Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Yasushi Misawa amemtembelea Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima ofisini kwake leo Julai 27, 2023 na kujadili masuala kadha wa kadha ya kimaendeleo.
Pichani ni Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa wakati akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Malima.
Moja ya sekta zilizoguswa kwenye mazungumzo ya viongozi hao wawili ni pamoja na kilimo, uwekezaji na utunzaji wa mazingira.
Balozi wa Japan nchini Tanzania Mhe. Yasushi Misawa akisaini kitabu cha wageni baada ya kuwasili katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
Pichani ni baadhi ya wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro wakiwa kwenye tukio hilo.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.