• Malalamiko |
    • Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
Mkoa wa Morogoro
Mkoa wa Morogoro

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Morogoro

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Maelezo ya Mkoa
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Sehemu na Vitengo
      • Utawala na Rasilimali
      • Serikali za Mitaa
      • Uhasibu na Fedha
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Sheria
      • TEHAMA
      • Afya
      • Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Kitengo cha Habari na Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Morogoro
    • Mvomero
    • Gairo
    • Kilosa
    • Kilombero
    • Ulanga
    • Malinyi
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Morogoro
    • Morogoro DC
    • Mvomero
    • Gairo
    • Ulanga
    • Malinyi
    • Mlimba
    • Ifakara Mji
    • Kilosa
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uchimbaji wa Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Kilimo
    • Huduma za Mifugo
    • Huduma za Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
    • Huduma za Ugavi
  • Machapisho
    • Miongozo Mbalimbali
    • Majarida
    • Fomu Mbalimbali
    • Ripoti mbalimbali
    • Mpango Mkakati
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Sheria Ndogo
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Videos
    • Hotuba
    • Picha

DC Mvomero awapongeza wananchi wa pemba kutoa maeneo kupunguza hewa Ukaa, asema hiyo ni biashara

Posted on: October 1st, 2023

Mkuu wa Wilaya ya Mvomero Judith Ngulli amewapongeza wananchi wa kata za Pemba, Diongoya na Kweuma Wilayani humo kwa kutoa mashamba yao 164 yenye ukubwa wa ekari 367.08 kwa ajili ya mradi wa urejeshaji hewa Ukaa unaoendeshwa na shirika lisilo la kiserikali la PAMS Foundation.

Mhe. Juditha amesema hayo Septemba 30,2023 wakati wa kukabidhi hatimiliki za kimila kwa wananchi 108 walioingia mkataba na shirika hilo la PAMS na mashamba hayo kutakiwa kupimwa na kuwamilikisha ili yaweze kutambulika kisheria.


Amesema, Ekari hizo 367.08 zitatumika kupanda miti itakayosaidia kurejesha uoto wa asili hivyo kupunguza wingi wa hewa ukaa hivyo amewapongeza na kubainisha kuwa kuyaingiza mashamba yao kwenye mradi huo ni kufanya biashara kama biashara nyingine itakayowaingizia kipato hapo baadae na kubadili Maisha yao kiuchumi.

Pamoja na shukrani hizo, amewataka wananchi hao kushika masharti ya mkataba walioingia na PAMS na kutotoa mashamba yao yote kwenye mradi huo ili maeneo yaliyobaki yatumike kwa matumizi mengine ya kiuchumi ikiwemo kilimo na kufuga.

Katika hatua nyingine Mhe. Judith amelitaka shirika la PAMS kuwalipa kwa wakati fedha wanufaika walioingia nao mkataba ili kuondoa migogoro inayoweza kujitokeza kwa kutotekeleza takwa hilo.

“cha msingi ni kuhakikisha malipo haya yanafanyika kwa wakati basi, hiyo lazima niwaagize PAMS, kwa wakati, ili tusiende kinyume na mkataba na ili msiwavuruge wananchi hawa” alisistiza Mkuu huyo wa Wilaya.

Mratibu wa Mradi wa PAMS ndugu Richard Paul alitaja faida za mradi huo kuwa ni Pamoja na wananchi kupatiwa hatimiliki za kimila ili kumilikisha maeneo yao, kutoa ajira zisizo za kudumu kwa vijana 150 na kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji sahihi wa mazigira.

Faida nyingine ni kurejesha uoto wa asili kwa mashamba ya wanufaika kwa kupanda miti ambapo mwaka 2022/2023 zaidi ya miti 200,000 ilipandwa na kupitia mradi huo Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imekusanya fedha zaidi ya shilingi 8,000,000/= kama ada ya  usajiri wa hati 164 zilizotolewa kwa wanufaika wa mradi.

Kwa upande wao wanufaika wa Mradi wa PAMS wakiwakilishwa na Mwenyekiti wao ndugu Omary Hamza Kivumbi wamekiri kuupokea mradi huo kwa moyo na kwa hiari yao huku Bi. Mariam Ally akiwataka wanawake wengine kuhamasika kuingia kwenye mradi huo kupata hatimiliki ili wasinyanyasike kwenye ndoa zao.

Shirika la PAMS Foundation lilisajiriwa mwaka 2009 na lilianza shughuli zake za uhifadhi katika Mkoa wa Ruvuma na baadae Mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Pwani, Manyara, Mbeya, Lindi, Dodoma, Tanga na Sasa Mkoa wa Morogoro.

Kwa Wilaya ya Mvomero Mradi huu upo katika vijiji vitano vya kata tatu za Pemba, Kweuma na Diongoya ambapo mradi umeanzia Kijiji cha Pemba ikiwa ni eneo ambalo linapatikana katika  hifadhi ya Msitu wa Mkingu uliopo katika safu za Milima ya Tao la Mashariki yaani (Eastern Arc Montains).

Lengo Kuu la mradi huu ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, kurejesha uoto wa asili kwa lengo la kupunguza wingi wa hewa ukaa na kuongeza kipato kwa wanufaika wa mradi kupitia miradi mingine kama kilimo Bora na chenye tija na kuunganishwa na masoko.

 

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA DARASA LA SABA 2024 October 30, 2024
  • TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. May 13, 2025
  • View All

Habari Mpya

  • RC MALIMA ASHIRIKI MATEMBEZI YA HISANI, ASEMA HOSPITALI YA RUFAA INAHIMILI WAGONJWA.

    May 17, 2025
  • VYAMA VYA SIASA NCHINI VYATAHADHARISHWA

    May 15, 2025
  • RC MALIMA ATAKA VYAMA VYA USHIRIKA VYA WAFUGAJI

    May 15, 2025
  • Vyama vya Ushirika Vyatakiwa Kutumia TEHAMA

    May 14, 2025
  • View All

Video

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima akikagua ujenzi wa jengo la ofisi mpya ya Mkuu wa Mkoa.
Video zaidi

Kurasa za Karibu

  • Maelezo ya Mkoa
  • Tangazo la Zabuni
  • Mkataba wa Huduma kwa Wateja
  • Hotuba
  • Taarifa kwa Umma

Kurasa Mashuhuri

  • Tovuti ya Tanzania
  • Wakala wa Serikali Mtandao
  • TAMISEMI
  • Ikulu
  • Katibu Mkuu Kiongozi
  • Tovuti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro

    Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO

    Simu: +2550232934305

    Simu: +255766828252

    Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.