Mwekezaji Bodi ya Pamba Tanzania amefanya Uwekezaji wa Kilimo cha zao la Dengu katika Eneo la Shamba la Kijiji cha Kikwawila lililopo Kata ya Kibaoni kwa Kipindi cha Miezi minne kuanzia Agasti hadi Novemba 2025 ambapo Shamba hilo huwa halitumiwi na Wanakijiji kwani kwa Kipindi hiko huwa wamevuna Mazao yao na kusubiri kipindi kingine cha Msimu wa Kilimo cha Mpunga ambacho huanza mwezi Novemba. Aidha Mwekezaji huyo amekodi shamba hilo kwa Shilingi Milioni 50,000,000 ambayo inawekwa katika Akaunti ya Benki ya Kijiji ambapo kila Ekari sh. 5,000.
Akizungumza wakati wa Mkutano wa Wanakijiji cha Kikwawila , Viongozi wa Serikali ya Kijiji, Halmashauri, Wilaya na Wawekezaji hao leo Jumapili Tarehe 20 Julai 2025, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima aliwaeleza Wanakijiji hao kuwa mbali na Mwekezaji huyo kukodi ekari hizo pia atawalimia Wananchi ekari elfu 2 ,000 kati ya Ekari 11 anazozikodi na kwamba Wananchi hao watazimamia na kuwa mfano kwa wengine.
" Zitalimwa Ekari elfu 11 zote na Ekari Elfu 2 zitalimwa kwaajili ya Wanakijiji kila mtu atapewa azisimamie kwenye utaratibu wa Ushirika wa Kijiji, Ekari elfu 9 zitakuwa kwaajili ya Mwekezaji". Alisema Mhe. Malima
Kwa upande wake Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Pamba Aggrey Mwanri alisema katika Uwekezaji huo Wanakijiji hao watanufaika kwa kuwa Bodi ya Pamba itachangia Shughuli za kimaendeleo za Kijamii kama Elimu, Afya, Miundo mbinu n.k
Mmoja wa Wananchi wa Kijiji hicho Bw. Martine Ngwega alieleza kuwa Ujio wa Mwekezaji huyo katika Eneo hilo utanufaisha Wananchi wa Kijiji hicho kwani kwa Kipindi ambacho wanakuwa wamevuna Mpunga eneo hilo linakuwa halitumiki hivyo kuja kwa Mwekezaji huyo kutaendelea kuongeza mapato na ustawi wa Kijiji hicho.
" Tunashukuru Mwekezaji kwa kulichagua eneo letu, kwani pia suala la Miundo mbinu ameahidi kututengenezea na Vijana wetu watapata Ajira kupitia Uwekezaji huu". Alisema Bw.Ngwega
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.