoro barabara ya Morogoro - Iringa leo Machi 18 2022. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Fortunatus Musilimu amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo pamoja na vifo vya watu hao.
akieleza kwa kina zaidi Kamanda Musilim amesma ajali hiyo imehusisha magari mawili ambalo ni Basi la abiria lenye namna za usajili T 732 ATH lililokuwa likitokea Mbeya kwenda Tanga na Lori lenye namba za usajili IT 2816 lililokuwa likitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya huku zoezi la uokoaji baadhi ya majeruhi likiendelea.
kutokana na ajali hiyo mbaya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amempa pole Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine shigela. "Nawapa pole wafiwa, nawaombea marehemu wapumzike mahala pema na majeruhi wapone haraka" . amesema Mhe Rais.
Aidha, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka watumiaji wote wa barabara kufuata sheria zote za Barabarani wakati wote wanapotumia miundombinu hiyo
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.