Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare amewataka wajumbe wa Bodi za Shule za Sekondari Mkoani hapa kutowafumbia macho Wanafunzi wote wanaofanya uhuni wowote Shuleni badala ya Kuzingatia masomo.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akimkabidhi kiti Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kihonda Paul Kadege.
Loata Sanare amesema hayo leo Februari 19 mwaka huu alipokuwa anapokea Madawati na viti 110 yaliyotolewa na Benki ya NMB katika shule ya Sekondari Lupanga iliyopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Loata Sanare amesema Serikali ya awamu ya tano pamoja na wazazi wanahangaika kwa ajili ya watoto wao hivyo si haki kwa Wanafunzi kuacha masomo yao na kujihusisha na masuala ya uhuni.
Mkuu wa Mkoa akimkabidhi kitu Mkuu wa Shule ya sekondari ya lupanga Flora Ndunguru.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa huyo ametoa pongezi kwa kanda ya Mashariki kwa kuwa na Utamaduni wa kuunga Mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hususan katika sekta ya Elimu
Naye Diwani wa Kata ya Kilakala Marco Kanga amewataka walimu na menejimenti za Shule zilizopata msaada huo wa viti na Madawati kutunza miundombinu hiyo ili iwasaidie kwa muda mrefu.
Shule zilizopokea msaada huo ni Shule ya Sekondari ya Lupanga iliyopo Kata ya Kilakala na Shule ya Sekondari ya Kihonda iliyopo Kata ya Mazimbu katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.