Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini (CDF) Jenerali Venance Mabeyo leo Septemba 9, 2021 amefanya ziara ya kikazi ya siku moja Mkoani Morogoro.
Akiwa Mkoani humo, Jenerali Mabeyo pamoja na waandamizi wake amefanya kikao kifupi na mwenyeji wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Morogoro ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa huo Martine Shigela.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini Jenerali Venance Mabeyo alipowasili Mkoani humo.
Jenerali Venance Mabeyo akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Morogoro.
Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na Jenerali Venance Mabeyo pamoja na Waandamizi wake mara baada ya kikao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mariam Mtunguja (kushoto) akisalimiana na Venance Mabeyo alipowasili Ofisini hapo
Generali Venance Mabeyo Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama akiwasili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.