Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima, Machi 15,2024 ametembelewa na Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Tone Tinnes Pamoja na mwakilishi wa Balozi wa Denmark Dkt. Mette Bech Pilgaard na kufanya mazungumzo kuhusu maendeleo ya Mkoa huo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima kushoto akiagana na mwakilishi wa Balozi wa Denmark Dkt. Mette Bech {kulia} mara baada ya kumaliza mazungumzo.
Wakiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa nyakati tofauti, Balozi wa Norway hapa nchini Pamoja na kufika Ofisini hapo kusaini kitabu cha wageni, mefanya ziara ya kujionea utekelezaji wa miradi ya wadau wa SAGCOT inayotekelezwa mkoani humo Pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambaye ndiye mdau namba moja katika kuratibu uwekezaji wa Kilimo biashara na utuzaji wa mazingira.
Aidha, Balozi huyo alifanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa kwenye hifadhi ya Taifa ya milima ya Tao la mashariki, miradi ambayo inafadhiriwa na Ubalozi huo kwa lengo la kuongeza kipato kwa wananchi wanaozunguka milima hiyo ili kupunguza kasi ya uharibifu wa mazingira wa milima hiyo kupitia kilimo na ukataji miti kwa lengo la kujipatia kipato.Mkuu wa Mkoa ameahidi kuendeleza Ushirikiano na SAGCOT ili kuleta mapinduzi ya kilimo hususan mazao ya viungo na matunda ndani ya Mkoa wa Morogoro.
Mkuu wa Mkoa ameahidi kuendeleza Ushirikiano na SAGCOT ili kuleta mapinduzi ya kilimo hususan mazao ya viungo na matunda ndani ya Mkoa wa Morogoro.
Baadhi ya wataalam wa Kilimo na biashara kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro wakati wa Mazungumzo ya Mkuu wa Mkoa na Mgeni wake. Kulia ni Dkt. Rozaria Rwegasira ambaye ni Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na uzalishaji Mali
Kwa upande wake Mwakilishi wa Balozi wa Dermark Dkt. Mette Bech Pilgaard na Mwenyeji wake wamezungumzia Uhifadhi wa Mazingira katika Bonde la Mto Kilombero Wilayani humo pamoja na ukuaji wa Uchumi kwa wananchi wa Wilaya hiyo na Mkoa wa Morogoro kwa ujumla.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemwambia Mwakilishi wa Balozi wa Denmark hapa nchini, nia ya Mkoa ya kurudisha uoto wa asili katika milima ya Uluguru, Udzungwa na milima mingine ndani ya Mkoa huo ambayo ni vyanzo vikuu vya maji yanayozalisha Umeme wa maji hapa nchini lakini pia maji hayo yanatumika katika kilimo cha mazao mbalimbali yakiwemo zao la mpunga Pamoja na zao la miwa ambalo linatoa sukari katika Viwanda vya Sukari vya Kilombero, Mtibwa na Mkulazi.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima (kushoto} akiwa na Balozi wa Norway Mhe. Tones Tinnes alipomtembelea Ofisini kwake
Kwa sababu hiyo Mkuu huyo wa MKoa amemwambia Dkt. Mett Bech Pilgaard kuwa Mkoa umeanzisha program ya kuwahamasisha wananchi kupanda mazao ya kimkakati ili kurudisha uoto wa asili kwenye milima hiyo ambayo pia itawaongezea kipato wananchi hao.
Kulia ni Balozi wa Norway hapa nchini Mhe. Tones Tinnes
Ameyataja Mazao hayo kuwa ni Karafuu, Kakao, Michikichi, Kahawa na Parachichi, kwamba wananchi wakipanda mazao hayo katika milima hiyo itasaidia kutunza mazingira na kuondoa uharibifu wa mazingira unaojitokeza kila uchao hivyo kumuomba Balozi kusaidia programu hiyo.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.