Kamisaa wa Sensa ya watu na Makazi Taifa Bi. Anna Makinda amekemea vikali kwa wale watakaohusika kupokea fedha kutoka kwa wanaoomba ajira ya ukalani wa zoezi la sensa na nafasi nyingine kwa kuwa kufanya hivyo ni kukiuka utaratibu uliowekwa.
Anna Makinda ambaye pia ni Spika Mstaafu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema hayo wakati akiongea na Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano Serikalini Katika Hotel ya Regal Naivera Jijini Tanga wakiwa Katika kikao kazi Chao Cha 17.
.
Aidha, Anna Makinda amewataka waombaji wenyewe kujiamini kupata ajira hiyo bila kutoa fedha kwa mtu yeyote hususan Kama sifa za kuomba nafasi hiyo anazo.
Amesema utoaji wa fedha wa namna yoyote kwa mtu yeyote kwa minajiri ya kupata ajira hiyo hautamsaidia mwombaji kupata ajira Kama hajatimiza vigezo husika na zaidi zoezi hilo linaendeshwa kidijtali zaidi hivyo hakuna nafasi ya kurubuniwa kwa namna yoyote.
Aidha, amewataka watanzania wote kujiandaa vema na kujitokeza wakati wa Sensa kuhesabiwa ili Taifa kuwa na takwimu sahihi kwa ajili ya Maendeleo ya Taifa na Maendeleo ya wananchi wenyewe.
Kwa mujibu wa Kamisaa huyo zoezi la sensa limefikiwa asilimia 81.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.