Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka viongozi wa dini nchini kutoa Elimu ya lishe bora kwa waumini wao kwa lengo la kuhamasisha matumizi bora ya chakula na kuwa na afya bora ili kuleta maendeleo yao na taifa kiuchumi na kijamii.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel akiteta jambo na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa
Waziri Mollel amesema hayo Oktoba 29, mwaka huu wakati wa Maaadhimisho ya siku ya lishe kitaifa yaliyofanyika Mkoani Morogoro katika uwanja wa Mpira wa Fulwe Tarafa ya Mikese Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro.
Waziri akitembelea mabanda mbalimbali ya maonesho
Akitoa hotuba mbele ya mamia ya watu walioshiriki maadhimisho hayo Dkt. Mollel amesema kama nchi inataka kuwa na taifa la wasiopenda dhambi na kama linataka kuwa na taifa la wacha mungu ni lazima kushughulika na uwezo wa akili za watu huku akiwaomba viongozi wa Dini kuongelea suala la lishe wakati wa ibada zao.
“tunawaomba watumishi wa Mungu iwe ni mojwawapo ya Cullicullam yetu kuzungumzia lishe kanisani...kuna uhusiano mkubwa wa akili na kutenda dhambi..”.amesema Dkt. Mollel.
Awali akitoa tathmini ya Lishe kimkoa, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa amesema, Mkoa wa Morogoro unashika nafasi ya nne katika uzalishaji wa chakula hapa nchini, Pamoja na uzalishaji huo Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa kumi ambayo haifanyi vizuri katika masuala ya lishe bora.
“… Maadhimisho ya lishe kitaifa yanafanyika Mkoani Morogoro, nikili tu kwamba Morogoro ni miongoni mwa Mikoa kumi ambayo haijafanya vizuri katika suala zima la lishe..” amesema Fatma Mwassa.
Akibainisha hayo amesema udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano katika mkoa huo umefikia asilimia 26.4, upungufu wa damu kwa watu wenye umri kati ya miaka 15 hadi 49 ni asilimia 29.8 hivyo Mkoa upo miongoni mwa mikoa ambayo inatakiwa kusaidiwa katika kuboresha lishe ndani ya jamii.
Ili kukabiliana na udumavu huo na utapiamlo amemhakikishia Mgeni rasmi kuwa tayari amesaini mkataba wa lishe na wakuu wa Wilaya, na Wakuu wa Wilaya nao wamesaini mkataba huo na Wakulugenzi wa Halmashauri zote za Mkoa huo kwa lengo la kuboresha lishe.
Mwanamasumbwi maarufu kama Mandonga alikuwepo kuhamasisha kuhamasisha wananchi kula chakula chenye mchanganyiko kamili ili kuwa timamu zaidi kiakili na kimwili, huku akidai ngumi zake aina ya Ndoige zinatokana na Lishe Bora anayopata kwa kila siku. hapa anasalimiana na mgeni rasmi baada ya kusema neno kwa wananchi.
Akizungumzia juu ya jitihada za Serikali ya awamu ya sita katika kuimarisha sekta ya Afya, Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa Mkoa umepokea kiasi cha shilingi Bilioni 22 kwa ajili ya kuboresha huduma za afya katika Mkoa huo, huku hospitali ya Rufaa ya Mkoa imepokea zaidi ya shilingi Bilioni tatu kwa ajili ya kuboresha hospitali hiyo huku akibainisha kuwa mipango ya baadae ni kujenga jengo la ghorofa ambalo litatoa huduma zote.Mwisho ameendelea kutoa wito kwa wananchi kujiunga na bima ya afya kwa lengo la kupunguza gharama za matibabu.
Mwonekana wa vyakula mchanganyiko anaotakiwa binadamu kula ili kuepuka hali ya udumavu na utapiamlo
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollelna , Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Fatma Mwassa (kushoto) na Viongozi wengine wakishiriki kupika Uji wa Lishe wakati wa maadhimisho ya siku ya Lishe Kitaifa Mkoani Morogoro
Katika hatua nyingine Fatma Mwassa amewataka wadau wa lishe kujikita katika kutoa elimu ya lishe mashuleni kwa kutumia ujumbe mbalimbali kupitia tv “online’ kwa kufanya hivyo elimu ya lishe itawafikia wengi.
Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel (katikati) akicheza mziki aina ya singeli wakati wa maadhimisho hayo. kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa na kulia ni mwanamuziki anayejulikana kwa jina la Hamza maarufu kwa mziki huo wa singeli Mkoani humo.
Mandonga mtu kazi (mtoto wa nyumbani Morogoro) alikuwepo kwenye maadhimisho hayo
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mariam Nkuwa ameelezea kuwa wao kama wasimamizi wa utekelezaji wa sera na miongozo ya Serikali hapa nchini ikiwemo sera ya haki na ustawi wa jamii na lishe katika mamlaka za Serikali za mitaa, wameendelea kusimamia mikataba ya uboreshaji wa lishe bora kwa jamii katika ngazi mbalimbali kuanzia Vijiji, kata, mitaa, na hadi Mkoa.
mwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI Mariam Nkuwa akitoa taarifa fupi ya masuala ya Lishe kitaifa
Aidha, ameongezea kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI watahakikisha Halmashauri zinatengeneza shughuli zinazolenga kutoa elimu ya lishe kwa jamii na kuhakikisha fedha zote za lishe zinazohitajika zinaelekezwa katika kuwafikia jamii ili elimu ya lishe itolewe kwa jamii kupitia majukwaa mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa siku ya Afya na lishe ya Kijiji.
Maadhimisho hayo ya lishe ya kitaifa yalikuwa na kaulimbiu inayosema “Lishe bora ni msingi wa maendeleo endelevu, sote tuwajibike” ni ya tatu kufanyika tangu kuanzishwa kwake mwaka 2020.
Afisa Lishe Mkoa wa Morogoro Salome Magembe alishiriki kwa karibu maandalizi maadhimisho hayo, hapa ni kama anasisitiza ulaji wa vyakula mchanganyiko yaani Lishe Bora
Maadhimisho hayo yalikwenda sambamba na washiriki kunywa uji wa lishe wakati wa sherehe hizo
Burudani hazikukosekana
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Urio Kusirye (mwenye shati jeupe) akisikiliza kwa makini hotuba ya Naibu Waziri wa Afya
Baadhi ya wajumbe wa Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Morogoro
Wananchi walijitokeza kwa wingi na kupatiwa elimu mbalimbali zinazohusu Lishe Bora
MWISHO.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.