DC Gairo awataka uzalendo makarani, wananchi kujitokeza kuhesabiwa.
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Jabir Makame amewataka makarani wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi kuwa wazalendo katika kutekeleza jukumu walilopewa wakitambua kuwa wamepewa dhamana kubwa na serikali kwa mstakabali wa maendeleo ya wananchi wenzao na taifa kwa jumla.
DC Gairo Jabir Makame akiwa ameshika picha ya Mhamasishaji wa sensa namba moja hapa nchini Rais wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa matembezi ya Tamasha la kuhamasisha Sensa
Jabir Makame ametoa rai hiyo Jana Agosti 13, 2022 wakati akihitimisha Tamasha la Sensa ya watu na Makazi lililofanyika Wilayani humo likitanguliwa na matembezi ambalo lililenga kuhamasisha wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo mengine kujitokeza kuhesabiwa wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.
“Niendelee kuwasihi ndugu zetu makarani, ndugu zetu mliopewa fursa na kupewa dhamana ya kulifanya hili jukumu, nendeni makalifanye hili jukumu kizalendo, mkitambua kwamba serikali imewapa dhamana kubwa sana kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu” amesema Mkuu wa Wilaya Jabir Makame.
“Ubora wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka huu, unategemea sana kazi ambayo mnayokwenda ninyi kuifanya” amesisitiza Jabir Makame.
wakati ewa maandamano ya tamasha
Mkuu wa Wilaya Jabir Makame akivishwa skafu wakati wa tamasha la sensa
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wa Gairo kujitokeza kwa wingi siku ya sense na kuhesabiwa ili kuisaidia serikali kutambua idadi ya watu wake na kupanga mipango ya kimaendeleo hivyo kuweza kuboresha huduma za kijamii ikiwemo huduma za Afya, Maji, Elimu na masuala mengine ya kijamii.
Amesema lengo jingine la sense ni kusaidia wadau wengine wa maendeleo kujua idadi sahihi ya watanzania ili kuungana na serikali katika kutoa huduma za kijamii na kiuchumi na kuwaomba wana gairo kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa wakati wa zoezi hilo na kuwahamasisha wengine kushiriki sense ya watu na makazi na kwa kufanya hivyo watakuwa wanaungana na Rais wao Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye halali kwa ajili ya kuwaletea watanzania maendeleo.
Viongozi mbali mbali walioshiriki tamasha hilo. kulia ni Mratibu wa Sensa Mkoa ewa Morogoro Charles Mtabo, na kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Gairo
DC Gairo akiserebuka pamoja na kikundi cha burudani cha gairo wakati wa tamasha la sensa
baadhi ya washiriki wa tamasha la sensa
Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa ambaye alitarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Jabir Makame amesema pamoja na kwamba Mkuu huyo wa Mkoa ameshindwa kufika baada ya kuwa na majukumu mengine ya kiofisi hata hivyo amesema anafarijika na kazi nzuri inayofanywa na wanaGairo na anaomba ushirikiano wa wananchi wa Gairo ili kuendelea kufanya kazi kwa maendeleo ya wanaMorogoro.
Kwa upande wake Mratibu wa Sensa Mkoa wa Morogoro Charles Mtabo amesema maandalizi ya zoezi la sense kwa Mkoa wa Morogoro linaendelea vizuri na kubainisha kuwa Mkoa umeongezewa vishikwamba vingine zaidi ya elfu kumi ambavyo vitasaidia kila karani Mkoani humo kuwa na kishikwamba kwa ajili ya zoezi hilo muhimu.
Katika hatua nyingine viongozi wa vyama vya siasa Wilayani Gairo wameungana na viongozi wa chama Tawala, chama cha mapinduzi na wananchi wa Gairo kwa ujumla kushiriki tamasha hilo, akiongea kwa niaba ya chama chake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilayani Gairo Bw. Ernest Bonifance Mkami amedai kuridhishwa na Serikali ya awamu ya sita kwa namna ambavyo imeshirikisha makundi mabali mbali kwenye jambo hilo la kimaendeleo.
“nimeona ni vema tushiriki zoezi hili la sense ya watu na makazi kwa kutambua kuwa jambo hili ni muhimu sana kwa taifa” amesema Bonifance Mkami.
“lakini sisi kama chama tumerishwa na namna serikali ilivyoshirikisha jamii na makundi mablimbali kushiriki kwa pamoja kuhakikisha Tanzania tunapata idadi halisi ya wananchi ambayo ni muhim kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla” amesisitiza Mwenyekiti huyo wa CHADEMA.
viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa wakiwa na bendera zao wakati wa tamasha la sensa, huku wakidai kuwa masuala ya maendeleo hayana chama
Zoezi la sense ya watu na makazi linatarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu.
SENSA KWA MAENDELEO, JIANDAE KUHESABIWA
Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabir Makame (aliyevaa Tisht nyeupe) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa vyama mbalimbali vya siasa vilivyopo katika Wilaya hiyo wakati wa tamasha la sensa ya watu na makazi lililofanyika Agosti 13 mwaka huu
MWISHO
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.