DARAJA LA GHARAMA YA TSH 1.3 Bil. LAWEKEWA JIWE LA MSINGI KILOMBERO
Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024 Ndugu Godfley Mnzava kwa mara nyingine amezikumbusha zote za Serikali hapa nchini Pamoja na mashurika ya umma kutumia mfumo wa manunuzi wa Nest ili kudhibiti matumizi mabaya ya fedha za Umma na kuondoa manung’uniko miongoni mwa wazabuni wanaoomba tenda bza kazi Serikalini.
Kiongozi huyo wa mbipo za Mwenge wa Uhuru Kitaifa ametoa maelekezo hayo wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru Wilayani Kilombero ambapo ameweka jiwe la msingi la Chiwa chiwa ambalo litawanufaisha wananchi wa vijiji zaidi ya vine.
Daraja hilo ambalo ujenzi wake uko zaidi ya asilimia 90, hadi kukamilika kwake litagharimu kiasi cha shilingi 1.3 Bil. Huku ujenzi wa Barabara inayopita Daraja hilo utagharimu kiasi cha shilingi milioni 600 hivyo kufanya jumla ya mradi wote kuwa shilingi Bil. 1.9.
Ukiwa Wilayani Kilombero Mwenge huo wa Uhuru utapitia mieadi 7 ya maendeleo yenye thamani ya shilingi Bil. 3.
Kesho Aprili 24,2024 Mwenge wa Uhuru utakimbizwa Wilaya ya Ulanga ambayo ni Wilaya ya tano kukimbizwa Mwenge huo wa Uhuru kwa Mkoa huo wa Morogoro.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.