• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

ANZISHA HUDUMA ZA KIPAUMBELE - DKT. GWAJIMA .

Posted on: April 27th, 2021

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima amewataka waganga wakuu wa Mikoa (RMO) na wa Wilaya (DMO) zote hapa nchini kuanzisha huduma za kipaumbele katika vituo vya Afya ambavyo havijakamilisha ujenzi wa jengo la mama na mtoto zikiwemo huduma za chanjo, kupima akinamama wajawazito na matatizo madogo ya dharura wakati Serikali inajipanga kukamilisha majengo hayo.

Dkt. Gwajima ametoa agizo hilo leo April, 27 wakati wa uzinduziwa wiki ya chanjo Kitaifa iliyofanyika katika viwanja vya Shule ya Msingiya Chamwino “B” katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

‘’Tutaanza kulia na jina la Gwajima kwasababu uwezekano wa kufanya vitu upo halafu hatufanyi, matatizo yetu nimengi na rasilimali ni chache lakini tukijiongeza tutaweza kupunguza tatizo mojawapo hasa matatizo yanayogusa huduma za mama na mtoto’’ amesema Dkt. Gwajima.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amesema lengo la siku ya chanjo duniani, ni kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa Afya katika kujikinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo na kuepuka vifo vinavyoweza kuzuilika kwa njia ya chanjo.

Aidha, Loata Sanare amewaagiza Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi Mkoani humo kuhakikisha wanasimamia zoezi la kuhamasisha wazazi kuwapeleka watoto katika vituo vya afya kwa ajili ya kupata chanjo na Elimu juu ya umuhimu wa chanjo.

Sambamba na hayo, Loata Sanare amebainisha kuwa kuongezeka kwa vituo vya kutolea huduma za Afya Mkoani humo, kumewanufaisha wananchi na kuhakikisha huduma zinawafikia popote walipo ikiwa ni sera ya Rais wa awamu ya sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. SamiaSuluhu Hassan.

Kwa upande wake Mwakilishi kutokaShirika la Afya Duniani – WHO Dkt. William Mwengee ameipongeza Tanzania kwa kutokomeza baadhi ya magonjwa kutokana na ufanisi wa chanjo ambayo imekuwa ikifanyika ikiwemo chanjo ya ugonjwa wa Fulio na Surua.

Dkt. Mwengee amesema WHO itaendelea kutoa ushirikiano na Tanzania katika kutoa huduma za Afya ili kufikia malengo endelevu ya kutoa huduma kwa wananchi ikiwepo huduma ya chanjo mbalimbali.

Mwakilishi kutoka Ofisiya Rais TAMISEMI Bi. Joseline Ishengoma, ametoa wito kwa wazazi kuwapeleka watoto katika vituo vya Afya kwa lengo la kupata chanjo na huduma nyingine kwa kuwa kwa sasa katika vituo vya kutolea huduma za Afya kuna vifaa na watumishi wakutosha wa kutoa huduma hiyo.


MWISHO.


Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • MSEMAJI MKUU WA SERIKALI AWATAKA MAAFISA HABARI KUFANYA KAZI ZAO KIMKAKATI.

    May 26, 2025
  • MWAROBAINI WA CHANGAMOTO YA MAJI MOROGORO HII HAPA, RC MALIMA ATOA MAAGIZO.

    May 24, 2025
  • UZALISHAJI WA MAZIWA KUCHANGIA BIL. 18 KWA MWAKA MOROGORO

    May 23, 2025
  • MAAFISA HABARI TOENI UFAFANUZI DHIDI YA UPOTOSHAJI- MCHENGERWA

    May 23, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.