Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amewataka wakuu wa mikoa, viongozi wa Wilaya na Bodi za Mabonde ya Maji nchini kuhakikisha wanadhibiti uharibifu wa mazingira unaosababishwa na shughuli za kibinaadamu jambo ambalo amesema linachangia kwa kiasi kikubwa upungufu wa kina cha maji katika mito hapa Nchini.
Hapa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anasalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Fatma Mwassa kushoto kwake ni Mhe. Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango ametoa maagizo hayo Novemba 9, mwaka huu alipotembelea mitambo ya uzalishaji wa Maji Ruvu chini iliyopo mkoa wa Pwani na kisha kupokea taarifa ya hali ya uzalishaji na upatikanaji wa maji katika mikoa ya Dar es na Pwani.
Mhe. Fatma Mwassa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro akiteta jambo na mwenyeji wake Mhe. Abubakar Kunenge Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Mussa Ali Mussa pamoja na viongozi wengine wa mikoa ya Pwani, Dar es salaam na Morogoro.
Aidha, Makamu wa Rais ameitaka Wizara ya Maji kushirikiana na Tamisemi kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya uchimbaji wa visima vya maji na mabwawa ili kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji hapa nchini.
Sambamba na hayo Makamu wa Rais amekemea vitendo vinavyofanywa na baadhi ya wananchi wasiokuwa waadilifu wanaochoma misitu kwa ajili ya kuandaa mashamba huku akitoa wito kwa wananchi wote kuachana na tabia hizo za uchafuzi wa mazingira kando kando ya vyanzo vya Maji.
Wakuu wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro walishiriki kwa pamoja ziara hiyo ya Makamu wa Rais ambayo ilikuwa na lengo la kudhibiti uharibifu wa Mazingira unaendelea kujitokeza kutokana na shughuli za kibinadam hususan kando kando ya vyanzo vya maji na Mto Ruvu ambao ni tegemeo kubwa la upatikanaji wa Maji Katika Mikoa ya Pwani na Dar es Salaam.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.