GENERALI VENANCE MABEYO AMUAGA MKUU WA MKOA WA MOROGORO, AVITAKA VYOMBO VYA ULINZI KUSHIRIKIANA.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama hapa nchini Generali Venance Mabeyo amevitaka vyombo vya Ulinzi na Usalama kufanya kazi kwa kushirikiana zaidi ili kuliweka taifa hiki Katika hali ya amani na Usalama zaidi.
Generali Venace Mabeyo akizungumza na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Morogoro wakati wa ziara yake ya kumuaga Mkuu wa Mkoa huo Martine Shigela Juni 8 Mwaka huu, hafla iliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.
Generali Venance Mabeyo amesema hayo Juni 8 mwaka huu alipofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kuzungumza na baadhi ya Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama Mkoani humo akiwa Katika ziara yake ya kuaga kutokana kukaribia kustaafu utumishi wa Umma ifikapo mwishoni mwa mwezi Juni mwaka huu.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Venance Mabeyo wakati wa ziara ya Mkuu huyo wa Majeshi ya kumuaga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Juni 8 Mwaka huu.
Aidha, Generali Mabeyo amemhakikishia Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela kuwa pamoja na kustaafu huko yuko ataendelea kushirikiana na Serikali na kutoa ushauri kuhusu masuala ya Ulinzi na Usalama kulingana na uzoefu wake na atafanya mara atakapohitajika.
Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama wa Mkoa wa Morogoro wakisalimiana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama Generali Venance Mabeyo alipowasili katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Juni 8 Mwaka huu.
Sambamba na hayo, Generali Mabeyo ameshauri kuwa Sasa umefika wakati ambapo maeneo yote yanayomilikiwa na jeshi lolote ambayo bado hayana hati miliki yaanze kutafutiwa hati hizo ili kukomesha migogoro ya Ardhi inayojitokeza Mara kwa Mara baina ya majejeshi na wananchi wanaozunguka huku ikidhaniwa kuwa majeshi hayo ndiyo yanavamia maeneo Jambo ambalo sio sahihi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela amempongeza Generali mabeyo namna alipofanya kazi yake kwa weledi na kwamba tangu ashike wadhifa huo Hali ya Ulinzi na Usalama nchini umeimarika zaidi. Aidha amempongeza kwa namna alivyokuwa mbunifu na kuhakikisha Kesho Hilo linakuwa tegemeo kwa Serikali kwenye masuala ya ujenzi wa majengo kupitia SUMA JKT.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela akizungumza na wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakati wa ziara ya Mkuu wa Majeshi hayo Generali Venance Mabeyo ya kumuaga Mkuu wa Mkoa huyo Juni 8 Mwaka huu.
Generali Venance Mabeyo ameendelea na ziara yake ya kuaga viongozi wengine katika maeneo mengine kabla ya kustaafu kwake utumishi wa umma ambapo kwa mujibu wa maelezo yake ametumikia taifa hili kwa zaidi ya miaka arobaini.
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Martine Shigela (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Generali Venance Mabeyo (wa sita kushoto), Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt Rozalia Rwegasira (wa tano kushoto) na wakuu wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.