Alhaji Sengulo na dhana ya kusaidia wahitaji.
Jamii imeaswa kuwa na tabia ya kusaidia watu wenye uhitaji wakiwemo yatima, wajane na wazee ili kujipatia thawabu za mwenyezi Mungu na kujenga jamii inayosaidiana bila kubaguana wala kujali utofauti wa imani zao.
Nasaha hizo zimetolewa Julai 11 mwaka huu na Alhaji Hamis Sengulo wakati wa sherehe ya kwaya ya Mtakatifu Petro na Paulo ya Kigango cha Kristu Mfalme kilichopo Parokia ya Mtakatifu Maria Modeco Jimbo katoliki la Morogoro.
Alhaji Sengulo akipokelewa na baadhi ya Viongozi wa Kwaya ya Mt. Petro na Paulo Modeko baada ya kualikwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo
Alhaji Sengulo (kushoto) akipokea Risalaya wanakwaya wa Mt. Petro na Paulo kigango cha Kristo Mfalme. Kulia ni mama Mlezi wa kwaya hiyo.
Alhaji Hamisi Sengulo (aliyevaa koti Jeusi) akishiriki kuimba kwaya pamoja na wanakwaya ya Mt. Petro na Paulo kigango cha Kristo Mfalme
Alhaji Sengulo ambaye licha ya kuwa yeye ni Muumini wa Dini ya Kiislamu amealikwa na wanakwaya wa Kigango hicho kusherehekea sherehe za somo wao Petro na Paulo huku akishauri kuwa dini zote zina lengo moja la kumwabudu mungu na kuhubiri Amani na upendo kwa watu wake.
“Kila mtu anaabudu mwenyezi Mungu kwa staili yake lakini anamwabudu mwenyezi Mungu, uwe unamwabudu kupitia kanisani, kupitia msikitini lakini unafanya ibada, kwa hiyo ndugu zangu naomba tuwe wamoja” alisema Alhaji sengulo.
Wanakwaya ya Mt. Petro na Paulo wakiimba nyimbo za kumwabudu Munguwakati wa maadhimisho ya sherehe yao
Katika hatua nyingine Alhaji Sengulo ameitaka jamii kwa jumla kudumisha Amani ndani ya nchi yetu ili kuwa na mazingira tulivu ya watu kuabudu na kujiletea maendeleo yao kwani bila amani hakuna Ibada wala maendeleo hivyo amewaasa viongozo wa madhehebu na dini zote kwa jumla waendelee kuwahimiza waumini wao jumuhimu wa Amani.
‘’Tudumishe sana Amani ya nchi yetu, kwa sababu bila Amani ibada hazifanyiki, kukiwa kuna vita kuna shida hata ibada hazifanyiki. Huwezi kufanya ibada msikitini wala Kanisani kama hamna Amani’’ alisisitiza Alhaji Sengulo.
Akiwa mgeni rasmi katika sherehe hizo, Alhaji Sengulo ameahidi kukarabati baadhi ya miundombinu ya kigango hicho ikiwemo ukarabati wa vyoo na kuunganishe nguvu zake na rafiki zake kwenye ujenzi wa nyumba ya mapadre katika kigango hicho kinachotarajiwa kuwa parokia hivi karibuni nyumba ambayo inahitaji zaidi ya Tsh. 100 Mil. hadi kukamilika kwake.
Kwa upande wake Katibu wa Kwaya ya Mtakatifu Petro na Paulo Ndugu Bertam Minde amemshukuru Alhaji Hamis Sengulo kwa kukubali kukarabati miundo mbinu ya kigango chao huku akiendelea kumuomba asichoke kusaidia Ujenzi unaoendelea wa nyumba ya Mapadre unaoendelea kujengwa katika kigango hicho.
Kwa upande wake Mama mlezi wa kwaya ya Mtakatifu Petro na Paulo amesema uongozi wao kwama viongozi wanaendelea kutafuta njia mbalimbali za kukijenga kigango hicho kwa kuwaomba marafiki ndugu na kjmaa zao huku akiwataka kupendana, kuvumiliana na kumtanguliza Mungu kwa kila jambo.
Alhaji akipokea Risala iliyosomwa kwake.
Awali akisoma risala kwa mgeni rasmi, Bi. Edina Gutapaka alibainisha changamoto mbalimbali zinazokabili Kigango cha Kristo Mfalme kuwa ni pamoja na ukosefu wa fedha za ujenzi wa nyumba ya paroko, Ukarabati wa Miundombinu ya Kigango hicho na ukosefu wa vyombo vya muziki kwa ajili ya kwaya hiyo.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.