CHMT yatakiwa kusimamia ufungaji vifaa tiba vya hospitali.
Mkurugenzi wa Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais -TAMISEMI Dkt. Rashid Mfaume ameitaka Timu ya Uendeshaji wa Huduma za Afya ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro (CHMT) kuhakikisha vifaa tiba vyote vilivyopelekwa katika Hospitali ya Halmashauri hiyo vinafungwa ili hospitali ianze kutoa huduma ya upasuaji kwa wananchi.
Dkt. Mfaume ametoa agizo hilo Januari 25, 2024 wakati akizungumza na CHMT watumishi wa afya wa hal shauri ya Wilaya ya Morogoro alipokuwa akikagua ujenzi na huduma zinazotolewa hospitalini hapo.
Mkurugenzi huyo amesema, hospitali imeanza kufanya kazi lakini baadhi ya vifaa na vifaa tiba hususan vya upasuaji vilivyopelekwa havijafungwa hivyo kukosesha utoaji wz huduma muhim kwa wananchi kutokana na vifaa hivyo kutofanya kazi.
“Serikali imenunua vifaa tiba ili kuwaondolea adha wananchi wake, katika bajeti ya mwaka 2022/23 jumla ya Shilingi Milioni 550 zilitengwa kununua vifaa na vifaa tiba katika hospitali hii na mpaka sasa fedha hizo zimekwishapokelewa na kwa upande wa ununuzi wa vifaa na vifaa tiba vimenununuliwa vyenye thamani ya Shilingi 247 hivyo ni jukumu la watumishi kushirikiana na kuhakikisha wanavifunga, wanavitumia na kuvitunza,” amesema Dkt. Mfaume.
Aidha, amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uaminifu na uadilifu huku akieleza kuwa takwimu zinaonesha wilaya hiyo ina viashiria vya upotevu mkubwa wa bidhaa za afya zikiwemo dawa hali inayopelekea Serikali kulaumiwa kwamba haipeleki dawa kwenye hospitali zake.
Naye Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt. Robert Manyerere amesema hospitali hiyo ni msaada kwa zaidi ya wakazi 387,736 wa Halmashauri hiyo na kwamba amepokea maagizo ya Serikali na kuahidi kuyatekeleza yeye pamoja na timu yake.
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.