NI MAONESHO YA UTALII NA UWEKEZAJI YANAYOENDELEA KUFANYIKA KATIKA VIWANJA VYA MAONESHO VYA KIHESA KILOLO – IRINGA, 2022.
Maonesho hayo yenye kauli mbiu “Utalii na Uwekezaji Kusini Fahari Yetu” ni maonesho ya pili yenye hadhi ya kimataifa yenye lengo la kutangaza fursa za Utalii na Uwekezaji katika mikoa ya kusini mwa Tanzania hivyo kukuza sekta hiyo kama inavyotiliwa mkazo na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususan baada ya kuanzisha filimu yake ya Royal Tour.
Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga akitembelea mabanda ya maonesho ya Halmashauri za Mkoa wa Morogoro.
Mikoa hiyo ni pamoja na Mkoa wa Njombe, Iringa, Mkoa wa Morogoro na Mbeya. Mingine ni Mkoa wa Katavi, Rukwa Songwe, Ruvuma, Lindi na Mkoa wa Mtwara.
Mkoa wa Morogoro ni miongoni mwa Mkoa ambao pia umeshiriki kikamilifu maonesho ya Utalii na Uwekezaji kwa mwaka huu 2022.
Saida Mahuga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga.
Baadhi ya viongozi kutoka Morogoro akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kilosa Alhaji Majid Mwanga na Saida Mahuga Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ulanga wametembelea mabanda ya maonesho ya halmashauri za Mkoa wa Morogoro na kujionea bidhaa na vivutio mbalimbali vinsavyooneshwa katika mabanda hayo.
Kivutio cha kiubunifu katika maonesho ya Utalii kanda ya Kusini.
MWISHO
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Morogoro
Sanduku la Posta: S.L.P 650 MOROGORO
Simu: +2550232934305
Simu: +255766828252
Barua pepe: ras.morogoro@tamisemi.go.tz
Haki Miliki © 2024 Ofisi Ya Mkuu wa Mkoa Morogoro. Haki Zote Zimehifadhiwa.