• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

DC GAIRO AWATAKA UZALENDO MAKARANI WA SENSA

Posted on: August 13th, 2022

DC Gairo awataka uzalendo makarani, wananchi kujitokeza kuhesabiwa.

Mkuu wa Wilaya ya Gairo Mkoani Morogoro Jabir Makame amewataka makarani wa zoezi la Sensa ya watu na Makazi kuwa wazalendo katika kutekeleza jukumu walilopewa wakitambua kuwa wamepewa dhamana kubwa na serikali kwa mstakabali wa maendeleo ya wananchi wenzao na taifa kwa jumla.

Jabir Makame ametoa rai hiyo Jana Agosti 13, 2022 wakati akihitimisha Tamasha la Sensa ya watu na Makazi lililofanyika Wilayani humo likitanguliwa na matembezi ambalo lililenga kuhamasisha wananchi wa Wilaya hiyo na maeneo mengine kujitokeza kuhesabiwa wakati zoezi la Sensa ya watu na makazi linalotarajiwa kufanyika Agosti 23 mwaka huu.

“Niendelee kuwasihi ndugu zetu makarani, ndugu zetu mliopewa fursa na kupewa dhamana ya kulifanya hili jukumu, nendeni makalifanye hili jukumu kizalendo, mkitambua kwamba serikali imewapa dhamana kubwa sana kwa mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu” amesema Mkuu wa Wilaya Jabir Makame.

“Ubora wa Sensa ya watu na Makazi ya Mwaka huu, unategemea sana kazi ambayo mnayokwenda ninyi kuifanya” amesisitiza Jabir Makame.

Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa Wilaya amewataka wananchi wa Gairo kujitokeza kwa wingi siku ya sense na kuhesabiwa ili kuisaidia serikali kutambua idadi ya watu wake na kupanga mipango ya kimaendeleo hivyo kuweza kuboresha huduma za kijamii ikiwemo huduma za Afya, Maji, Elimu  na masuala mengine ya kijamii.

Amesema lengo jingine la sense ni kusaidia wadau wengine wa maendeleo kujua idadi sahihi ya watanzania ili kuungana na serikali katika kutoa huduma za kijamii na kiuchumi na kuwaomba wana gairo kutoa ushirikiano kwa makarani wa Sensa wakati wa zoezi hilo na kuwahamasisha wengine kushiriki sense ya watu na makazi na kwa kufanya hivyo watakuwa wanaungana na Rais wao Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye halali kwa ajili ya kuwaletea watanzania maendeleo.

Akitoa salamu za Mkoa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa ambaye alitarajiwa kuwa Mgeni rasmi wa tamasha hilo, Jabir Makame amesema pamoja na kwamba Mkuu huyo wa Mkoa ameshindwa kufika baada ya kuwa na majukumu mengine ya kiofisi hata hivyo amesema anafarijika na kazi nzuri inayofanywa na wanaGairo na anaomba ushirikiano wa wananchi wa Gairo ili kuendelea kufanya kazi kwa maendeleo ya wanaMorogoro.

Kwa upande wake Mratibu wa Sensa Mkoa wa Morogoro Charles Mtabo amesema maandalizi ya zoezi la sense kwa Mkoa wa Morogoro linaendelea vizuri na kubainisha kuwa Mkoa umeongezewa vishikwamba vingine zaidi ya elfu kumi ambavyo vitasaidia kila karani Mkoani humo kuwa na kishikwamba kwa ajili ya zoezi hilo muhimu.

Katika hatua nyingine viongozi wa vyama vya siasa Wilayani Gairo wameungana na viongozi wa chama Tawala, chama cha mapinduzi na wananchi wa Gairo kwa ujumla kushiriki tamasha hilo, akiongea kwa niaba ya chama chake Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo  (CHADEMA) Wilayani Gairo Bw. Ernest Bonifance Mkami amedai kuridhishwa na Serikali ya awamu ya sita kwa namna ambavyo imeshirikisha makundi mabali mbali kwenye jambo hilo la kimaendeleo.

“nimeona ni vema tushiriki zoezi hili la sense ya watu na makazi kwa kutambua kuwa jambo hili ni muhimu sana kwa taifa” amesema Bonifance Mkami.

“lakini sisi kama chama tumerishwa na namna serikali ilivyoshirikisha jamii na makundi mablimbali kushiriki kwa pamoja kuhakikisha Tanzania tunapata  idadi halisi ya wananchi ambayo ni muhim kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa jumla” amesisitiza Mwenyekiti huyo wa CHADEMA.

Zoezi la sense ya watu na makazi linatarajiwa kufanyika tarehe 23 mwezi Agosti mwaka huu.

SENSA KWA MAENDELEO, JIANDAE KUHESABIWA

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA AKEMEA ULANGUZI WA MAZAO.

    May 08, 2025
  • WAAJIRI MOROGORO WATAKIWA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WAFANYA KAZI WAO.

    May 01, 2025
  • SERIKALI KUJENGA BARABARA YA LUPILO – MALINYI KWA KIWANGO CHA LAMI, Bil. 18 ZATOLEWA KUJENGA MADARAJA MAWILI.

    April 25, 2025
  • MWENGE WA UHURU 2025 WATAJA TUNU NNE ZA TAIFA.

    April 19, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.