Bajeti ya TARURA Mkoani Morogoro yapaa hadi Tsh. bilioni 61.
Meneja wa Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini Tanzania (TARURA) Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Ndyamukama ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuwaongezea fedha za utekelezaji wa miundombinu ya barabara Mkoani humo kutoka shilingi bilioni 7 hadi kufikia shilingi bilioni 61.
Mhandisi Ndyamukama ameyasema hayo Novemba 2, mwaka huu wakati wa mkutano wa Mkuu wa Mkoa pamoja na Msemaji Mkuu wa Serikali na Waandishi wa Habari ikiwa ni Kampeni ya kutangaza Mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita yaliyofanyika mkoani humo, mkutano uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Mhandisi Ndyamkama amesema wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia Madarakani imekuta bajeti ya TARURA Mkoani humo ikiwa ni shilingi bilioni 7. 9 kwa mwaka, lakini kwa kipindi cha miaka miwili na nusu ya Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan bajeti hiyo imeongezeka hadi kufikia shilingi bilioni 61.45.
“...wakati Serikali ya Awamu ya Sita inaingia Madarakani tulikuwa tunapata mgao wa fedha shilingi bilioni 7. 9 kwa mwaka, lakini alivyoingia tu mpaka sasa hivi tumeweza kupata jumla ya shilingi bilioni 61.45...kwahiyo hii ni kazi kubwa ambayo Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameifanya...” amesema Mhandisi Ndyamukama.
Aidha, ameongeza kuwa fedha hizo zimesaidia kufungua barabara mpya zenye jumla ya km 190 ambazo zimeelekezwa kwenye huduma za jamii zikiwemo shule, hospitali, masoko, maeneo ya utalii, maeneo ya kuabudia na maeneo ya uzalishaji hususan kilimo.
Sambamba na hayo, Meneja wa TARURA amesema fedha hizo zimeongeza mtandao wa barabara za lami kutoka km 87.63 hadi km 99. 15, changarawe km 987.24 hadi km 1456.75, barabara za kiwango cha zege km 5.6, Madaraja mawaili likiwemo daraja la Berega lenye urefu wa mita 140 amabalo limegharimu shilingi bilioni 7.9 na daraja la Luhembe lenye mita 40 amabapo gharama yake ni shilingi bilioni 1. 2.
Nao wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mlimba Mhandisi Stephano Kaliwa wamekiri uboreshaji wa miundombinu katika halmshauri zao huku akimshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassa kupitia TARURAna kwamba Halmashauri ya mlimba inatarajia kuchonga barabara ya Mlimba - Uchindile yenye km 80 ambayo itawasaidia kuondokana na adha ya kuzunguka kwenda Mafinga Wilyani Mufindi Mkoani Iringa kufuata huduma za Afya.
“Mhe. Rais amewasikia na amewafikia Wananchi wake”.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.