TANROADS Morogoro yaongezewa bajeti kwa ajili ya matengenezo ya Barabara
Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutoa fedha katika Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matengenezo ya barabara na miundombinu mingine na kuongeza Bajeti kutoka Tsh. Bil. 24.8 mwaka 2020/2021 hadi kufikia Tsh. Bil. 26.02 mwaka 2021/2022.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela wakati akifungua kikao cha 37 cha Board ya Barabara Mkoa wa Morogoro kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ualimu Morogoro leo Oktoba 7, 2021.
Mkuu huyo wa Mkoa ameendelea kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho kuwa kwa upande wa Bajeti ya Maendeleo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 ilikuwa Tsh. Bil. 2.75 na kuongezeka hadi Tsh. Bil. 5.37 mwaka 2021/2022 zikiwemo Tsh. Bil. 2.4 iliyotolewa kwa ajili ya Barabara ya Bigwa – Kiloka Km. 15 kwa kiwango cha lami.
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.